Robinho ahukumiwa miaka 9 kwa kosa la kumshambulia na kumdhalilisha kijinsia mwanamke wa miaka 22

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil na klabu za AC Milan na Real Madrid amehukumiwa kifungo cha miaka 9 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumshambulia na kumdhalilisha kijinsia mwanamke mwenye umri wa miaka 22 raia wa Albania huko Milan mwaka 2013

Sshambulio hilo lilitokea January 22 mwaka 2013 wakati alipoingia mkataba na Klabu ya AC Milan, wanaume wengine watano pia walipatikana na hati kwenye kesi hiyo
==================================================

Former Real Madrid and AC Milan forward Robinho has been sentenced to nine years in prison after being found guilty of sexual assault of a 22-year-old Albanian woman in a Milanese disco in 2013.

According to Football Italia, the assault took place on January 22, 2013, when the Brazilian was contracted to AC Milan. Five other men were also found guilty in the case.

The report outlined the 33-year-old will have an opportunity to dispute the sentence as the Italian law system allows for "several levels of appeal" before any sentence is enforced.

Robinho is currently plying his trade with Atletico Mineiro in his native Brazil, having moved back to the Brasileiro Serie A after a brief stint with Chinese Super League outfit Guangzhou Evergrande in 2015.

Robinho was also accused of raping a university student in a Leeds nightclub in January 2009, per the Telegraph's Chris Irvine. It was announced in April of that year that he would not face charges.
 
Sawa kabisa acha anyooke huko aliko___na Iwe fundisho kwa wengine
 
Mchezaji mpira wa miguu wa timu ya taifa ya Brazil na Atletico Mineiro ya huko huko Brazili, Robinho, amehukumiwa kwenda jela miaka 9 kwa kosa la kushiriki katika tendo la ubakaji wa pamoja (gang rape au mtungo) wa mwanamke mmoja lililofanyika jijini Milan Italia mwaka 2013.

Mahakama kuu ya nchini Italy imemuhukumu Robinho mwenye miaka 33 kwenda jela miaka 9 yeye na wenzake wengine 5 kwa kosa la kumbaka kwa pamoja msichana huyo aliyekuwa na miaka 22 baada ya kumlewesha pombe kwenye Club moja ya usiku.

Mshambuliaji huyo aliyekuwa akiichezea timu ya Ac Milan kipindi hicho cha mwaka 2013, hakuwepo mahakamani wakati uamuzi huo ukitolewa leo. Hata hivyo Robinho amejitetea kupitia mwanasheria wake kuwa yeye hakuhusika katika ubakaji wa msichana huyo na amekwisha kata rufaa.


 
Ukiwa maarufu lazima uwe mwangalifu sana,.. People can be intimidated and take advantage of your status at any point in time,
 
Ingelikuwa wachezaji wote wamefuata tabia kama ya MFALUME MESSI Mchezaji kuwahi kutokea katika dunia ingelikuwa poa sana.
 
Dogo alikuwa na mashauzi sana kipindi yuko kwenye prime tena ndio aliyempa kiburi Dunga hadi akumuacha Dinho kwenye kombe la dunia 2010.

Acha akanyee ndoo wangempiga hata mvua 30 ubakaji sio kosa dogo.
 
Hata hivyo hataenda kutumikia kifungo hichi, amehukumiwa na mahakama za Italy, ila yeye yupo Brazil kwa sasa, sheria za Brazil zinamlinda. hairuhusiwi kumchukua Mbrazil kwao na kwenda kumfunga nje ya kwao. [emoji23][emoji23]
 
Dah huyu dogo nilimkubali sana ila hakudumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…