Riwaya ya kipelelezi: Maiti 15 tu nitafurahi tena

Riwaya ya kipelelezi: Maiti 15 tu nitafurahi tena

gilbert35

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2021
Posts
253
Reaction score
475
Riwaya: Maiti 15 tu Nitafurahi Tena
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
WhatsApp: +255765824715

Hii ni Sehemu ya 01
SURA YA KWANZA
Zimepita takribani dakika 15 tangu awasili ndani ya ofisi yake. Ofisi ndogo tu iliyoweza kuendana na cheo chake cha uinspekta wa jeshi la polisi. Ameketi juu ya kiti, mikono yake miwili imetamalaki juu ya meza ya mbao huku juu ya mikono kukiwa na faili kubwa lenye maandishi makubwa yanayosomeka "MAUAJI KISHUMUNDU". Naam, ni faili lililobeba maelezo kuhusiana na mauaji yanayoendelea katika kijiji cha Kishumundu kilichopo wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro. Ni siku ya kumi tangu akabidhiwe kesi hii lakini hakukuwa na hatua yoyote ile ambayo ameshaipiga ingeweza kumpa mwangaza.

"Inspekta, Inspekta Jasmine, unaitwa na mkuu ofisini kwake sasa hivi" Sauti ilimkurupua na kumuondolea utulivu aliokuwa nao. Jina lake ni Jasmine Wahab. Mwanamke shupavu mwenye cheo cha uinspekta wa polisi.
Akalifunga faili lile na kuliweka juu ya meza, akanyanyuka na kuelekea hadi ilipo ofisi ya mkuu wake wa kazi.
Alipofika Ofisini kwa mkuu wake wa kazi alikaribishwa kiti kwa ishara ya mkono. Ni ishara ya mkono ilitumika kumkaribisha kitini kwa sababu mkuu wake anaongea na simu kutoka kwa kamanda wa polisi wilaya ya Moshi.

"Inspekta Jasmin, leo ni siku ya kumi tangu ukabidhiwe kesi hii lakini hujapiga hatua yoyote ile. Inamaana muuaji anakuzidi akili? Maana tangu nikukabidhi hadi sasa wameshauwawa tena watu saba na kufanya idadi kamili kutimia kumi." Bwana Elius Benjamin alizungumza bila kuweka tuo. Alikuwa akimtazama Inspekta Jasmine usoni.

Inspekta Jasmine hakujua aseme nini kwa wakati huo, kichwa chake kilikuwa kikitafakari mambo mengi kwa wakati mmoja. Moyoni alishanyanyua mikono yake juu kuashiria kwamba alikosa namna. Angesema nini Jasmine mbele ya mkuu wake? Kwamba atafutwe mtu mwingine aifanye kazi hii? Alikuwa kimya akitafakari.

"Leo mchana atafika hapa mpelelezi kutoka idara ya usalama wa taifa, utakuwa naye na pia nahitaji umpatie ushirikiano wa kutosha. Mtakuwa mnaripoti kwa kamanda mkuu wa polisi wilaya kila hatua mtakayoipiga, Sawa?" Alisema Bw Elius

"Sawa Mkuu" Inspekta Jasmine akaitikia. Akasimama, akapiga saluti na kutoka nje ya ofisi ya mkuu wake wa kazi.

"Bora hata wamepanga kuniletea wa kusaidiana naye. Hata Adam aliwekewa msaidizi kule bustanini bwana." Inspekta Jasmine alijiambia huku akitabasamu. Tumbo lake likamshtua kidogo, akaelekea mgahawa uliopo jirani na kituo cha polisi kwa ajili ya kupata kifungua kinywa.

"Kama kawaida yangu. Supu ya kushiba na chapati nne. Pilipili na limao usisahau" Inspekta Jasmine alisema baada ya kuingia ndani ya mgahawa ule. Ilikuwa yapata saa nne asubuhi.

Jua lilizidi kuzidisha kero na manung'uniko kwa wakazi wa Kishumundu. Lilikuwa likiwaka litakavyo. Lakini kuhusu joto wala halikuwa kali kivile, kwa sababu mlima Kilimanjaro haukuwa mbali sana na kijiji hiki. Baridi linalocheuliwa na mlima nalo si haba. Ni mchana wa saa saba sasa katika kituo cha polisi cha Kishumundu. Gari aina ya Haier Hybrid nyeusi inafunga breki zake mbele ya jengo la kituo cha polisi. Anateremka kijana aliyevalia suti nyeusi akiwa na briefcase nyeusi. Haraka anapokelewa na kupelekwa hadi ilipo ofisi ya mkuu wa kituo.

Jina lake ni Gilbert Mwaitika, mpelelezi na askari kijana aliyedaiwa kutokea usalama wa taifa kuja kusaidiana na Inspekta Jasmine. Anafanikiwa kuonana na mkuu wa kituo cha polisi Kishumundu, wanateta pamoja kwa dakika sita kabla ya mkuu kuagiza kuitwa kwa Inspekta Jasmine.

Inspekta Jasmine haraka anatii wito na baada ya muda mchache watu watatu wanaizunguka meza na kuteta pamoja. Gilbert Mwaitika, Inspekta Jasmine pamoja na mkuu wa kituo, bw Elius Benjamin wanajadiliana pamoja kwa dakika takribani kumi na tano kisha Mkuu anawaruhusu kuondoka tayari kwa kuanza uchunguzi wao.

Ilikuwa ni saa kumi na nusu jioni Gilbert Mwaitika akiwa pamoja na Inspekta Jasmine ndani ya Tulizo Restaurant wakipata chakula.

"Lile faili la mauaji haya si lipo kwako?" Akauliza Gilbert Mwaitika wakati wanakula.

"Yeah, lipo ofisini kwangu." Akajibu Inspekta Jasmine.

"Utanipatia hilo pamoja na magazeti yote ambayo yamehawi kuandika habari kuhusiana na mauaji haya. Halafu kesho asubuhi tutapata pa kuanzia" Gilbert Mwaitika akasema huku akijipangusa mikono yake kwa tishu. Akagida juisi yake kisha akaegemea kiti chake kutazama juu akionesha kumsubiri Inspekta Jasmine amalize kula waondoke.

Baadae wakaagana. Ni baada ya Inspekta Jasmine kumkabidhi Gilbert Mwaitika vitu vyote alivyohitaji. Gilbert Mwaitika alikuwa amepewa nyumba nzuri ya kuishi iliyopo jirani kabisa na kituo. Inspekta Jasmine yeye alikuwa akiishi nyumbani kwake, umbali wa kilomita moja na nusu kutoka kituo cha polisi.

Gilbert Mwaitika alifungua mlango baada ya kufika, akaweka briefcase lake mezani, akaelekea moja kwa moja hadi chumbani na kuvua nguo zake, akachukua taulo kubwa kutoka kwenye sanduku la nguo. Akaelekea bafuni kuoga. Baada ya dakika kadhaa akatoka bafuni na taulo lake, akaelekea hadi sebuleni na kukamata briefcase lake, akalifungua na kutoa faili pamoja na magazeti aliyopatiwa na Inspekta Jasmine. Yalikuwa ni magazeti tisa. Akayapangilia magazeti yale kuanzia la awali kuchapishwa hadi la mwisho. La awali kabisa lilionekana kuchapishwa tarehe 12 Januari. Huku gazeti la mwisho kuchapwa likionesha tarehe ya kuchapwa ni 27 Januari.

