I DIED TO SAVE PRESIDANT
Sehemu 57
Baada ya kuachana na akina
Patricia,Meshack Jumbo akaelekea
moja kwa moja katika makazi ya
Elvis ambako alikaribishwa na
Graca na baada ya muda mfupi
Elvis akatoka wakasalimiana
"karibu mzee"
"Ahsante Elvis.Poleni kwa
shughuli ya usiku kucha"
"Ahsante mzee" akajibu Elvis
"Umekutana na Patricia?
"Ndiyo nimeonana naye"
"Anaendeleaje? Ni rahsi sana kusema
anaendelea vyema kwa
kumtazama lakini hatuwezi kujua
ndani ya moyo wake maumivu
anayokutana nayo ila yule
mwanamke ni jasiri
sana.Anajitahidi kukubaliana na
hali halisi ilivyo ili maisha yaende
mbele"
"dah ! Nimemuumiza mno
Patricia.Maisha yake hayatakuwa
sawa tena"akasema Elvis
"Nilijaribu kumgusia kuhusu
suala la kufungua mirathi lakini
amekataa kabisa na ameelekeza
suala hilo aachiwe mama yako.Ni
jambo gani baya ambalo ndugu
zako walimfanyia na kumfanya
asihitaji kitu chochote cha kwako? Ninaamini kuna mambo
alikuwa anafanyiwa na ndugu
zangu ila hakuwa
ananieleza.Nafahamu manyanyaso
aliyokuwa anayapata toka kwa
ndugu zangu wakitaka mtoto
lakini inaonekana kuna mengi
zaidi alikuwa ananificha.Natamani
hata leo hii niibuke na kumchukua
mke wangu twende mbali
tukaishi.Inaniumizz mno
anavyoteseka"
"Usihofu Elvis na wala usiwe
na wazo hilo la kuitaka kuibuka
kwani utafanya mambo yawe
magumu zaidi.Mimi nipo na
nitahakikisha Patricia anakuwa na
maisha mazuri yenye furaha"
Elvis akazama kidogo katika
tafakari halafu akaulizaMzee sifahamu operesheni
hii itachukua muda gani.Ni vipi
kama Patricia ataamua kuwa na
mwanaume mwingine?
"Elvis kijana wangu naomba
nikuweke wazi bila kukuficha
kwamba matumaini ya wewe na
Patricia kurudiana ni asilimia
ndogo mno au naweza kusema
kwamba safari yenu imeishia
hapa.Hakuna namna unayoweza
ukajitokeza tena kwa Patricia na
kudai kwamba hukuwa
umekufa.She'll never trust you
again.Kwa sasa weka pembeni
mawazo kuhusu Patricia I need
you to focus in your
mission.Mambo ya kuhusu
Patricia yatajulikana baada ya
operesheni kumalizika.Umenielewa Elvis?
akauliza Meshack
"Nimekuelewa mzee"
"Good.Nipe taarifa za jana
usiku" akasema Meshack na Elvis
akamsimulia kila kitu kuhusu
Vicky
"Do you trust her? akauliza
Meshack baada ya kuhadihiwa
kila kilichotokea
"yes I do trust her"akajibu
Elvis
"Vizuri kama umemuamini na
unaona anaweza kuwa na msaada
kwetu mimi sina tatizo.Mjumuishe
katika timu yetu,wewe ndiye
nahodha wa jahazi hili hivyo
siwezi kukuingilia katika
kuliongoza ninachoweza kufanya
mimi ni kutoa tu ushauri.Umekwisha wasiliana na
Steve kama tayari amefika
numbani kwa Vicky?
