SadariKisesa
New Member
- Feb 1, 2021
- 1
- 0
MAMA USINIFUNDISHE UCHAWI.
SEHEMU YA KWANZA
“Mkoani Morogoro, wilaya ya Mvomero, kata ya Kibaoni, na kijiji cha Maharaka. Anga yote ilikuwa imetanda kuashiria mvua saa yoyote inanyesha. Hali ya hewa si shwari baridi lilikuwa kali kupita maelezo. Ardhi baada ya muda ukali wa jua ulipoa ikaacha shamrashamra za wanakijiji zikilindima. Ndege nao walifurahia ujio wa mvua. Shorwe kwa makundi wakawa wanarukaruka na kukimbizana huku wakionyesha furaha kwaajili ya ujio wa mvua.
Yange yange hawakuachwa nyuma walikuwa kipaumbele kupendezesha anga kwa rangi zao nyeupe na kuruka kwa madaha, “Kwaa kwaaa kwaaaa.”
Alaah! Kunguru nae anafurahia ujio wa mvua kwa kurukaruka huku akitoa sauti angavu angani. Anga kikweli siku ya leo imependeza ama kweli Mungu hakukosea kuumba viumbe vyake. Ameumba na sasa wanamtumikia.
Yaani ni kazi kwelikweli, nakuambia ujio wa mvua ulileta hekaheka hadi kwa wanakijiji. Wanakijiji walitimua mbio na kurudi majumbani wakijua mvua itanyesha kumbe lahasha!!!. Lakini katika pilikapilika za wanakijiji kujihami na mvua, alionekana kijana wa kiume chini ya mwembe akiwa kajiinamia huku mkono wake wa kuume ukiwa umeshika tama. Kijana huyu hakuonyesha dalili ya kuhofia ujio wa mvua. Alijikatia tamaa kabisa na ndipo alipoamua kutulia chini ya mwembe.
Kichwa chake kilionekana kimejaa msongo mkubwa wa mawazo huku asijue kinachoendelea angani. Alikuja kushtuliwa na mama yake mara baada ya kuitwa kwa muda mrefu na mama yake kwa kutingishwa mabega.
“Naam!,” Kijana yule aliitika kwa mshangao na kukurupuka toka kwenye lindi la mawazo mara baada ya kusikia mama yake akimuita.
“Mbona unaonekana una mawazo sana... nini kinachokutatiza?,” Mama yule aliuliza huku akiangalia juu ya anga na kuhofia ujio wa mvua.
“Unajua fika mwanao ninavyoteseka kwa kulima, lakini hata mwaka mmoja sijafanikiwa kupata mafanikio,” Kijana yule alieleza mambo yanayomsumbua.
“Hayo mambo ndiyo yanakufanya ujikatie tamaa mapema?.”
“Sio mapema unavyodhani... `ebu wewe fikiria miaka mingapi imepita lakini mimi nipo vile vile.”
“Miaka mitano si mingi, nakusihi zidi kupambana tu ipo siku utafanikiwa.”
“Lini sasa?.. kama kupambana nimepambana sana hadi nimechoka.”
“Eeh... nyanyuka tukazungumzie nyumbani hapa tusije nyeshewa na mvua. Unaona hali ya hewa ilivyobadilika mvua itanyesha sasa hivi,” Mama yule alisema huku akimvuta mwanae mkono wa kuume upesi anyanyuke waondoke.
Kabla kuondoka wakaficha majembe kisha wakaongoza njia ya kuelekea nyumbani wakafika jioni. Kijana yule akaenda chumbani kwake akamwacha mama yake akiandaa chakula cha usiku jikoni.
**********
Kijana huyu alibahatika kuishi na mama pekee, sababu baba yake alifariki akiwa katika umri mdogo na katika mazingira ya kutatanisha. Hakubahatika kusoma alikuwa ni mtoto wa kulima na kufanya kazi za nyumbani.
Zao kubwa alilopendelea kulima hasahasa ni nyanya. Akalima Nyanya kwa uchungu huku akijipa matumaini ya kuwa ipo siku atafanikiwa. Kijana huyu na mama yake wakaishi katika nyumba ya urithi iliyoachwa na marehemu baba yake, ambaye alitambulika kwa majina ya Iddy Ramadhan Mbawala. Wakasongesha maisha katika nyumba iliyojengwa kwa matofali ya kuchoma. Njaa upande wao waliizoea huku kejeli za majirani zikishamiri juu yao kwa kuwatupia vijembe vya chinichini wakisema; “Wanajifanya maskini tajiri, wacha wafe na njaa.”