Alianza kufungua kurasa iliyoandikwa habari kwa kina kuhusiana na mauaji yale katika gazeti la tarehe 12 Januari. Baada ya kusoma habari ile akagundua waliuwawa watu wawili usiku wa tarehe 11 Januari, yaani mtu na mkewe ndio waliouwawa majira ya saa mbili usiku wakiwa wanatoka baa kuelekea nyumbani kwao. Akachukua kitabu chake cha kutunzia kumbukumbu kilichokuwa ndani ya briefcase na kuandika maelezo mafupi, akaweka kando gazeti lile na kukamata gazeti linalofuata. Gazeti hili lilichapwa tarehe 14 Januari.

Liliripoti mauaji ya mzee mmoja mwanaume mwenye umri wa miaka 79 mchana wa tarehe kumi na tatu nyumbani kwake. Lakini pia aligundua wale watu wawili waliouwawa awali pamoja na mzee huyo wameuwawa kwa kupigwa mshale wenye sumu. Yaani ilionekana muuaji alikuwa akiua kwa mtindo wa kizamani, na kwa staili moja tu ya kutumia mshale. Na kweli hata alipolipitia gazeti la tatu hadi la tisa yote yalionesha waliouwawa wote walipigwa kwa mshale shingoni ama kifuani, na mshale huo ulikuwa na sumu kali iliyoweza kuushambulia mfumo wa damu kwa haraka sana.

"Waliouwawa ni wanaume sita na wanawake wanne. Kati ya wanaume sita, mzee ni mmoja tu, huku wanawake wanne pia mzee ni mmoja tu. Kumi waliouwawa ni wanne tu wenye undugu wa damu. Kwanini Muuaji anatumia mshale wenye sumu wakati kuna silaha nyingi tu kwa sasa katika ulimwengu huu wa kitekinolojia? Lazima kuwe na sababu. Katika ulimwengu wa kipelelezi kila kitu lazima kiwe na sababu." Gilbert Mwaitika alikuwa akiwaza huku akichora na kuandikaandika kwenye kile kitabu chake kidogo. Akalikamata na faili alilopewa pia. Hili hakulisoma kwa kina kama alivyofanya kwenye yale magazeti. Alilipitia tu juujuu na kisha kulifunga.

" Muuaji ni mwanamke bila shaka. Ni lazima awe mwanamke" Gilbert Mwaitika akawaza huku akitabasamu.
Akaandika pia kwenye kitabu chake kisha akakusanya kila kitu na kuhifandhi ndani ya briefcase. Akatazama saa ya ukutani na kugundua ilishatimu saa nne usiku. Akapeleka briefcase lile chumbani na kulihifadhi chini ya uvungu wa kitanda. Akakamata simu yake na kufungua uwanda wa ujumbe mfupi.

'Kesho saa mbili asubuhi tukutane palepale mgahawani. Nina jambo' alichakata ujumbe mfupi na kuutuma kwa Inspekta Jasmine. Akazima taa ya chumbani na kisha kupanda kitandani, akavuta shuka tayari kwa kuusaka usingizi. Lakini kabla ya kujifunika vizuri simu yake ikawaka mwangaza kwenye kioo na kisha mlio mfupi ukafuatia.

'Sawa, usiku mzuri kwako' aliona ujumbe mfupi uliotoka kwa Inspekta Jasmine. Akatabasamu na kisha kuiweka simu pembeni. Akalala.

Sauti ya jogoo ilisikika kwa mbali, baadaye kukafwatiwa na sauti za ndege wa angani. Ni siku nyingine kwa Gilbert na wanakishumundu. Gilbert Mwaitika aliyafumbua macho yake taratibu na kisha kujinyoosha akiwa bado amelala. Sauti ya chaga ikasikika ikionekana kukereka kutokana na kitendo cha Gilbert kujinyoosha angali amelala bado. Bila shaka kitanda hiki kilionekana kuwa chakavu ama hakijakazwa nati zake vizuri.

Gilbert Mwaitika hakujali sana, aliamka na kuvalia traksuti nyeusi ya mazoezi na kuelekea nje. Ilikuwa ni desturi yake kila asubuhi kuamka na kupiga mazoezi ya kukimbia ili kuimarisha viungo vya mwili. Alikimbia hadi katika shule ya msingi Kishumundu, akauzunguka uwanja wa shule ile mara mbili na kisha kuanza safari ya kurejea katika ile nyumba aliyolala usiku. Akiwa njiani akakumbuka kwenye magazeti aliyoyapitia jana usiku, gazeti la saba liliripoti mauaji ya mwalimu wa shule ya msingi Kishumundu palepale shuleni. Ilikuwa ni asubuhi wanafunzi na walimu walipoenda shuleni na kumkuta mwalimu huyo amefariki akiwa nje ya mlango wa bafu kwani ilionesha mwalimu huyo alikuwa akielekea bafuni majira ya usiku kwani alikuwa ikiishi shuleni pale.

Gilbert Mwaitika alikuwa akikumbuka wakati anarejea katika nyumba aliyopewa. Alifika na kuingia bafuni kujiandaa tayari kwa kuingia kibaruani. Ndani ya muda mfupi alikuwa tayari ndani ya suti safi ya kijivu, akajihakikisha yupo vyema, akakamata briefcase lake na kuelekea hadi Tulizo restaurant alipopanga kukutana na Inspekta Jasmine saa mbili asubuhi.

Saa mbili ikawakuta pamoja wakipata supu safi ya Ng'ombe ndani ya Tulizo restaurant. Wakipata supu Gilbert akaanzisha mazungumzo.

"Inspekta Jasmine" Gilbert Mwaitika aliita

"Abee" Inspekta Jasmine aliitikia kwa adabu

"Muuaji wa watu wote kumi waliouwawa ni mwanamke bila shaka" Gilbert Mwaitika akasema na kisha kupangusa mafuta kwenye lipsi ya mdomo kwa kutumia tishu iliyokuwa pembeni ya sahani aliyowekewa bakuli la supu.

"Mmmh! Inawezekanaje? Umejuaje Gilbert?" Inspekta Jasmine akaachia mguno na kuachia maswali mawili mfululizo. Alishangaa kivipi muuaji akawa mwanamke.

"Ni hivi, Muuaji anaonekana kutumia mshale wakati wa shambulio. Na sote tunajua sio mara zote mshale unaweza kuondoa uhai wa mtu, ni mara chache haswa unapopiga sehemu ambazo ni dhaifu kama kifuani, kooni au mara chache tumboni. Sasa muuaji anatumia mshale ambao tayari ameupakaa sumu ili iwe rahisi kwa mlengwaji kufa haraka, ikimaanisha kwamba mtu huyu anaonekana ni dhaifu kimwili na ni mwoga pia ndiyo maana anaona atumie mshale wenye sumu kwani bila kuuwekea sumu hawezi kumfwata mpinzani wake na kummalizia kama hatofanikiwa kumuua kwa mshale huo."

"Bado sijakupata vizuri. Kwahiyo muuaji ametumia njia hii kwa sababu anaonekana ni dhaifu? Sasa kwanini awe mwanamke wakati hata mwanaume ambaye ni kilema anaweza kuwa dhaifu?" Inspekta Jasmine akauliza tena

RIWAYA HII INAUZWA KWA TSHS 2,000/= TU YA KITANZANIA.
KAMA UTAIHITAJI HADI MWISHO FANYA MALIPO KWENDA M PESA NAMBA 0765824715 AU HALOPESA NAMBA 0621249611 KISHA NJOO WHATSAPP AU INBOX HAPAHAPA FB UWEZE KUIPATA.
PIA UNAWEZA KUWASILIANA NASI KWA NJIA YA EMAIL mushigilbert28@gmail.com

Ahsanteni..

