Kwanza ngoja nikupe darsa dogo ili siku nyingine uwe makini kidogo unapoongolea usiyo na yakini nayo, kisha nikuwachie "homework" ukaifanye.
Siyo "New Jersey" ulipo take kupaongelea, ni Jersey, Channel Islands. New Jersey ni USA na hakuna asondae pesa huko.
Wanaosonda pesa Jersey hususan pale St. Helier, ni wale wasiofahamu maana ya neno "biashara". Kwa Rostam, unaongea kichwa kingine kabisa. Hajaanza leo kuyaona ma red carpet. Umemsahau "The King Maker"?
Naomba tafuta mtu anaeitwa Yusuf Fahd (Esop Pahad) katika serikali ya Afrika Kusini kuanzia wakati wa Ian Smith, Mandela mpaka leo hii. Ukipata kumuelewa mtafute Openheimer aliyekuwa mshauri wa kibiashara wa Mandela mwanzo mwanzo tu wa utawala wake. Ukiwaelewa hao watu wawili, kumbuka; Rostam Mbunge ambae hajawahi kushindwa uchaguzi, Rostam Mweka Hazina Mkuu wa CCM.
Pia ni mfanya biashara pekee Tanzania hii anaeweza kumtumia Waziri Mkuu ampelekee ujumbe wa mchango wake klabu ya Yanga kwa kumpatia simu tu. Mwengine utaanzia wapi?
Nnakuhakikishia, "The King Maker" pia ni mfanya biashara pekee ambae ana uwezo wa "kuombwa" (appointment) na wale watoao maagizo.
Hao niliokutajia ni partners wa Rostam kwa namna moja au nyengine katika biashara zao Afrika Kusini na hapa Tanzania labda au hata ndani ya Mwadui Diamond Mine.
Unganisha dots kama ni mtu wa kuchimbua utapata picha ya Rostam ni nani.