"Amenipigia simu dakika
chache kabla hujafika hapa na
kunijulisha kuwa anaweza
akachelewa kufika kwa Vicky
kwani njia aliyopita kuna ajali
imetokea hivyo gari zimesimama
na foleni ni ndefu sana"
" Anatakiwa kufanya kila
awezalo ili kumuwahi Vicky.She's
in danger.Nimepewa maagizo na
makamu wa rais kwamba
akamatwe na awekwe sehemu
fulani kuna mtu anataka kumuhoji
na baada ya hapo auawe kwani
tayari amekwisha anza kuwa
tishio kwao"Amefahamuje kama Vicky
alikuwepo eneo la tukio wakati
Pascal anauawa? akauliza Elvis
"Hata mimi
nashangaa.Kwanza aliponipigia
aliniuliza kama ninamfahamu
Vicky nikamuuliza ni Vicky yupi
anayemzungumzia akanifafanulia
kwamba kuna mwanamke
anaitwa Vicky ambaye
anahusishwa na kifo cha Pascal
akataka kujua kama Vicky ni mtu
wangu ambaye nilimtumia katika
kumuua Pascal nikamweleza
kwamba simfahamu huyo Vicky
ila yawezekana alitumiwa na
vijana wangu ili kuweza kumpata
pascal kirahisi ndipo akasema
kwamba anataka Vicky apatikane ahojiwe na baadae auawe kwani
tayari ni mtu hatari kwao."
"Vicky ndiye aliyempigia simu
Pascal na kumuomba waonane
pale hotelini yawezekana
wamefanya uchunguzi wa
mawasiliano ya Pascal na
wakagundua kwamba Vicky ndiye
aliyemtaka Pascal afike pale
hotelini na
akauawa.Kinachonishangaza ni
kwamba hawa jamaa walitaka
pascal auawe sasa wana wasiwasi
gani tena?
"Wasi wasi wao ni kuhusu
huyo Vicky kuhusika katika kifo
cha Pascal"akajibu Meshack
"Vicky ni mshirika wa Frank
na Pascal na ndiye walimtumia
kumuua kanali Norman.Kwa nini sasa wawe na wasiwasi?Anyway
tuliache kwanza suala hili
tutajadiliana na Vicky pale
atakapofika hapa.Patricia alikuwa
na shida gani? akauliza Elvis
"Patricia hakuwa na tatizo
lolote kubwa,alitaka tu kufahamu
kama tayari uchunguzi wa
kuwabaini wale waliosababisha
kifo cha mumewe umekwisha
anza nikamuhakikishia kwamba
uchunguzi mkali unaendelea hivi
sasa"
"Only that? akauliza Elvis kwa
mshangao
"Haikuishia hapo.Patricia
alikuwa ameongozana na dada
yake anaitwa Juliana"
"Ninamfahamu Juliana ni mtu
wa karibu sana naye na kwa sasa ndiye aliyemchukua anaishi
kwao"akasema Elvis
"Huyo Juliana ndiye
aliyekuwa na tatizo na Patricia
alimleta kwangu kwa ajili ya
kumpatia msaada "Ana tatizo gani
Juliana? akauliza Elvis na Meshack
akamueleza kila kitu alichoelezwa
na Juliana
"Oh my God!! akasema Elvis
baada ya Meshack kumaliza
kumsimulia mkasa wa Juliana
"Elvis,mbona
umestuka?akauliza Meshack
"Sijastuka mzee ila ninapatwa
na wasi wasi mkubwa kwa
Patricia kuendelea kuishi
pale.Yuko katika hatari.Kuna kila
sababu ya kuamini kwamba
familia hii ya akina Juliana inawindwa na mtu au kikundi cha
watu na hivyo kumfanya mke
wangu awe katika hatari kubwa
endapo kuna lolote
litatokea.Meshack we have to get
her out of there.Patricia hatakiwi
kuendelea kukaa pale kwa akina
Juliana ni sehemu hatari sana
kwake"
"Hata mimi nimeliona hilo na
nitajaribu kumueleza Patricia ili
aweze kuondoka na kutafuta
sehemu nyingne ya
kuishi.Nitamtafutia makazi
mengine.Kuna nyumba
zinapangishwa kule maeneo ya
Peninsula nitamfanyia mpango ili
aweze kupata nyumba moja aishi
kwa wakati ambao tunaangalia
namna ya kumtafutia nyumba yake mwenyewe ili maisha yake
yaweze kuendelea kama kawaida"
"Ahsante sana kwa hilo mzee
naomba lifanyike kwa haraka"
"Nitalitekeleza hilo usijali."
"Good.Sasa umeamua nini
kuusu suala hili la Juliana?
