Robertinho: Yanga itatisha sana msimu ujao Kwa kumsajili Chama

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
YANGA ITATISHA SANA MSIMU UJAO KAMA ITAMSAJILI CHAMA - ROBERTINHO

Kocha wa zamani wa Simba, Robero Oliveira 'Robertinho' licha ya kushituka kusikia uwezekano wa Chama kwenda Yanga amesema endapo hilo litatimia linaweza kuleta shida kubwa kwa timu pinzani kwani kikosi Cha Mabingwa hao kitaongeza ugumu katika safu yao ya ushambuliaji.

"Muda unavyosogea Chama anazidi kwenda mwisho lakini haina maana kuwa hataweza kuisaidia Yanga. Tatizo ninaloliona hapa ni kwamba mchezaji bora anakwenda kuungana na wengine bora hili litakuwa tatizo kwa timu pinzani", amesema Robertinho.

"Nadhani unakumbuka safu yao ya kiungo ilivyokuwa bora msimu uliomalizika, walikuws na watu wabunifu sana eneo hilo kama yule Pacome, Aziz KI na Maxi Nzengeli, anapokeenda na Chama itakuwa ngumu zaidi itategemea na hesabu za kocha wao", amesema Robertinho.

Kumekuwa na taarifa kuwa Chama amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Yanga na kinachosubiriwa ni kumtangaza tu.

Je: Makolo hauogopi .......yajayo yanatisha[emoji3063][emoji3063]
1719493975263.jpg
 
Habari za Chama tumeshazichoka sasa.... hivi hakuna habari nyingine ndugu zangu
"hamjasema mpaka mseme.......na mtasema ×2

"Hamjasema mpaka mseme na mtasema " ....... harmonize verse in sensema

Rayvanny song featuring harmonize [emoji23][emoji23]
 
Nafikiri Simba inahitaji kuachana na Chama ili utulivu upatikane na ibaki imara. Huyu Chama amekuwa wimbo. Ni kweli amefanya makubwa Simba lakini ni wakati wake wa kuondoka sasa.
Japo inauma[emoji23]
 
YANGA ITATISHA SANA MSIMU UJAO KAMA ITAMSAJILI CHAMA - ROBERTINHO

Kocha wa zamani wa Simba, Robero Oliveira 'Robertinho' licha ya kushituka kusikia uwezekano wa Chama kwenda Yanga amesema endapo hilo litatimia linaweza kuleta shida kubwa kwa timu pinzani kwani kikosi Cha Mabingwa hao kitaongeza ugumu katika safu yao ya ushambuliaji.

"Muda unavyosogea Chama anazidi kwenda mwisho lakini haina maana kuwa hataweza kuisaidia Yanga. Tatizo ninaloliona hapa ni kwamba mchezaji bora anakwenda kuungana na wengine bora hili litakuwa tatizo kwa timu pinzani", amesema Robertinho.

"Nadhani unakumbuka safu yao ya kiungo ilivyokuwa bora msimu uliomalizika, walikuws na watu wabunifu sana eneo hilo kama yule Pacome, Aziz KI na Maxi Nzengeli, anapokeenda na Chama itakuwa ngumu zaidi itategemea na hesabu za kocha wao", amesema Robertinho.

Kumekuwa na taarifa kuwa Chama amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Yanga na kinachosubiriwa ni kumtangaza tu.

Je: Makolo hauogopi .......yajayo yanatisha[emoji3063][emoji3063]View attachment 3027539
Amrsahau alikuwa anmpiga benchi, mpaka mashabuki walipomshinikiza?!
 
Bwege huyo yeye si alikuwa nae huyo Chama mbona.hakutisha? hasira za kuachwa hizo
 
Back
Top Bottom