FB_IMG_1697127513680.jpg
 
MAITI 15 TU NITAFURAHI TENA

Inspekta Jasmine anamsaka Muuaji anayezidi kuteketeza roho za wanakijiji wa Kishumundu. Cha kushangaza ni kwamba Bi Sandra kabla ya kupoteza maisha alidai kwamba Jasmine amerudi, na bila shaka ndiye anayewamaliza.
Kama haitoshi mpelelezi Gilbert Mwaitika anajikuta yupo hospitali kisa kuwekewa sumu katika juisi ya embe aliyopatiwa na Inspekta Jasmine. Hapo sasa ndio nazidi kuchoka nikijiuliza inamaana ni Inspekta Jasmine ndiye muuaji au kuna Jasmine mwingine? Na kama kuna mwingine kwanini Inspekta Jasmine alipoiokota simu ya marehemu Bi Sandra alivunga kimya bila kumshirikisha Gilbert?

Riwaya ya Kipelelezi iitwayo MAITI 15 TU NITAFURAHI TENA inapatikana whatsapp kwa bei ya Tshs 2000 tu. Njoo whatsapp kwa namba 0621249611 uweze kujipatia yote
 
MAITI 15 TU NITAFURAHI TENA

Inspekta Jasmine anamsaka Muuaji anayezidi kuteketeza roho za wanakijiji wa Kishumundu. Cha kushangaza ni kwamba Bi Sandra kabla ya kupoteza maisha alidai kwamba Jasmine amerudi, na bila shaka ndiye anayewamaliza.
Kama haitoshi mpelelezi Gilbert Mwaitika anajikuta yupo hospitali kisa kuwekewa sumu katika juisi ya embe aliyopatiwa na Inspekta Jasmine. Hapo sasa ndio nazidi kuchoka nikijiuliza inamaana ni Inspekta Jasmine ndiye muuaji au kuna Jasmine mwingine? Na kama kuna mwingine kwanini Inspekta Jasmine alipoiokota simu ya marehemu Bi Sandra alivunga kimya bila kumshirikisha Gilbert?

Riwaya ya Kipelelezi iitwayo MAITI 15 TU NITAFURAHI TENA inapatikana whatsapp kwa bei ya Tshs 2000 tu. Njoo whatsapp kwa namba 0621249611 uweze kujipatia yote
Hongera mkuu mzigo uko poa
 
Hawa watu wanaondika baadhi ya riwaya ni watu waovyo sana
 
Huyu hua hamalizi simulizi ni muongo muongo na mpuuzi pia mhuni msijihangaishe
 
Riwaya: Maiti 15 tu Nitafurahi Tena
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
WhatsApp: +255765824715

Hii ni Sehemu ya 02
"Bado sijakupata vizuri. Kwahiyo muuaji ametumia njia hii kwa sababu anaonekana ni dhaifu? Sasa kwanini awe mwanamke wakati hata mwanaume ambaye ni kilema anaweza kuwa dhaifu?" Inspekta Jasmine akauliza tena

"Mwanaume hata kama ni kilema ni lazima apambane kwa namna yoyote kufanikisha lengo lake. Na pia mwanaume huyo hangetumia silaha kama hii. Huyu ni mwanamke ambaye amejawa na woga anafanya mauaji kwa kutumia mshale wenye sumu kwani anaamini akishamdungua mpinzani wake shughuli imeisha. Anahitaji kumaliza shughuli mapema kwani hana nguvu za kupambana. Labda tuseme anaweza akawa ni mwanaume wa makamo pia. Lakini asilimia 90 ni mwanamke ambaye ni mkazi wa hapahapa Kishumundu" Gilbert Mwaitika akaeleza.
Wakati huo walikuwa wameshamaliza kunywa supu na ilikuwa yapata saa tatu kasoro asubuhi.

"Hapo nimekuelewa. Kwahiyo sasa tunafanyaje?"

"Cha kufanya ni kupita kila familia iliyokumbwa na msiba tufanye mahojiano nayo. Naamini kwa kutumia njia hii tutafika tunapopahitaji kufika."
Gilbert Mwaitika akasema

"Lakini nilishafanya nao mahojiano na hakukuwa hata na jipya lolote lile, na ripoti nzima niliiandika kwenye faili lile nililokupatia jana jioni" Akasema Inspekta Jasmine.

"Nahitaji kufanya nao tena mahojiano Inspekta Jasmine. Turudue tu naamini wao ni njia ya kumpata muuaji" akasema Gilbert Mwaitika.
Basi mahojiano baina ya familia za wafiwa na wapelelezi hawa wawili yakafanyika, na ndani ya siku mbili walishazifikia familia saba ambazo ziliwapoteza watu tisa.
Ilikuwa ni jumamosi, saa nne asubuhi Gilbert Mwaitika na Inspekta Jasmine walikuwa katika familia moja wakizungumza nayo. Kwa mujibu wa data zao ilikuwa ni familia ya nane kuihoji. Na aliyeuwawa katika familia hii alikuwa ni mtu wa kumi.
Gilbert Mwaitika alikuwa akijaribu kumtia moyo mama wa makamo ambaye alikuwa akitokwa na machozi huku akiteta kwa uchungu. Mama huyu alimpoteza mumewe baada ya kuuwawa kwa mshale majira ya asubuhi akitoka haja kubwa. Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa mama huyo ni kwamba mumewe aliamka asubuhi na kumwacha pekee kitandani akiaga anaelekea chooni. Mama huyo alieleza baada ya dakika chache alisikia kelele za kuomba msaada kutoka kwa mumewe, ndipo alipomkuta akiwa chini huku mshale ukionekana kuzama katika kifua chake.

"Acha tu kijana wangu usinikumbushe zaidi, Mume wangu alikuwa ni mtu mzuri tu, hakuwa na ugomvi na yeyote. Mume wangu alikuwa ni msaada wangu wa pekee hapa duniani lakini sina yeyote wa kuniangalia, sina watoto, sina ndugu wa kunitazama" Mama huyu alizidi kulalama kwa uchungu.
Alionyesha wazi kwamba kifo cha mumewe kilimnyong'onyesha kwa kiasi kikubwa na kukata matumaini ya kuishi.

"Pole sana Mama yangu, nipo hapa kwa ajili ya kumsaka huyu muuaji na ninakuahidi nitamkamata na kumkabidhisha katika vyombo vya sheria." Gilbert Mwaitika alimpa matumaini mama yule aliyeonesha kukata tamaa ya maisha.
Baadaye kidogo walimuaga mama huyo huku Inspekta Jasmine akimwachia noti mbili za shilingi Elfu kumi ya Tanzania. Wawili hao walishika njia hadi ilipo nyumba ya Balozi wa mtaa. Walipanga kwenda kuzungumza na balozi mawili matatu kwani katika upelelezi wao waligundua kati ya watu kumi waliouwawa, watu saba wanatokea katika mtaa ambao balozi Ruwenzori anakaa huku watatu wakikaa mtaa unaofuata. Mitaa hii yote inaunda kijiji cha Kishumundu.
Inspekta Jasmine akiwa na Gilbert Mwaitika ambaye ni mpelelezi kutoka idara ya usalama wa taifa walikuwa wakiikaribia nyumba ya balozi Ruwenzori. Kwa mbali walisikia sauti ya kelele ya kuomba msaada. Sauti hii ilikuwa ikitoka kwa binti wa Balozi Ruwenzori aitwaye Clara.

