Jumakidogo
R I P
- Jul 16, 2009
- 1,851
- 420
Ni shabiki wa kusoma riwaya, lakini nimekuwa mvivu siku hizi baada ya uandishi wa riwaya kufifia tofauti na zama za kina Willy Gamba. Juzi nimepata bahati ya kusoma riwaya inayoitwa Joka kuu Kagera mpaka Maputo ambayo nimemkuta nacho kitabu hicho rafiki yangu mmoja akikifanyia tafsiri katika lugha ya kifaransa. Japo yaliyoandikwa humo ni hadithi inayodaiwa kuwa ya kubuni ambayo kwa hakika imeandikwa kwa umahiri mkubwa na mvuto katika kuisoma. Lakini yaliyoandikwa humo huenda yakawa yanapotosha ukweli kuhusu vita ya Kagera, ni vigumu kujua siri hiyo. Ama labda mwandishi ameleta mjadala kutokana na hadithi za mapokeo kutoka upande wa pili wa shilingi. Kama hayo ni kweli, basi kazi ilikuwepo...