Robert Lewandowski au Luis Suarez; nani no.9 bora duniani?

Ngoja nijaribu kuwatofautisha kwa kadri nijuavyo.
Luis Suarez ni mpiganaji uwanjani, anapigana kadri anavyoweza ili apate goli uwanjani, ni mroho wa magoli uwanjani.
-Jamaa hawezi kutumia miguu yote miwili sawasawa.
-Sio mzuri kwa mipira ya juu.
-Hana uwezo wa kukokota ama kuwachambua mabeki.
-Sio mtu ws kukaa na mpira muda mwingi mguuni hata zile radha za kiburudani ndani ya soka huwa hana kiviile kama Aguero ama Lewandowsk.



Lewandoski sio mpiganaji kama Suarez ila yeye uwanjani anacheza kama hataki kucheza vileeeee!!!!
-Mpira ukija kwa mguu wowote ule kama yupo sehemu nzuri hesabu goli.
-Mpira uje chini au Juu anaweza kuuweka wavuni, tofauti na Suarez
-Anaweza kukokota na kupiga chenga japo sio sana.
-Jamaa ana skills za kuweka mpira mguuni kwa muda mrefu.
-Lewandowski Magoli yake ni ya kiufundi zaidi, jamaa ana skillz kubwa za kufunga.


Yote ya Yote hawa wote hawamfikii bwana mkubwa Kun Aguero. Hatari sana huyu Jamaa!!!
 

suarez anakokota watu pia,
 
kwa mtazamo wangu Suarez ni mchezaji machachari but robert ni mchezaji hatarii
 
Kwa mtazamo wangu Suarez anaweza kung'anta meno vizuri zaidi ya Lewandowski
 
Luis Suarez Anaweza kwenye National Team na Hata Ligi Zote alizocheza kafanya Bie
 
mkuu alleyn upo vizuri, kun aguero ni habari nyingine jamaa ana balaa.
 

Lol, Luis Suarez hajui kudribble na kuchambua Mabeki..?

Au ulikuwa unamaanisha Jeffren Suarez????
 
1.AGUERO. 2.suarez. 3.lewandosky. 4.zlatan.
 
Ningeambiwa nichague kati ya Suarezz na Lewandowski ningemchagua Suarez.

Nimeiona kazi yake akianzia Liverpool.

Anajua kutafuta mpira na anaisaidia timu inapobanwa zaidi.
 
Najua kuna namba tisa bora duniani wengi tu kwa sasa kama kina Vardy, Ibrahimovic, Benzema na wengine. Lakini kati ya hawa wawili nani zaidi....?

na vardy nae striker bado sna !!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…