"Msaadaa jamani msaidieni baba yanguu.... Uwiiiii msaadaa!" Zilikuwa ni kelele kutoka kwa Clara, binti yake balozi Ruwenzori.
Inspekta Jasmine pamoja na Gilbert wakaanza kuongeza kasi na kujikuta wakikimbia kuelekea ilipo nyumba ya Balozi. Sio wao tu, hata majirani pia walikuwa wakielekea huko wakikimbia.

"Ameshakufa, inaonekana sumu inayotumiwa na muuaji ni kali sana aisee. Yaani dakika haijaisha mtu ameshakufa wakati mshale hata haujazama ndani! Kweli hii ni ajabu" Baba mmoja alionekana akiongea.
Pembeni alikuwa amelala binti yake Balozi baada ya kupoteza fahamu kwa kile alichokisikia. Mwili wa Balozi ulikuwa chini ukionekana kuvimba kutokana na sumu.

"Tumechelewa kidogo sana, tungekutana na muuaji. Ametutangulia kidogo sana" Inspekta Jasmine alimwambia Gilbert baada ya kufika pale.

"Wenda muuaji anatufwatilia pia, anajua hatua tunazozipiga. Yaani kutoka kwa yule mama na kuja huku tayari tumetanguliwa. Ni nani alijua kama tunakuja huku zaidi ya mimi na wewe?" Gilbert alimgeukia Inspekta Jasmine, wakabaki wanatazamana.

"Hakuna tuliyemuambia. Inamaana muuaji yupo katika akili yetu? Alijua tutakuja hapa?" Inspekta Jasmine akahoji.
Walijitambulisha kwa watu waliokuwa pale, haraka wakapiga simu kituoni kuita gari ili kuichukua maiti ya Balozi Ruwenzori kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya kuukabidhi mwili ule kwa taratibu za mazishi.

"Mke wake yuko wapi? Labda anajua kitu." Gilbert Mwaitika akasema kwa sauti kubwa

"Leo jumamosi mkewe huwa anaenda sokoni kununua mahindi." Mama mmoja akasema

"unamaanisha huwa anaenda kila jumamosi sio? Ni kwanini mahindi kila jumamosi? Anafanyia shughuli gani hayo mahindi ya kila jumamosi?" aliuliza Gilbert wakati anamtazama mama huyo.

"Hiki kijiji ni maarufu kwa zile pombe za kienyeji zinazotengenezwa kwa mahindi. Yeye ni mmoja wa watu wanaofanya biashara ya pombe hiyo." Inspekta Jasmine akamnong'oneza Gilbert sikioni.

"Twende huko sokoni sasa hivi. Bila shaka sio mbali sana na hapa, kama mkewe hajui kitu basi labda yeye anafuata ama ni mmoja ya watu wanaopaswa kuuwawa." Gilbert akamwambia Inspekta Jasmine kwa sauti ndogo. Wakawahi huko.
Ilikuwa ni barabara ya vumbi ikiwapeleka lilipo soko la Kishumundu. Ni umbali wa kilometa moja tu kutoka sokoni hadi nyumbani kwa balozi Ruwenzori ambaye tayari ni marehemu.
----------------
Bibi Sandra ambaye ni mke wa balozi Ruwenzori alikuwa akiusukuma mkokoteni wake taratibu. Ndani ya mkokoteni huo kulikuwa na mahindi pamoja na baadhi ya mahitaji ya nyumbani. Simu yake ilianza kupiga kelele kuashiria kuna mtu anapiga. Akausogeza mkokoteni wake hadi pembeni ya barabara ili aweze kuipokea simu ile. Naam, akaitoa katika kipochi alichokuwa amekivaa shingoni kama kidani.
'Mama Atukuzwe'! Kwenye simu ilisomeka hivyo. Akapokea na kuweka sikioni.

"Haloo mama Atu!" Bi Sandra aliongea.

"Naam Bi Sandra, bado upo sokoni?" Sauti ya mama Atukuzwe ilisikika simuni.

"Hapana, ndio nipo njiani. Vipi upo baa au? Nasikia kelele za sauti nyingi kweli. Au umeenda kule k..!" Bi Sandra hakuweza kuendelea kuzungumza.
Mshale mwembamba ulitua katika tumbo lake, na mbele yake alimwona mtu aliyeushika upinde wa mshale huku akimtazama kwa macho makali. Mtu yule alianza kurudi kinyumenyume na kutoweka ndani ya shamba lililopo jirani na barabara.

'Mh.. m.m.h, amerudi Jasmine. Jas..s.m.i.n.e!'.
Bi Sandra alitamka kwa shida, taratibu akaelekea chini na kuanguka kama mzoga uliotupwa chini.

"Bi Sandra.. Bi Sandra kuna nini? Haloo!" Sauti ya mama Atu ilisikika simuni.
Wakati huohuo Inspekta Jasmine pamoja na Gilbert Mwaitika walikuwa wakisogea karibu na pale alipo Bi Sandra.

"Inspekta Jasmine kile nini pale?" Gilbert aliuliza.

"Kama mtu kalala pale, halafu mbona kama ule ni mkokoteni wa Bi Sandra?" Inspekta Jasmine alisema huku akiongeza mwendo. Mapigo yake ya moyo yalianza kudunda kwa kasi kuashiria kulikuwa na hatari. Gilbert naye hivyohivyo, mikono yao ikaelekea viunoni mwao ikijitahidi kupapasa kitu, na kitu hicho kilikuwepo.

Nini kitaendelea? Kwanini Bi Sandra kabla ya kupoteza maisha alilitaja jina la Jasmine? Amerudi kufanyaje? Ungana nami hadi mwisho ili mimi Gilbert nikusimulie kisa hiki kizuri cha kipelelezi. Uzuri ni kwamna kila lililojificha litajulikana hapahapa. [emoji3060]
Ni rasmi sasa simulizi hii haitapostiwa tena hapa, badala yake kama utaihitaji unaweza kulipia Tshs 2000 tu kwenda Halopesa namba 0621249611 au Mpesa namba 0765824715 kisha njoo whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie yote.
Ahsanteni [emoji3062][emoji120]
 
Riwaya: Maiti 15 tu Nitafurahi Tena
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
WhatsApp: +255765824715

Hii ni Sehemu ya 03

Wakati huohuo Inspekta Jasmine pamoja na Gilbert Mwaitika walikuwa wakisogea karibu na pale alipo Bi Sandra.

"Inspekta Jasmine kile nini pale?" Gilbert aliuliza.

"Kama mtu kalala pale, halafu mbona kama ule ni mkokoteni wa Bi Sandra?" Inspekta Jasmine alisema huku akiongeza mwendo. Mapigo yake ya moyo yalianza kudunda kwa kasi kuashiria kulikuwa na hatari. Gilbert naye hivyohivyo, mikono yao ikaelekea viunoni mwao ikijitahidi kupapasa kitu, na kitu hicho kilikuwepo.
Walichomoa bastola zao kutoka viunoni mwao, zikakokiwa tayari kwa kukabiliana na adha yoyote itakayojitokeza mbele yao.
Walifika pale na kukuta mwili wa bi Sandra umeanza kuvimba kutokana na sumu ya mshale ule. Kwa mara nyingine tena walipishana na muuaji ambaye bado hafahamiki ni nani na kwanini anaua.
Inspekta Jasmine aliiona simu ya mkononi pembeni kidogo ya mwili wa bi Sandra. Akaiokota, lakini Gilbert Mwaitika hakuiona.
Siku ilikuwa ikiisha taratibu kwa magharibi ya jua kuzama. Gilbert Mwaitika na Inspekta Jasmine hawakuwa wamepata chochote kile. Mwili wa balozo Ruwenzori pamoja na wa Bi Sandra haukuwa na chochote chenye kuwapa faida katika uchunguzi wao. Mwili ukakabidhiwa kwa ndugu ili taratibu nyingine ziendelee. Vichwa vya hawa wapelelezi wawili vikabaki vikiuma.
'Muuaji ni nani? Kwa nini anaua?'
Yakawa ni maswali tu yasiyokuwa na majibu.

