Riwaya za Eric Shigongo

Niliacha kusoma hadithi za shigongo baada ya kuona anatumia tone moja ya hadithi kama tamthilia za kifilipino unaanza kupredict mwisho ukiwa unasoma hadithi mwanzo
Namkubali husein tuwa yupo poa anatunga kila aina ya hadithi anapoamua anaweza
 
Sijaona hata mmoja aliyetoa ushahidi wa wizi wa shigongo katika hadithi zake,kama kweli ameiba leteni ushahidi wa huko alikoiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
shigongo anachukua mambo ya kwenye muvi na kutingia hadithi Nina uhakika
 
Guys...mimi nimefanya kazi na Shigongo kwa miaka minne. Ukisikia kuna watu magenius wa kuandika yule jamaa ni shida sana. Akitaka kuanza hadithi...anachukua kalamu na karatasi na kuanza kuandika...anaiandika kwa vipande kisa anaiandika yote.

Kwa miaka yote hiyo...nimeshuhudia akiandika hadithi zaidi ya nane, tena alipokuwa akianza ananiita na kunofundisha jinsi ya kuipangilia na kutengeneza matukio.

Kama ni shahidi...mm nitakuwa namba moja kusema shigongo haibi sehemu...yeye si muangaliaji muvi...yupo bize...atapata muda upi wa kuangalia muvi za kifilipino?

Yeye ni msomaji wa vitabu vya ujasiriamali...sijawahi kumuona akiwa na kitabu cha hadithi...kwenye kikabati kwake ofisini ni vitabu vya ujasiriamali tu...na nilipomuuliza why hana kitabu cha hadithi...alisema muda mchache sana...hawezi kusoma simulizi.

Kwa miaka yangu minne nilimfuatilia sana...sijaona sehemu ameiba...au kama mna ushahidi muweke manake alishawahi kusema mwene ushahidi atapewa milioni moja ila hadi leo hakuna liyeibuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
afadhali uwaambie maana watu wakiamua kumuandama doooooh....... na mwenye ushahidi akachukue 1mill
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…