"Bado sijaamua chochote kwa
sasa kwani bado kuna kazi kubwa
inatukabili mbele yetu hivyo sitaki
kuchanganya mambo.Tumalize
kwanza suala hili la mtandao wa
silaha halafu tutamsaidia
Juliana.Au wewe
unasemaje?akauliza Meshack
"Wazo lako si baya
mzee.Tuna suala kubwa mbele
yetu lakini hata hivyo bado
tunaweza kumsaidia Juliana
pia.Tunaweza kuzungumza naye na kupata picha halisi ya suala
lake na pale tutakapokuwa
tumemaliza operesheni yetu
tuanze kulifuatilia suala lake.Steve
na Vicky wanaweza wakamuhoji
Juliana ili tuone ni wapi pa
kuanzia.Nataka ukaribu na Juliana
ili iwe raisi kwetu kujua
maendeleo ya Patricia"
"Elvis huoni kama tutakuwa
tunaongeza kazi nyingine hasa
kwa wakati huu ambao
tunakabiliwa na jukumu zito
ambalo ndilo kwanza limeanza
kushughulikiwa?Ninao vijana
wengi pale ofisini ninaweza
kuwapa kazi hiyo wakaifanya na
ninyi mkaendelea na kazi moja ya
kuufumua mtandao huu wa kuuza
silaha" Hapana mzee tuachie sisi
suala hili tutalifanya
wenyewe.Juliana ni mtu wa karibu
sana na Patrcia hivyo suala lake
linapaswa kushughulikiwa kwa
uzito mkubwa sana.Ni mtu
ambaye anaweza kumsaidia sana
Patricia na hata baadae
operesheni itakapokuwa
imekwisha anaweza akanisaidia
kurejesha tena mahusiano na
Patricia.Usijali mzee tutajipanga
kufanya kazi zote mbili"
"Una hakika Elvis?
"Ndiyo mzee ondoa hofu"
"Sawa.Nataka kufahamu
kuhusu namna mlivyojipanga
kuiendesha operesheni hii ya
kuubaini mtandao wa akina
Frank" Kwanza tunataka
kuwachunguza Frank na makamu
wa rais.Kupitia hawa wawili
tunaweza kuufahamu ukubwa
mtandao wote wa kuuza
silaha.Tayari Vicky amekwisha
zungumza na rafiki yake yuko
nchini Afrika kusini na
amemuomba aje atusadie na
tunasubiri jibu lake na endapo
akikubali nitakufahamisha mara
moja.Anaitwa Omola
Otola.Atajifanya ni mwandishi wa
habari za mazingira na kwa kuwa
ofisi ya makamu wa rais ndiyo
inashughulika na mazingira
itakuwa rahisi sana kumchunguza
Dr Shafi.Vicky atazungumza na
rais na kumjulisha kwamba
anataka kumchunguza makamu wa rais na rais atafanya mpango
ili kuwe na ukaribu kati ya
makamu wa rais na Omola.Vicky
yeye atamchunguza Frank kwani
wana ukaribu mkubwa.Kupitia
wawili hawa kuna mambo
tutayafahamu kuhusu mtandao
huu mkubwa.Kuna mtu ambaye
anaonekana ni kinara katika huu
mtandao anaitwa Deusdedith
ambaye Vicky amewahi kuwa na
ukaribu naye na kumchunguza
lakini hakuwahi kuambulia
chohiote kwani ni mtu makini
sana anayejua kujificha.Huyu naye
tunamtafuta na tuna imani
tukimchunguza Frank tutafahamu
mengi kuhusu Deus.Ndani ya
muda mfupi ujao kutakuwa na
hatua kubwa imepigwa katikakuwabaini watu hawa na na
namna wanavyofanya biashara
yao ya silaha"
"Ni mpango mzuri ila nina
ushauri mdogo.Huyu Vicky kama
anaripoti kwa rais asithubutu
kuweka wazi kwamba
anashirikiana nanyi.Hili ni suala la
siri sana"
"Tumekwisha liona hilo na
kumuonya asithubutu kufanya
hivyo" akasema Elvis
"Good.Nimeridhiswa na
mpango huo.Fanyeni kila
muwezalo kuikamilisha
operesheni hii muhimu sana kwa
taifa letu.Muda wowote kama
kuna lolote ambalo
mtahitaji,mnijulishe na mimi
nitakikishaninalifanikisha.Nitakuja tena jioni
ya leo ili kwa pamoja tujadiliane
namna ya kulishughulikia suala la
Juliana.Kuhusu Patricia
nitashughulikia nyumba kama
nilivyokuahidi ili aweze kuondoka
pale kwa akina Juliana.Mambo
yote haya tutakuja kufahamishana
jioni nimefikia wapi"
"Ninashukuru sana mzee"