************

Ibada ya misa jumapili ndiyo ilikuwa imefikia ukingoni huku Waumini wakionekana kuanza kutawanyika ndani ya kanisa katoliki Kishumundu. Gilbert Mwaitika anaonekana ndani ya gari yake akiwa pamoja na Inspekta Jasmine. Walikuwa ni miongoni mwa waumini walioshiriki katika ibada ile. Wakaiondoa gari yao na kuelekea Tulizo Restaurant. Hupendelea Tulizo Restaurant kwa sababu ya utulivu wa pale na isitoshe ni karibu na kituo cha polisi. Kama kawaida wakapata kifungua kinywa baada ya kufika pale, wakiwa bado na mavazi yao waliyotoka nayo kanisani.

"Unayakumbuka maswali yetu mawili ambayo yanatuumiza vichwa vyetu?" Gilbert akavunja ukimya

"Naam" Inspekta Jasmine akasema huku akifungua juisi ya embe kutoka kwenye kopo kubwa. Akaimimina katika glasi moja na kumkabidhi Gilbert Mwaitika. Gilbert akaipokea na kuimiminia kinywani bila kupumzika mithili ya mtu aliyekuwa na kiu sana.

"Sasa yatupasa kukomaa na swali namba mbili kwanza. Tukishajua kwanini anaua basi ni rahisi kujua muuaji ni nani." Gilbert akaeleza.

"Tuanzie wapi?" Akauliza Inspekta Jasmine huku akifuta lipsi zake kwa kutumia tishu.
Alikuwa akifuta mafuta yaliyobakia katika lipsi zake kutokana na kunywa supu. Yeye hakunywa juisi ile, madai yake ni kwamba angekesha maliwatoni kwa siku nzima kama angesubutu kuchanganya supu na juisi ya embe kwa wakati mmoja.

"Kila kitu kinachotokea na kutendeka kina sababu. Muuaji anaua kwa sababu, wanaouwawa wanauwawa kwa sababu. Ni lazima tujue kwanini wanauwawa ndipo iwe rahisi kumjua aliye nyuma ya haya. Wameshafika watu kumi na mbili waliouwawa. Wanne kati yao wana undugu wa damu, wengine saba, watano kati yao ni majirani huku wawili wakiwa ni balozi wa mtaa na mkewe waliouwawa jana. Bila shaka muuaji anajaribu kulipa kisasi kwa watu fulani waliowahi kumtendea ubaya. Twende kwenye familia za hao ndugu wanne waliouwawa kwa mara nyingine, kuna kitu nimekihisi. Wakanyanyuka na kumwita mhudumu aweze kuchukua malipo ya supu na juisi.
Lakini katika kunyanyuka kukazuka kizaazaa. Gilbert Mwaitika alianguka chini ghafla na kupoteza fahamu.

Ilikuwa ni Saa kumi na moja jioni. Gilbert Mwaitika alirejewa na fahamu akiwa juu ya kitanda cha wagonjwa ndani ya hospitali kubwa ya Kibosho Mission. Aliyashangaa mazingira ya pale kwani hakutarajia kuwa pale.
Katika kuangaza akafanikiwa kumwona nesi aliyevalia gauni jeupe akipita. Akajaribu kumpungia mkono lakini hata mkono wake haukuwa na nguvu kama ilivyo kawaida.

"Nini kimenisibu?" alijiuliza bila kupata jibu.

"Ooh! Umeamka? Pole sana. Unahitaji muda zaidi wa kupumzika ili mwili wako uweze kurejea katika hali yake ya awali uliyoizoea." Nesi yule akasema mara baada ya kufungua mlango wa kioo na kuingia ndani ya chumba alicholazwa Gilbert.

"Kwani kimenipata nini?" Gilbert Mwaitika akamuuliza nesi. Nesi huyu alikuwa amesimama pembeni ya kitanda chake.

"Ulikunywa juisi iliyokuwa imechanganywa na sumu. Kama usingewahishwa hospitalini basi ungepoteza maisha kwani sumu hiyo ilikuwa ni kali sana." Nesi huyu akamwacha Gilbert kinywa wazi.

"Eti sumu. Kivipi?"
Halmashauri ya kichwa cha Gilbert ikaanza kuushughulisha ubongo. Analolisema nesi linamwacha kinywa wazi
Akajaribu kuvuta kumbukumbu ya mara ya mwisho ni nini kilitokea kabla ya kuwa hapa. Naam, akakumbuka mara ya mwisho alikuwa na Inspekta Jasmine Wahab ndani ya tulizo Restaurant wakipata supu baada ya kutoka kanisani. Akakumbuka pia Inspekta Jasmine alimmiminia juisi ya embe katika glasi na kumpatia. Akaipokea na kuimiminia kinywani.
Baada ya hapo je? Hakumbuki tena kilichoendelea.

"Inspekta Jasmine. Umefanya nini?" alikuwa akiwaza. Lipsi za mdomo wake zilikuwa zikichezacheza kuashiria ni hasira zilifika kunako.

Akamgeukia Nesi huku akijitahidi kuinuka angalau akae na sio kulala. Alishindwa, bado hakuwa na nguvu za kutosha. Nesi akamsaidia kumwinua aweze kuketi kama anavyotaka.

"Unaweza kuniambia ni nani aliyenileta hapa?" akamuuliza Nesi.
Kabla Nesi hajasema lolote mara mlango ukafunguliwa, anayeingia ni daktari akiongozana na mkuu wa kituo cha polisi Kishumundu Bw. Elius Benjamin akiwa na sare yake ya kazi.
Gilbert anafanyiwa baadhi ya vipimo tena na daktari yule huku akimtaka afungue kinywa chake ammulike kunako mdomoni, anahamia machoni kuyamulika, anapima mapigo yake ya moyo kisha anamgeukia bwana Elius.

"Angalau kwa sasa sio mbaya, japo anahitaji bado muda zaidi wa kupumzika." Dokta anasisitiza

"Siwezi kuendelea kulala hapa angali bado kazi yangu iliyonileta huku haijakamilika." Gilbert naye anavunja ukimya. Anachomoa dripu ya maji na kujitahidi kunyanyuka.
Maskini, anahisi kizunguzungu lakini kabla hajaanguka anashikiliwa vyema na kuketishwa juu ya kitanda.

"Sumu bado haijaisha mwilini kijana, kuwa na subira utapoteza maisha" Dokta anamsisitiza Gilbert Mwaitika.

"Ni kweli Gilbert, kwa sasa pumzika hadi hali yako itengamae. Nimeagiza vijana wangu kumtafuta Inspekta Jasmine maana tangu saa nne ulipodondoka pale mgahawani alitoweka na simu yake haipo hewani kabisa." Bwana Elius anasema kwa mara ya kwanza tangu afike pale.

