Roast-Arm azizi kupenya

Mandesy

Senior Member
Joined
Mar 22, 2018
Posts
115
Reaction score
125
Baada ya kupata upenyo wa kuingia Red Carpet, sasa ndugu yetu Rost-Arm ameanza sarakasi mpya. Juzi juzi kazindua kampuni ya taifa Gas, ambayo kimsingi iko Seychelles. Sasa anataka kuiuza kampuni hiyo kwa kampuni ya kutoka Mauritius. Huyu bwana hataki kabisa kampuni zake zikawa za ndani na hii ina maana kwamba akizinguliwa tu, basi anasepa maana fedha zote zitakuwa zikienda New Jersey…

Tutaona mengi
 
Sasa afanye nini? Wafanyabiashara wengi wanafanya risk analysis na kufanya maamuzi. Sasa kwa awamu hii kila siku kuna mtu anakurupuka na kutoa maamuzi na faini, imejaa visasi na chuki,
Kwa nini mfanyabiasha a-risk mtaji wake? Ndio maana wanahamisha nje kwenye capital security ambao wanaweza pata returns (faida).
 
Na yale mapipa makubwa ya kuhifadhia gas yapo ngambp ya nchi, kuuza share or company is a normal /
 

Kwanza ngoja nikupe darsa dogo ili siku nyingine uwe makini kidogo unapoongolea usiyo na yakini nayo, kisha nikuwachie "homework" ukaifanye.

Siyo "New Jersey" ulipo take kupaongelea, ni Jersey, Channel Islands. New Jersey ni USA na hakuna asondae pesa huko.

Wanaosonda pesa Jersey hususan pale St. Helier, ni wale wasiofahamu maana ya neno "biashara". Kwa Rostam, unaongea kichwa kingine kabisa. Hajaanza leo kuyaona ma red carpet. Umemsahau "The King Maker"?

Naomba tafuta mtu anaeitwa Yusuf Fahd (Esop Pahad) katika serikali ya Afrika Kusini kuanzia wakati wa Ian Smith, Mandela mpaka leo hii. Ukipata kumuelewa mtafute Openheimer aliyekuwa mshauri wa kibiashara wa Mandela mwanzo mwanzo tu wa utawala wake. Ukiwaelewa hao watu wawili, kumbuka; Rostam Mbunge ambae hajawahi kushindwa uchaguzi, Rostam Mweka Hazina Mkuu wa CCM.

Pia ni mfanya biashara pekee Tanzania hii anaeweza kumtumia Waziri Mkuu ampelekee ujumbe wa mchango wake klabu ya Yanga kwa kumpigia simu tu. Mwengine utaanzia wapi?

Nnakuhakikishia, "The King Maker" pia ni mfanya biashara pekee ambae ana uwezo wa "kuombwa" (appointment) na wale watoao maagizo.

Hao niliokutajia ni partners wa Rostam kwa namna moja au nyengine katika biashara zao Afrika Kusini na hapa Tanzania labda au hata ndani ya Mwadui Diamond Mine.

Unganisha dots kama ni mtu wa kuchimbua utapata picha ya Rostam ni nani.
 
Kula tano bibie! CCM NI ILEILE! Hata ukija na mbwembe zako utatulia tu ...Kuna makundi ya watu wachahche sana wanaiongoza Dunia ,ila wanaoitawala ndio hubwata!
 
Kula tano bibie! CCM NI ILEILE! Hata ukija na mbwembe zako utatulia tu ...Kuna makundi ya watu wachahche sana wanaiongoza Dunia ,ila wanaoitawala ndio hubwata!
Hilo nalo neno.

Nahisi kama ni wachache sana watakielewa ulichoandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…