akasema Elvis na mzee Meshack
Jumbo akaondoka kwenda
kuendelea na majukumu mengine
"Patricia kuendelea kukaa
kwa akina Juliana ni hatari kubwa
kwake na kama ningekuwa na
uwezo ningekwenda sasa hivi
kumtoa lakini ngoja nifuate
ushauri wa mkurugenzi.Mimi
ndiye chanzo cha Patricia kuingiakatika hatari hii.Kama
nisingefanya jambo hili la
kudanganya kifo changu haya yote
yasingemkuta.Kuna nyakati
najiona sijafanya jambo sahihi
lakini nikikumbuka namna ndugu
zetu wanavyouliwa na waasi
wanaopata silaha kutoka kwa
akina Frank najiona nimefanya
kitu sahihi.Frank na genge lake
ndio waliosbabisha haya na
ninaapa lazima watalipa" akawaza
Elvis na kuchukua simu akampigia
Steve.Simu ikaita kidogo na
kukatwa.Akajaribu tena kupiga
haikuwa ikipatikana.Elvis
akaingiwa na wasiwasi Hatimaye askari wa usalama
barabarani walimaliza kupima
kufuatia ajali iliyokuwa imetokea,
magari yaliyokuwa yamegongana
yakaondolewa na gari zikaanza
kwenda.Ulikuwa ni msururu
mrefu sana wa magari yaliyokuwa
yamekwama katika barabara hii
na Steve akiwa ni mmoja wao
akielekea nyumbani kwa
Vicky.Kila wakati alikuwa
anatazama saa yake na tayari
ilikwisha fika saa tatu na dakika
kumi na nane
"Ningejua kama yangetokea
haya nisingepita barabara
hii.Nilitakiwa kuwahi sana
nyumbani kwa Vicky.Ajali ile
imenichelewesha sana na
nisingeweza kuondoka na kulitelekeza gari barabarani
lingeleta usumbufu kwa wengine
na hata kuibiwa.Nitajitahidi
kupita barabara za vichochoro ili
nifike kwa haraka.Kama kuna
hatari yoyote itakuwa imetokea
siwezi kujilaumu sana kwani
sikuwa na namna nyingine ya
kunifikisha kwa haraka" akawaza
Steve na kutolewa mawazoni
baada ya simu yake kuita
.Akatazama mpigaji alikuwa
Samira.Kwa kuwa gari lilikuwa
linakwenda taratibu kutokana na
wingi wa magari akaipokea
"Hallow baby summer"
"Steve kulikoni hadi mida hii
hujanipigia simu?Umenogewa na
Vicky? Si hivyo mpenzi wangu ni
kutingwa tu na kazi.Hivi sasa niko
barabarani nitakupigia baadae
tutazungumza"
"Sawa Steve je ulifanikiwa
kupata ulichokuwa unahitaji?
"Nilifanikiwa na Vicky
niliachana naye usiku ule ule"
"Kweli?
"Kweli kabisa Samira"
"Niambie uliitimiza ahadi
uliyonipa? akauliza Samira
"Ahadi ipi Samira?
"Tulikubaliana kwamba
hautafanya mapenzi na Vicky"
"Ouh! Usihofu kabisa kuhusu
hilo baby summer.Mimi shida
yangu ilikuwa ni taarifa tu na si
mapenzi.Kama ni mapenzi
ninayapata kwako tu kwani hakuna wa kufikia kiwango
chako.Nitawasiliana nawe baadae
kidogo nitakapokuwa nimetulia
kwa sasa niko barabarani"
akasema Steve ana kuagana na
Samira
"Nilimuahidi Samira kwamba
nisingefanya chochote na Vicky
lakini sikuitimiza ahadi
hiyo.Samira mwenyewe
anafahamu ugonjwa wangu ni
wanawake wazuri sasa
ningewezaje kumuacha mrembo
kama Vicky?Daah ! mwanamke
yule ni mjuzi sana kitandani na
ukichanganya na uzuri wake ndo
balaa kabisa utajiona kama uko
anga za mbali.Japo tulifanya kwa
muda mfupi lakini nilipata raha ya
ajabu sana.Baada ya mambo kumalizika lazima nitafute wasaa
niweze kujivinjari naye tena
kiumbe yule asiyeisha utamu"
akawaza Steve na kutabasamu
"Elvis amekuwa ananiusia
kila mara kwamba siku zote
nisiwaamimi wanawake wazuri
kwani wanaweza kunitoa uhai na
hii ndivyo ilivyotokea kwa
Vicky.Katu huwezi kudhani kuwa
ni mpelelezi.Watu wanamchukulia
kama kahaba kumbe mwenzao
yupo kazini.Vigogo
wanampapatikia huku
wakimwaga mahela yao kumpata
hawajui kama anawachunguza.