"Unaamini kama yeye ndiye anayehusika na hili?" Gilbert Mwaitika anamkazia macho bwana Elius.

"Kwa asilimia chache. Kuna kitu nyuma ya pazia, Jasmine hawezi kufanya hivi. Na kama kafanya basi kuna sababu kubwa. Ni yeye pekee anayeweza kutufafanulia zaidi kuhusiana na hili lililotokea." Bwana Elius akatetea.
Haikuwa rahisi kwake kuamini kama ni kweli Inspekta Jasmine kahusika na tukio la kumwekea sumu mpelelezi kutoka idara ya usalama wa taifa aliyekuja kijijini kwao kutokana na mauaji yanayoendelea. Alikuwa anamwamini sana Inspekta Jasmine.
Gilbert Mwaitika alikuwa akiwaza mambo mengi kichwani mwake. Kwanza ni nani muuaji, japokuwa alikuwa na uhakika kwamba muuaji ni wa kike. Pili ni nani yupo nyuma ya swala la yeye kutaka kuuwawa kwa kuwekewa sumu kwenye juis ambayo Inspekta Jasmine alimpatia.

"Hii siwezi kuinywa sasa hivi eti. Nitakesha maliwatoni kwa siku nzima kama nitsthubutu kuchanganya supu na juisi ya embe kwa wakati mmoja."
Maneno haya yakapita katika ufahamu wake Gilbert. Maneno haya yalisemwa na Inspekta Jasmine wakati yeye anauliza kulikoni anywe juisi ya embe peke yake.

"Inspekta Jasmine" Alitamka kwa sauti kubwa huku akiachia pumzi ndefu itoke nje.

"Kwani ilikuwaje Gilbert?" Bwana Elius Benjamin aliuliza. Ndipo Gilbert Mwaitika akamwelezea kuanzia walipotoka kanisani hadi kufikia Kicheko Restaurant.
Wote walishangaa. Hawakutegemea kama Inspekta Jasmine angefanya vile.

"Kama si yeye ni kwanini akimbie na azime simu?" Bwana Elius akauliza huku akijaribu kurudia kupiga namba ya Inspekta Jasmine.

"Hilo swali hata mimi najiuliza nakosa jibu" Gilbert Mwaitika akasema.

Vipi na wewe unajiuliza kama wao? Hebu vaa sura ya kipelelezi leo, unahisi muuaji ni Nani? Usikose mwendelezo wa riwaya hii, uzuri ni kwamba kila lililojificha majibu yatapatikana ndani ya riwaya yetu nzuri[emoji3526]
Cha kufanya ni wewe kulipia Tshs 2000 tu kwenda Halopesa namba 0621249611 au Mpesa namba 0765824715 kisha njoo whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie.
Ni lazima maiti 15 zitimie [emoji1787][emoji1787]
Storika na Gilbert
 
Riwaya: Maiti 15 tu Nitafurahi Tena
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
WhatsApp: +255765824715

Hii ni Sehemu ya 04

"Kwani ilikuwaje Gilbert?" Bwana Elius Benjamin aliuliza. Ndipo Gilbert Mwaitika akamwelezea kuanzia walipotoka kanisani hadi kufikia Kicheko Restaurant.
Wote walishangaa. Hawakutegemea kama Inspekta Jasmine angefanya vile.

"Kama si yeye ni kwanini akimbie na azime simu?" Bwana Elius akauliza huku akijaribu kurudia kupiga namba ya Inspekta Jasmine.

"Hilo swali hata mimi najiuliza nakosa jibu" Gilbert Mwaitika akasema.
Gilbert ilimbidi akubaliane na alichosema daktari. Aliendelea kupumzika juu ya kitanda huku dripu yenye maji ikiendelea kumminia maji katika mshipa wa mkono wa kushoto. Mkuu wa kituo cha polisi Kishumundu naye akaaga kuondoka huku akiahidi kumjuza Gilbert kila kitakachoendelea huko uraiani.
Lilishapita lisaa limoja na nusu baada ya Gilbert Mwaitika kuachwa peke yake katika chumba kile cha dharura ndani ya hospitali ya Kibosho Mission. Maisha ya kukaa na kulala juu ya kitanda yalishamchosha kwa kiasi kikubwa, alikuwa akijigeuza upande wa kushoto, wa kulia, mara asimame au akae. Yaani kwa ufupi alikuwa akitamani kutoka nje lakini hali yake ya kiafya haikuweza kumruhusu. Alijisachi mfukoni labda kulikuwa na simu yake, hakuiona. Lakini alisikia mlio wa simu ikilalamika upungufu wa chaji ndani ya droo katika meza iliyo karibu na kitanda alichokalia.

"Bila shaka ni simu yangu waliniwekea kwenye droo" Alijisemea Gilbert.
Akaisogelea droo na kuifungua. Ilikuwa ni simu yake kweli, japokuwa ingezima wakati wowote ule kama angeitumia. Angalau sasa aliweza hata kusimama bila kuhisi kizunguzungu, lakini mtihani ilikuwa ni kuunyanyua mguu na kuusogeza mbele. Kutembea kwake ilikuwa ni vigumu.
Akaichukua simu yake na kupiga namba ya Inspekta Jasmine bila kujali kama simu itazima kwa chaji. Naam, sauti nyororo ya mwanamke ikasikika ikimjuza juu ya kutokupatikana kwa nambari anayoipigia. Hakusita kurudia kupiga kwa mara nyingine, ndipo simu yake ikazima kabla hata mwanamke anayezungumza simuni hajamaliza kutoa taarifa juu ya kutokupatikana kwa namba ya Inspekta Jasmine.

Baadae kidogo aliingia nesi yule aliyemjia mara ya kwanza. Nesi huyo alikuja na chupa yenye mtori.

"Nimeagizwa nikuletee chakula, ngoja nikuwekee kabisa kwenye bakuli uweze kuria taratibu. Ni mtori wa utumbo wa Ng'ombe." Nesi akasema huku uso wake ukitandaza tabasamu linaloweza kumpa matumaini tosha mgonjwa yeyote ambaye angemtazama.

"Eti wakati naletwa hapa ulikuwa karibu?" Gilbert akamuuliza nesi huyo

"Mimi ni moja kati ya watu waliokupokea uliposhushwa tu garini. Tulikuja na kitanda cha magurudumu kukuchukua." akaeleza Nesi

"Ni nani na nani waliongozana nami hadi hapa?" akauliza tena Gilbert Mwaitika

"Alikuwemo dada mmoja aliyevalia gauni la rangi ya zambarau, pamoja na askari wawili waliovalia sare za kazi." Nesi alieleza. Mwanadada aliyetajwa alikuwa ni Inspekta Jasmine kwani Gilbert Mwaitika alikumbuka vyema muda huo wakipata kifungua kinywa, Inspekta Jasmine alivaa hivyohivyo kama anavyoelezwa na nesi.

"Huyo dada alikaa hapa kwa muda gani?" Gilbert akauliza tena.

"Hakuchukua muda, baada ya wewe kubainika ulitumia kinywaji chenye sumu alitoweka. Baadae akaja bwana Elius Benjamin akajaribu kumpigia lakini hakuweza kumpata hadi sasa."
Nesi aliendelea kufunguka huku akipooza mtori kwa kijiko. Akampatia Gilbert mtori ule, Gilbert akaupokea na kuanza kuunywa taratibu huku akitafakari.