Lakini kijana huyu na mama yake wakaziba masikio hawakutaka kabisa kusikiliza maneno yanayosemwa na majirani. Kipindi cha mavuno kijiji cha Maharaka huwa kinakuwa na ahueni kwa wanakijiji kwa sababu ya mavuno kupatikana kwa wingi msimu huo.
Mama yake kijana huyu ambaye anayetambulika kwa majina ya Lola Binti Mngane, ambaye ni mama wa mtoto mmoja anayetambulika kwa majina ya Sharifu Bin Mbawala alizoea hali ya maisha. Kijana Sharifu alijikatia tamaa lakini msimu wa mavuno kwa upande wake anakuwa na furaha yote sababu msimu huo unakuwa ahueni.
Binti Mngane ameishi na mwanae muda mrefu bila kumwambia mwanae siri nzito aliyohifadhi ndani ya moyo wake, licha ya mwanae pia hakutaka mtu yeyote atambue hiyo siri atakaetambua hiyo siri kifo halali yake.
Usiku huo Binti Mngane baada ya kupumzika na kuondoa uchovu wa shambani akaivisha chakula cha usiku, hatimaye akamuita mwanae waje kula achana na kula tu bali kulikuwa na jambo muhimu analohitaji amwambie mwanae.
“Sharifuuu,” Binti Mngane akapaza sauti.
“Naam,” Sharifu aliitika kutoka kwenye chumba chake chenye mwanga hafifu wa Koroboi.
“Unafanya, nini?,” Binti Mngane aliuliza huku akitenga chakula ukumbini.
“Nakunja nguo, siunajua ndani humu kulivyo na Panya,” Sharifu alijibu huku akitokwa na jasho usoni na machozi yakimtoka machoni kutokana na moshi wa Koroboi.
“Achia...ugali tayari.”
“Sawa, nakuja anzaga kula.”
Sharifu kukunja nguo ikamchukua dakika akamaliza akatoka chumbani akasogea hadi kilipo chakula. Akashangaa kumkuta mama yake akimngoja wakati alimwambia aanze kula.
“Si nilikuambia uanze kula, mbona unanisubiri tena?,” Sharifu aliuliza huku akishangaa kumuona mama yake mikono jinsi ilivyokauka kutokana na kunawa muda mrefu.
“Mwanangu, sijazoea kula peke yangu,” Binti Mngane alijibu huku akiachilia tabasamu.
“Sawa... lakini mboga ya leo, sijapenda,” Sharifu alisema mara tu baada ya kuona na kuila mboga ile.
“Nitafanyaje?..muda ulikwenda nikaona mboga nyepesi ni hii.”
“Mboga nyepesi ni mrenda peke yake...kuna mchicha, matembele kwa nini hujapika hizo?.”
“Hizo zina utaratibu wake nazo kama vile kuchambua na kuosha lazima zingenichelewesha...tule, tena huu leo nimeupika vizuri,” Binti Mngane alijibu huku akionyesha tabasamu kufurahia mrenda aliokaangiza.
Sharifu hakupendezwa nao mrenda, akala kwa kujilazimisha kwa kuwa palikuwa hakuna mboga nyingine, hivyo hakuna budi kula. Akala kwaajili ya kutuliza njaa tu, walipomaliza kula akatoa vyombo na kuvipeleka mahali koridoni.
“Ukishaweka vyombo njoo, kuna mazungumzo kidogo” alisema Binti Mngane kwa kumhabarisha mwanae.
“Kiukweli, umetahabika sana” alizungumza Binti Mngane mara baada ya mwanae kurudi ukumbini mara baada ya kuweka vyombo.
“Sanaaa...mpaka sasa nishachoshwa na hayo matahabiko.”
“Kama ulishachoshwa mimi leo kuna kitu nahitaji nikuambie...upo tayari?.”
“Kitu gani hicho mama?.”
“Si unahitaji mafanikio, sasa presha yako ya nini?.”
“Lazima niwe na presha, kwa kuwa kitu chenyewe sikijui unachotaka kuniambia.”
“Ondoa shaka...nitakuambia.”
“Sawa nakusikiliza, niambie nipate kujua hicho kitu.”
“Lakini si unania kweli ya kufanikiwa?.”
“Ndiyo... nahitaji kufanikiwa leo hata kesho.”
“Kwasasa ushakua mkubwa na hali ya kijijini ushaiona...vijana wengi hapa kijijini wamepata mafanikio kwa haraka wewe hushangai hilo.”