Safari hii kifaranga katua katika
miguu ya mwewe.Nitachagua
nimlie angani au ardhini" akawaza Steve huku akitabasamu kwa
mbali.
Ilmchukua takribani saa moja
kufika nyumbani kwa
Vicky.Hakukuwa na mlinzi nje
akapiga honi ili kumstua afungue
geti lakini zikapita dakika mbili
bila mlinzi au mtu yeyote
kutoka.Steve akafungua mlango
wa gari na kushuka akatemea
taratibu na kwa tahadhari hadi
getini akachungulia katika dirisha
dogo la chumba cha walinzi lakini
hakukuwa na mtu.Akatazama kila
upande kuona kama kuna mtu
maeneo yale ya karibu,hakukuwa
na mtu aliyemtilia maanani zaidi
ya wapita njia.Akausukuma
mlango mdogo wa geti
ukafunguka haukuwa umefungwa akaingia ndani taratibu na kwa
tahadhari kubwa.Nyumba ilikuwa
kimya na hakukuwa na dalili za
kuwepo mtu.Ndani aliyaona
magari mawili.Moja ni lile ambalo
Vicky aliondoka nalo na halafu
kukawa na gari lingine jeupe.
"Vicky aliondoka na lile gari
letu hii ina maana kuwa yupo
ndani.Yawezekana amepumzika
na hataki usumbufu hata hivyo
huu ukimya mbona kama si wa
kawaida?Hakuna mlinzi wala mtu
yeyote humu ndani? akawaza
Steve na kusogea taratibu hadi
katika gari la kwanza jeupe
lililokuwa na vioo vyeusi
akachungulia ndani hakukuwa na
mtu akatembea taratibu kuelekea
katika mlango mkuu wa kuingilia sebuleni.Kabla hajafika mlangoni
akasikia sauti ikiuliza kwa ukali
"Una hakika hakuna wengine
humo ndani?
"Hakuna mkuu nimepitia
vyumba vyote hakuna mwingine
ni hawa tu" ikajibu sauti nyingine
"Sawa.Nenda nje kahakikishe
hakuna anayeingia humu
ndani.Mimi nitamalizana na
hawa.Una hakika wote
umewafunga vizuri?