"Naomba uniwekee chaji simu yangu, imezima kabisa" Gilbert akasema. Nesi yule akaichukua na kuondoka nayo.
*******

SURA YA PILI
Baada ya kuhakikisha Gilbert Mwaitika amepatiwa huduma katika hospitali aliyompeleka, Inspekta Jasmine alirejea katika kituo cha polisi Kishumundu na kutoa taarifa ya kupoteza fahamu kwa Gilbert Mwaitika. Hata hivyo hakuweka wazi kilichompata Gilbert Mwaitika zaidi ya kueleza tu hospitali aliyompeleka.
Baada ya kutoka nje ya kituo cha polisi aliitoa simu yake na kuizima, akaichomoa laini yake na kuitenganisha na simu, akachukua pikipiki na kumtaka dereva ampeleke nyumbani kwake. Inspekta Jasmine baada tu ya kufika nyumbani kwake aligonga kengele getini na baada ya sekunde kadhaa alifunguliwa na msichana wa kazi za ndani anayeishi naye.

"Yeyote atakayefika hapa kuniulizia mwambie sijafika nyumbani tangu asubuhi nilipoenda kanisani." Akatoa maelekezo kwa binti wa kazi.

"Sawa Dada." Binti akaitikia kwa heshima na kufunga mlango mdogo wa geti. Inspekta Jasmine alishazipiga hatua nne kuliacha geti, lakini akasimama na kumgeukia binti wa kazi tena.

"Kumbuka nimesema yeyote atakayefika kuniulizia. Sijasema isipokuwa fulani. Natumaimi umenielewa" Inspekta Jasmine akakazia tena. Awamu hii hakungoja kupewa jibu, aliondoka kuelekea ndani, na huko akapitiliza moja kwa moja hadi chumbani kwake.
Akiwa chumbani kwake alichukua karatasi na kalamu, akaanza kuandika ujumbe kwa takribani dakika zipatazo ishirini kisha akaikunja, akafungua droo ndogo iliyopo katika kabati la nguo na kutoa laini ya simu. Laini hiyo ni laini yake ya siri ambayo wengi wamjuao hawaifahamu. Wengi wao wamezoea kuwasiliana naye kupitia laini ile aliyoitoa kwenye simu yake. Akafanya kuiweka kwenye simu laini hii ya siri na kuitia katika droo ile laini nyingine. Akafunga mlango wa chumba chake, akamwita msichana wa kazi na kumpatia karatasi ile aliyoikunja baada ya kuandika ujumbe mrefu.

"Tazama simuni picha ya mtu huyu, akifika hapa nyumbani mpatie hii karatasi. Ninasafiri kidogo ndani ya siku mbili nitakuwa nimerejea. Kwaheri" Inspekta Jasmine akaaga na kutokomea.
Unamkumbuka mama Atukuzwe? Mwanamke aliyekuwa anazungumza na Bi Sandra ambaye sasa ni marehemu? Naam, Inspekta Jasmine aliichukua namba ya mama Atukuzwe kutoka kwenye simu ya Bi Sandra kwani kupitia simu ya marehemu Bi Sandra, Inspekta Jasmine aliweza kugundua kuwa yeye ndiye mtu wa mwisho kuwasiliana nae tena muda ambao mauaji yanatendeka. Alipiga namba ile kwa kutumia laini yake ya siri. Simu iliita na baada ya sekunde chache tu ikapokelewa.

"Hellow mama Atukuzwe, habari ya mchana?" Inspekta Jasmine alisabahi punde tu baada ya simu kupokelewa upande wa pili.

"Haloo, habari ya mchana ni njema, nazungumza na nani?" Sauti ya mama Atu ikasikika simuni.

"Naam Mama Atu, ninahitaji tuzungumze faragha tukiwa wawili rafiki yangu. Mimi ni Inspekta Jasmine, kama utakumbuka ni jana tu tumetoka hapo kwa marehemu Balozi Ruwenzori nikiwa na mwenzangu." Inspekta Jasmine akasema

"Ohoo, nimekupata mpendwa. Nipo nyumbani sasa hivi, waweza kuja hapa? Ni nyumba ya tatu baada ya kwa balozi. Imeezekwa kwa bati la rangi nyekundu." Mama Atu akaeleza

"Sawa Mama Atu, nakuja sasa hivi. Upo na nani?" Akauliza Inspekta.

"Ni mimi peke yangu mpendwa. Baba Atu yupo safarini, Atu na mdogo wake wapo kwenye michezo" Alisema mama Atukuzwe. Na Inspekta Jasmine ndivyo alivyokuwa akitamani, Mama Atu awe peke yake.

Ilikuwa ni saa Tisa alasiri mchana. Inspekta Jasmine alikuwa akiingia nyumbani kwa Mama Atukuzwe akiwa ni mwingi wa wasiwasi. Hakutaka kuonekana kwa watu kama yupo eneo lile. Alipiga hodi na baada ya sekunde kadhaa alipokelewa na mwenyeji wake.

"Karibu sana mpendwa. Ingia ndani tafadhali." akakaribishwa.
Inspekta Jasmine kabla hajaupokea ukaribisho huu aliyatazama mazingira ya nyumba kwa nje. Yalimpa tumaini la kutokuonekana kwa wapita njia kwani nyumba ilizungushiwa uzio wa majani ya mgomba na miti mirefu ya alizeti.

"Usijali mama Atu, nitapendelea zaidi nje kuliko ndani. Tukae tu hapa." akasema Inspekta Jasmine huku akitangulia kukaa kwenye kiti kirefu cha mbao.

"Basi ngoja nikuletee hata chochote kitu kabla ya kuanza kuzungumza mpendwa." Mama Atu akadokeza huku akizipiga hatua kuelekea ndani.

"Mama Atu tafadhali, muda ni mchache sana njoo tuzungumze." Inspekta akatia ukali kidogo.

"Hata maji mpendwa?" Mama Atu akageuka na kuuliza. Lakini jicho alilotazamwa na Inspekta Jasmine likamfanya arejee na kukaa. Amani iliyokuwa imemtawala ikapungua kiasi, woga ukaanza kumnyemelea taratibu kwa ajili ya kuchukua umiliki.

Nini kitaendelea?[emoji849] Muuaji ni nani? Kwanini anaua? Usikose sehemu ijayo hapahapa[emoji3062]..

Una haraka ya kusoma riwaya yote leo? Fanya malipo ya Tshs 1500 tu kama ofa utumiwe riwaya yote whatsapp, lipia kwenda M pesa namba 0765824715 au AirtelMoney namba 0784973700 kisha njoo whatsapp kwa namba 0621249611 au 0765824715 nikutumie. Wengine tusubiri hadi kesho[emoji3059]
 
Riwaya: Maiti 15 tu Nitafurahi Tena
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
WhatsApp: +255765824715

Hii ni Sehemu ya 05

"Hata maji mpendwa?" Mama Atu akageuka na kuuliza. Lakini jicho alilotazamwa na Inspekta Jasmine likamfanya arejee na kukaa. Amani iliyokuwa imemtawala ikapungua kiasi, woga ukaanza kumnyemelea taratibu kwa ajili ya kuchukua umiliki.

"Mama Atukuzwe" Inspekta Jasmine akaita baada ya kuhakikisha mwenyeji wake ameketi tayari.

"Naam mpendwa, nipo hapa kukusikiliza."

