Robert Kiyosaki wa Rich Dad, Poor Dad ni tapeli?

Robert Kiyosaki wa Rich Dad, Poor Dad ni tapeli?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Nimeangalia video moja Youtube inamuelezea kamajamaa ni magumashi sana. Sehemu kubwa ya pesa anazopata ni kupitia semina anazotoa akichaji dola 12K hadi 45K, na si kupitia biashara ya Real Estate kama anavyodai. Pia japo anasifika kwa kuandika kitabu hicho lakini hasa aliyefanya kazi ni muandishi mwenza, Sharon Lechter ambaye ni mhasibu kitaaluma. Walikuja kutengana na huyu mama kibiashara baada ya kuona utapeli wa Kiyosaki unataka kuvuka mpaka.

Pia wanadai mauzo ya kitabu hicho yalipaa zaidi baada ya jamaa kufanya kolabo na kampuni ya Amway Corp ambayo inakashfa ya kuendesha pyramid scheme. Inadaiwa watu walikuwa wakienda kwenye semina za Amway walikuwa wanaambiwa kwanza wanapaswa kununua kitabu Rich Dad, Poor Dad.

Zaidi ni kuwa mzee wake anayemwita Poor Dad hakuwa poor, hata alimpa mtaji wa dola laki moja ili aanzishe biashara.
Sikiliza mwenyewe.


View: https://youtu.be/D2fHbbOmu_o?si=UyxZUaUAPUsiITAs
 
Kivyovyote vile jamaa ni tajiri. Awe ameshirikiana au kutoshirikiana na watu wengine huyo Kiyosaki ni tajiri. Kitabu chake kipo karibu dunia nzima... nakala zaidi ya 32m zimeuzwa. Hata kama kwenye kila nakala anapata Tsh 1000/= bado ni noti ndefu. Mimi nampongeza.
 
Soma 4 quadrants kama ni tapeli basi ni Pro Max huyu mwamba anajua kazi yake wivu tu unawasumbua
 
Akili ya kupata pesa ni akili nzuri sana kivyovyote, hata kwa ujanja mzuri ki smart fulani.

Bila kuua na kuumiza wengine kimwili.
Exactly, as long as hajaua wala kulazimisha mtu kwenda kwenye hizo semina na kununua hivyo vitabu basi hana baya.😅

Nakumbuka miaka fulani kwenye ukuaji, kama hujasoma vitabu vya jamaa basi you don't fit into the circle among colleagues.😂
 
Kiyosaki amewahi firisika baada ya kuandika vitabu vyake na kuuza nakala nyingi. Uwezo wake kusimamia biashara ni mdogo sana hivyo kubaki kwenye kula hela za semina sio ajabu.
 
Utapeli upo wapi hapo hicho kitabu kimetengeneza matajiri wengi sana
Kudanganya watu katajirika kupitia real estate kumbe katajirika kwa kufundisha watu kuhusu utajiri. Kushirikiana na kampuni ya upatu.

Kupotosha watu wachukue mikopo ya hadi dola 35,000(karibu milioni 100Tsh) ili walipie kozi zake za utajiri.
 
Kiyosaki amewahi firisika baada ya kuandika vitabu vyake na kuuza nakala nyingi. Uwezo wake kusimamia biashara ni mdogo sana hivyo kubaki kwenye kula hela za semina sio ajabu.
Na ili auze semina anapotosha watu kwa kujidai Guru wa biashara. Hana tofauti na Kiboko ya Wachawi🤣
 
Na ili auze semina anapotosha watu kwa kujidai Guru wa biashara. Hana tofauti na Kiboko ya Wachawi🤣
Vitu anavyotaja kwenye vitabu vyake havitekelezeki ndio maana yeye mwenyewe alitumia mbinu hizohizo na akafirisika akawa na madeni mengi huku akiwa na assets chache.

Hiyo real estate nayo ilimpa hasara. Ana makampuni yaliyofungwa kwa kufirisika ila kuna biashara nyingine anazodaiwa anazo ambazo hazijulikani. Kwahiyo anatumia mwanya wa biashara zisizojulikana ambazo zipo au hazipo ili kupata hela ya kuuza elimu ya fedha.
 
Back
Top Bottom