"Ndiyo mkuu wote
wamefungwa vizuri"
"Good.Nenda nje" ikasema ile
sauti kali na haraka sana Steve
akajibanza pembeni ya mtungi
mkubwa wa maua ambao
haukuwa mbali sana na mlango na
taratibu akaitoa bastora yake kwani alikwisha ng'amua hatari
iliyopo.Katika mlango mkubwa wa
kuingilia sebuleni kijana mmoja
aliyevaa fulana nyeupe na suruali
ya jeans ya rangi ya bluu na koti la
rangi ya kahawia akatoka akiwa
ameshika bastora mkononi.Usoni
alikuwa amevaa miwani myeusi
na kichwani alikuwa na kofia
nyeusi pia.Aliangaza pande zote
kuhakiki usalama kisha akaanza
kupiga hatua kwa tahadhari
kuelekea getini.Alipita katika
chungu alichokuwa amejibanza
Steve na alipompita kama hatua
nne simu ya Steve ikaita,kwa
haraka sana akaikata na kuizima
kabisa.Yule kijana alistuka
aliposikia mlio ule wa simu
akageuka na kukutana na kitu ambacho hakuwa
amekitegemea.Alikuwa
anatazamana na mtu mwenye
sura yenye kuonyesha hamu ya
kutoa roho ya mtu.Steve akaweka
kidole mdomoni ishara ya
kumtaka yule jamaa anyamaze
kimya halafu akamfanyia ishara
atupe chini bastora yake na kisha
aanze kutembea kuelekea
getini.Yule kijana hakuwa mbishi
akaitupa chini bastora yake
akaanza kupiga hatua kuelekea
getini.Steve akaiokota bastora ya
yule jamaa na kuifutika kiunoni na
kumfuata nyuma akiwa katika
tahadhari kubwa,akamuamuru
aingie katika kile chumba kidogo
cha walinzi na kumtaka apige
magoti Brother naonba usiniue
mimi sifahamu
chochote"akajitetea yule kijana
"Ninyi ni akina nani na
mmefuata nini hapa?Steve
akauliza
"Mimi sifahamu chochote
brother naomba uniamini"
akasema yule kijana na Steve
akiwa katika sura inayotisha
akaiweka sawa bastora yake na
kumlenga yule jamaa kichwani
"Kijana naomba unitazame
vizuri machoni sina muda wa
kupoteza na mimi kazi yangu ni
kuua hivyo usiponijibu kwa
ufasaha ninachokuuliza
nitausambaratisha ubongo
wako.Nakupa sekunde tano unieleze ninyi ni akina nani na
mnatafuta nini hapa?
"Nitakueleza brother
tafadhali naomba usinidhuru"
akasema yule kijana kwa woga
"Kama nilivyokwambia mimi
sifahamu chochote
nimechukuliwa na Obi
ameniambia kwamba kuna kazi ya
kufanya na tukaja
hapa.Hajanieleza chochote zaidi
ya kuvamia hapa na kuwakusanya
watu wote sebuleni ambako ndiko
aliko yeye na mimi amenitoa kuja
kuangalia ulinzi"
"Mko wangapi?
"Tuko wawili tu mimi na Obi"
akasema yule kijana
"Nani kawatuma? Sifahamu chochote
brother.Obi ndiye anayefahamu
kila kit......" hakumaliza sentensi
yake Steve akampiga teke kali
lililomrusha hadi ukutani
akajibamiza na kutoa mguno wa
maumivu.Akamfuata pale chini
alipokuwa ameangukia akivuja
damu mdomoni akampiga teke
lingine kali la uso na yule kijana
akapoteza fahamu
"Nina hasira sana nanyi,tena
una bahati nina haraka ya kwenda
ndani kumuokoa Vicky vinginevyo
ningekumwaga ubongo wako"
akasema Steve kwa hasira na
kutembea kwa tahadhari kuelekea
sebuleni.Alinyata na kuukaribia
mlango na kuangaza kila upande kuhakiki kuwa hakuna mtu
mwingine.
"Nahitaji kujua namna
walivyokaa huko ndani ili nijue
namna ya kumkabili huyo shetani
ndani" akawaza Steve na kusogea
kuelekea katika
dirisha.Akachungulia ndani na
mtu wa kwanza kumuona alikuwa
ni Vicky akiwa amefungwa
mikono kwa nyuma amepiga
magoti.
"Nieleze unashirikiana na
akina nani?sauti kali ya yule jamaa
kule ndani ikauliza lakini Vicky
hakujibu kitu na yule jamaa
akamsogelea na kumpiga teke kali
lililompeleka hadi chini.Steve
alikiona kitendo kile akauma
meno kwa hasira Huyu jamaa hana habari
kama ziraili yuko hapa nje
akisubiri kuichukua roho yake"
akawaza Steve na kuanza
kuusogelea mlango.Wakati
akinyata kuelekea mlanoni
akagonga kopo.
"Gabi !! akaita yule jamaa
aliyeko ndani lakini hakujibiwa
"Mambo yameharibika"
akawaza Steve na kujiweka tayari.