"Nadhani wanijua, naitwa Inspekta Jasmine. Ni Inspekta wa jeshi la polisi la Tanzania. Nipo hapa kwa mwendelezo wa upelelezi kuhusiana na mauaji yanayoendelea hapa kijijini kwenu Kishumundu. Nahitaji tu ushirikiano wako kwa kile nitakachokijadili nawe ama kukiuliza."
Kusikia vile, kijasho chembamba kikamtoka Mama Atu katika miimo ya macho kuelekea hadi katika pua. Aliikumbuka sauti ya mwisho ya marehemu mke wa balozi Ruwenzori ambaye naye pia ni marehemu.

"Jumamosi ya tarehe 2 mwenzi huu wa tisa, nikimaanisha siku mbili zilizopita nilifika mimi na mpelelezi mwenzangu nyumbani kwa Marehemu balozi Ruwenzori kwa ajili ya kuja kumuuliza baadhi ya maswali, lakini tulikutana na tukio tofauti na matarajio yetu, nadhani unafahamu kilichotokea na ulikuwa ni miongoni mwa waliofika ama waliokuwepo pale." Inspekta Jasmine alianzisha mjadala uliomleta pale.

"Ndiyo, nilikuwa miongoni mwao" Akasema mama Atu.

"Lakini tulitoka pale na kumfuata sokoni mkewe ambaye pia naye tayari ni marehemu. Na lengo la kumfwata huko ni baada ya kuhisi kuna hatari ya yeye kuuwawa ama anafahamu kitu juu ya mauaji haya yanayoendelea. Kwa bahati mbaya tulichelewa kwani tulikuta naye ameshauwawa kwa namna ileile muuaji anayoitumia katika kutekeleza mauaji." Akaweka tuo, akaingiza mkono wake katika mfuko wa suruali ya kitambaa aliyovalia.
Akaitoa simu ndogo aina ya nokia tochi.

"Hii ni simu ambayo tuliikuta pembezoni kidogo ya mwili wake. Na simu hii kwa mujibu wa simu yenyewe inaonekana ilikuwa ni yake. Baada ya uchunguzi wa awali niligundua wewe ndiye uliyekuwa unazungumza naye kabla ya umauti kumkuta kwani ulimpigia simu. Si kweli?" Inspekta Jasmine akamtazama mama Atu

"Ni kweli Dada yangu, nilimpigia kutaka kumuuliza yuko wapi kwa muda ule na yupo katika mazingira gani baada ya mumewe kupoteza maisha." Mama Atu akajitetea.

"Wakati tunatoka pale kwao kuelekea sokoni ni nani aliyetuambia kwamba mke wa Balozi Ruwenzori yupo sokoni?" Inspekta Jasmine akauliza.

"Ni mimi nilisema Afande" akajibu mama Atu

"Sasa utampigiaje simu wakati tulikuwa tunamwendea? Vipi kama nikisema wewe ndiye uliyesababisha kifo chake ama ulikuwa na nia ya kumwambia mumewe kafariki? Ulikuwa na lengo gani kumpigia maana pale tulifika saa tano na dakika thelathini na saba, kwenye simu inaonyesha ulimpigia dakika ya thelathini na nne na hamkumaliza hata dakika mbili kuzungumza."

"Hapana Afande, sikuwa na lengo baya mimi, naapa kwa Mungu mimi sihusiki na chochote kile. Nilimpigia tu kujua kama anafahamu kinachoendelea na sikuwa na lengo la kumfahamisha kinachoendelea nyumbani kwake." Aliendelea kujitetea mama Atu.
Inspekta Jasmine alikuwa akifahamu fika kwamba Mama Atu hajahusika kwa lolote, ila aliamini kuna kitu labda mama Atu anakifahamu na anaweza kudokezewa akapata mwangaza fulani.

"Kwahiyo mama Atu unataka kusema hujahusika na chochote juu ya mke wa balozi Ruwenzori? Mama Atu kumbuka una familia. Mwanao Atu bado anahitaji malezi kutoka kwako. Si vizuri akakosa malezi yako kusa tu wewe upo gerezani eti." Inspekta Jasmine akasema kwa sauti iliyojaa wingi wa huruma
Subira yavuta heri, Wahenga walinena. Na sasa ukafika wakati wa heri kwa Inspekta Jasmine baada ya kusubiri kutoka kwa mama Atu.

"Afande" Akaita Mama Atu.

"Nakusikiliza Mama Atu" Inspekta Jasmine akasema

"Jana wakati mmetuacha pale na kuwahi sokoni, nilijisogeza pembeni kidogo na kuitafuta namba ya Bi Sandra na kuipiga. Baada ya sekunde chache ilipokelewa. Wakati tunazungumza nilisikia akilalama kwa uchungu mkubwa kama vile kuna kitu kimemkaba koo kuzuia sauti isitoke" Mama Atu akaeleza huku akitetemeka kwa hofu.

"Halafu ikawaje?"

"Kuna maneno aliyatamka kisha nikasikia kishindo halafu kukawa kimya."

"Unaweza kuniambia ni maneno gani aliyatamka?"

"ndiyo Afande. Alilalama hivi....., 'Mh.. m.m.h, amerudi Jasmine. Jas..s.m.i.n.e!'. Baada ya hapo kukafwatiwa na kishindo, nadhani ni yeye alianguka labda, nikabaki nikiita haloo bi Sandra bila matumaini, mwishowe nikakata simu."
Alieleza mama Atu.

"ni watu wangapi umeshawaeleza kuhusiana na tukio hili?" Aliuliza Inspekta Jasmine

"Ni wewe tu Afande"

"Iwe kweli. Usimweleze yeyote yule tena, utaingia matatizoni. Labda mimi nitakapokutaka ueleze tena mbele yangu ama nikiwa na mtu mwingine. Nakuahidi hakuna kibaya kitakachokukumba."
Inspekta wa jeshi la polisi akamaliza na kunyanyuka aweze kuondoka. Alitazama upande ilipo nyumba ya marehemu balozi Ruwenzori. Ilikuwa ni umbali wa kama mita themanini na tano kutoka pale.

"Taarifa imeshatoka balozi Ruwenzori anazikwa siku gani na mkewe?" Inspekta Jasmine akauliza.

"Maziko ni siku ya Jumatano afande. Watazikwa pamoja palepale nyumbani kwao" Mama Atu akajibu

"Mungu awapatie pumziko jema, wana watoto wakubwa?

"Kati ya watano, ni mmoja tu ndiye mdogo. Yule binti aliyekuwa akilia jana pembeni ya mwili wa baba yake kabla ya kupoteza fahamu."

"Poleni sana wafiwa wote. Nitahudhuria msibani. Lakini pia nitakutafuta kama nitakuwa na lingine la kusema nawe. Kwaheri na uwe na jioni njema mama Atu." Inspekta Jasmine akaaga na kuondoka. Alimwacha mama Atu akiwa kama alivyomkuta. Cha zaidi sana ni kwamba alimpunguza kilo chache kutokana na hofu iliyokuwa imemvaa.
Hata hivyo Inspekta Jasmine hakurudi nyumbani kwake tena. Alielekea kijiji cha tatu kutoka kijiji cha Kishumundu kulala huko.
ITAENDELEA

Unataka kuimaliza riwaya hii leo? Lipia Tshs 1000 tu, m pesa namba 0765824715 au AirtelMoney namba 0784973700 kisha njoo whatsapp kwa namba 0621249611 au 0765824715 nikutumie.
Ijue nguvu ya buku leo na ujionee maajabu yake katika riwaya hii ya aina yake yenye visa vya kinyama na Upelelezi uliotukuka.
@OfficiallySimuliziZaGilbert
[emoji2398]2024
 
Back
Top Bottom