“Naliona hilo na nashangaa...ila bado sijakuelewa unamaanisha nini?” aliuliza Sharifu ili apate kuelewa mama yake anataka kuzungumza nini.
“Ninachomaanisha, nitakuambia,” Binti Mngane alimeza mate kidogo kisha akauliza.
“Ila una moyo?.”
“Moyo ninao...niambie.”
“Kama una moyo vizuri, sasa nisikilize kwa makini.”
“Eeeeh!.”
“Vijana wenzako hapa kijijini, wanafanikiwa kwa kitu hiki kimoja tu ambacho ni...,” Binti Mngane kabla ya kuendelea kuongea akapaliwa akakohoa mfululizo hatimaye akaendelea kuongea.
“Ambacho ni uchawi, sasa wewe upo tayari kujiunga na uchawi?.”
Sharifu alichoambiwa na mama yake kilimshangaza sana, hakuamini akafikiri kuwa labda ni mzaha hivyo akabaki akicheka sana.
“Unacheka nini?,” Binti Mngane aliuliza huku akikunja ndita kwa hasira.
“Nimefurahi tu.”
“Kilichokufurahisha ni nini eti?.”
“Ujue sijakuelewa...hivi unatania au unaniambia kweli?.”
“Kuna muda wa matani na usio wa matani, haya ninayokuambia hapa ni kweli hakuna utani wowote.”
“Kabisa!?.”
“Eeenh!.”
“Ujue mama unanichanganya kiukweli.”
“Kivipi?.”
“Mimi na uchawi wapi na wapi?.”
“Kwa hiyo unataka kusema unataka kuendelea kuteseka...si ndiyo?.”
“Sihitaji.”
“Kumbe?.”
“Sio mzoefu pia naogopa mno kuwa mchawi, kwa sababu ni aibu kubwa katika jamii kujihusisha na masuala kama hayo.”
“Sijaona hapo kinachokuogopesha...unajitakia kuteseka kumbe mwenyewe.”
“Lakini mama mbona naona kama unaning'ang'aniza unaona huko kuzuri. MAMA USINIFUNDISHE UCHAWI......sitaki kabisa kama mafanikio yenyewe yanapatikana hivyo, bora nife nikiwa maskini tu.”
“Nani alikuambia huko ni kubaya?, kuwa mjinga...utabaki kuwasindikiza vijana wenzako hadi mwisho wa dunia,” Binti Mngane alisema kwa hasira huku akinyanyuka kwenye mkeka kama ugomvi na mashavu kutunisha kama Panya buku akaingia chumbani.
Sharifu naye akaingia chumbani kwake kwa kuona mama yake kaondoka kakasirika na kumwacha peke yake ukumbini. Alipofika kitandani usingizi haukuja kabisa alikuwa bado anafikiria maneno aliyoambiwa na mama yake.
Akawaza na kuwazua mara mbili mbili ndipo akagundua anayosema mama yake yana ukweli mtupu baada ya kukumbuka baadhi ya vijana wenzake waliofanikiwa pale kijijini. Sharifu kadri anavyozidi kukumbuka wivu unamshika anatamani leo kesho aweze kufanikiwa.
“Bora, nikubali tu,” Sharifu alijiwazia moyoni huku akipinduka pinduka kitandani kwa kukosa hata lepe la usingizi.
“Lakini hata nikikubali...uchawi huo nitaupata wapi?” alijiuliza Sharifu kwa kutokujua mama yake kama yupo kwenye chama cha uchawi.
“Lakini potelea pote............ Mama nahisi atakuwa anapajua. Ngoja nitamuuliza, ikiwezekana nijiunge.”
Unaambiwa hakuna mkate mgumu mbele ya chai na hakuna Bausa yeyote mbele ya usingizi. Sharifu usingizi ukamnyong'onyesha akawa mpole hatimaye akapitiwa na usingizi. Kesho yake akaamka mapema akatoka nje alipofika nje akakutana na mama yake ukumbini akamsalimu lakini cha ajabu mama yake hakujibu ile salamu.
“Ina maana mama, yaani kitu kidogo tu umeninunia hivyo?,” Sharifu akauliza.
“Umenishangaza sana yaani nafanya kwa faida yako, lakini wewe unaniona kama hayawani.... Sasa endelea kutahabika maana ndiyo hali uliyoichagua” aliongea Binti Mngane kwa sauti iliyojaa ukali.
ITAENDELEA...
Kitabu hiki kipo kwenye harakati ya kutoka ukikihitaji weka oda mapema. Ili kitakapotoka nikuhifadhie nakala yako au kitabu chako 🙏.