"Gabi !! yule jamaa akaita
tena na aliposikia kimya akatoka
taratibu ili kuchungulia na ghafla
akapigwa teke kali la uso
lililomrusha ndani.Kwa wepesi wa
aina yake Obi akajigeuza na
kuruka sarakasi halafu akatua
chini kwa ufundi mkubwa na
kuachia risasi kuelekea mlangoni alikokuwa amesimama
Steve.Risasi toka katika bastora ya
Obi ikamchubua Steve begani na
kumuangusha.Obi akasimama
lakini kabla hajafanya chochote
Vicky kwa kutumia miguu yake
akajigeuza na kumkata mtama
akaanguka.Steve akasimama ili
kumuendea Obi pale chini
alipoangushwa lakini Obi alikuwa
mwespi sana alimuona na
akaiwahi bastora yake akaachia
risasi mfululizo.Kwa jicho kali
kama tai Steve alikiona kidole cha
Obi kikiizinga bastora hivyo
akaruka katika korido na
kunusuru maisha yake,akaingia
katika chumba cha chakula.Obi
akainuka haraka haraka na kutoka
kwa kasi ya mshale akakimbia Steve!! akaita Vicky kwa
sauti kubwa na baada ya muda
Steve aliyekuwa amechafuka
damu akajitokeza.
"Are you ok? Steve
akamuuliza Vicky
"Amekimbia,go after him !!
akasema Vicky na Steve akatoka
nje na kuliona gari jeupe
likimalizika kutoka
getini.Akakimbia hadi katika
kibanda cha walinzi lakini yule
jamaa aliyekuwa amempoteza
fahamu hakuwemo.
"Bastard !! akasema kwa
hasira halafu akarejea ndani
"We lost them.Wamekimbia"
akasema huku akianza
kuwafungua Vicky na wenzake waliokuwa wamefungwa mikono
kwa nyuma
"Nyote mko
salama.Hawajawaumiza? akauliza
Steve
"Hapana
hawajatuumiza.Umefika kwa
wakati muafaka sana kwani
alikuwa anaanza kunihoji.Ahsante
sana Steve kwa
kutuokoa.Umejuaje kama niko
katika hatari? akauliza Vicky
"Vicky tutazungumza kuhusu
hilo lakini nataka kufahamu yule
jamaa ni nani?Unamfahamu?Steve
akauliza
"Hapana simfahamu.Ni mara
ya kwanza leo kumuona.Nikiwa
chumbani ninajipumzisha mlango
wangu ukagongwa nilipokwenda kuufungua nikajikuta
nikitazamana na bastora hivyo
sikuwa na ujanja tena zaidi ya
kufuata walivyotaka wale jamaa"
"Vicky hatuna muda wa
kupoteza.Jiandaeni chukueni
baadhi ya vitu vyenu vichache
tunaondoka"
"Tunakwenda wapi? akauliza
Vicky
"At our place.Hapa si sehemu
salama kwenu kwa sasa"akasema
Steve na kutoka nje Vicky na
Winnie wakainuka wakaelekea
chumbani.Steve akamtazama kwa
hasira mlinzi aliyekuwa amekaa
chini akitafakari.Alikuwa ameloa
jasho mwili mzima.Tukio lile
lilimuogopesha mno.Inaonekana hajawahi kukumbana na tukio
kama lile.
"Na wewe mni mlinzi wa aina
gani?Ilikuaje ukakamatwa kirahisi
na wale jamaa?Hujapitia mafunzo
maalum ya kujihami?akauliza
Steve kwa ukali
"Nimepitia mafunzo kaka
lakini wale jamaa ni wataalamu
sana kwa namna walivyoweza
kunidhibiti hata mimi nashangaa"
"Natamani nikuchape vibao
kwa uzembe huu mkubwa
ulioufanya.Wewe umewekwa
hapa ili kuwalinda hawa watu
lakini wavamizi wamevamia kana
kwamba hakuna mlinzi. Hufai
kabisa kufanya kazi hii.Kumlinda
mtu unayatoa maisha yako kwa
ajili yake.Unatakiwa kupambana hata ikibidi kupoteza maisha
kumuokoa mtu unayemlinda
kuliko kukubali kukamatwa
kizembe namna hii!! akasema
Steve kwa ukali
"Nisamehe brother.Naomba
taarifa hizi zisifike kwa wakuu
wangu.Nitajitahidi sana kuwa
makini katika kazi" akajitetea yule
mlinzi ambaye miguu yake ilikosa
nguvu.Steve akamtaka ainuke
haraka atoke mle sebuleni
"Dada yule jamaa
aliyetuvamia ni nani? Naomba
unijibu ama sivyo sintaondoka
hapa"akasema Winnie wakiwa
chumbani kwa Vicky
"Winnie tuko katika hatari
kubwa hivi sasa na hawa jamaa wananitafuta kufuatia tukio
lililotokea jana"
"Unakiri kuwa jana umeua
mtu? Kwa nini?Unajihusisha na
mambo gani mabaya dada?Huoni
kuwa unaniweka katika matatizo
makubwa hata mimi?akauliza
Winnie .Vicky akamshika mkono
akamketisha kitandani
"Hatuna muda wa kutosha
lakini itanilazimu nikueleze japo
kwa ufupi na ninakuomba
uniamini na ufuate yale
nitakayokuelekeza"akasema Vicky
halafu akavuta pumzi ndefu
"Mimi ni mpelelezi"
"What? akauliza Winnie kwa
mshangao
"Shhhhhh!! Vicky akamfanyia
ishara anyamazeMimi ni mpelelezi wa
siri.Sikuwahi kukueleza kuhusu
jambo hili kwa ajili ya usalama
wako.Kwa sasa kuna jambo
ninalichunguza na ndiyo maana
yakatokea yale yaliyotokea jana
na hawa jamaa kuanza
kunifuatailia.tayari wanafahamu
kuwa nimehusika katika kifo cha
Pascal na wanaanza
kunitafuta.Wanataka kujua kwa
nini ndiyo maana wakamtuma
yule jamaa kutuvamia lakini
imekuwa bahati Steve amefika
kwa wakati akatuokoa.Tupatapo
nafasi nitakueleza zaidi kila kitu
na kwa nini ninaifanya kazi
hii.kwa sasa nakuomba ujiandae
tuondoke kwani hapa si salama sana kwetu kwa sasa" akasema
Vicky
"Kwa nini ukanificha
hukunieleza muda huu wote kama
wewe ni mpelelezi?Huniamini
hadi ukanificha?Winnie akauliza
"Winnie sikukueleza chochote
kuhusiana na jambo hili kwa ajili
ya kukulinda.Sikutaka kukuingiza
katika hatari.Naomba tuokoe
muda Winnie,jiandae tuondoke"
akasema Vicky
"Tunakwenda wapi?Huko
tuendako hao jamaa hawataweza
kutufuata?Winnie akauliza
"Winnie naomba uniamini
dada yao nitafanya kila lililo ndani
ya uwezo wangu kukulinda na
kuhakikisha hakuna mtu yeyote atakaye hatarisha maisha
yako.Naomba unielewe"
"Huyu jamaa aliyekuja
kutuokoa ni mmoja wa wale jamaa
waliokuwa wananichoma na
umeme jana.Anataka kutupeleka
wapi?
" Winnie tutaongea vizuri
baadae.Jiandae
tuondoke"akasema Vicky na
Winnie akatoka kwa shingo
upande
"Yule mtu ni nani na
katumwa na nani?Yawezekana
tayari wamekwisha fahamu kama
nilishiriki katika kifo cha Pascal na
sasa wanaanza kunisaka.Hii si vita
ndogo”akawaza Vicky
"Namshukuru sana Steve kwa
kutokea kwa wakati na kutuokoa.Nilikuwa sina ujanja
tayari nilikuwa nimenaswa.Lakini
Steve alifahamuje kama niko
katika matatizo?akajiuliza
"Nisipoteze muda ngoja
niongozane na Steve na nitapata
ufafanuzi kutoka kwao kuhusu
tukio hili la leo.Kwa sasa nahitaji
sana kuwa karibu na akina Elvis
kwani peke yangu siwezi
kujilinda,tayari nimeanza
kuwindwa na si mimi peke yangu
bali na familia yangu hasa mdogo
wangu Winnie.Nani lakini
wananiwinda? akajiuliza na
kuendelea kupakia nguo na
baadhi ya vitu vichache katika
sanduku na alipokuwa tayari
akamfuata Winnie akamsaidia
kuchukua baadhi ya vitu vyake vichache wakaondoka na
kuwaacha nyumbani mlinzi
pamoja na mtumishi wa ndani
ambaye Vicky alimtaka aende
mapumzikoni kwa wiki mbili na
asimueleze mtu yeyote kile
kilichotokea pale nyumbani
Sent using
Jamii Forums mobile app