Robo Fainali kombe la Shirikisho: Madini FC Vs 'Bingwa Mtarajiwa' Simba SC.

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Hatimae ratiba ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) imetoka. Bingwa mtarajiwa wa michuano hii TIMU ya Simba SC atamenyana na Madini FC ya Arusha katika Robo Fainali.
Mtanange huu utachezwa mnamo Machi 18, mwaka huu katika dimba la Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Ratiba ya mechi zingine ni kama ifuatavyo;


Kabla ya kupangwa ratiba hii... niliwahi kupeleka ombi hili TFF.

Japo TFF wamekaidi ombi langu.. Bado kuna nusu fainali na fainali.. naamini hao jamaa hawataweza kutukwepa na huko.. dozi zao zipo pale pale.
 
Angalau umeweka akiba - mtarajiwa.
Hata bwana arusi huitwa hivyo maana ndoa inaweza kuyeyuka
Lakini ungesema mmoja wa watarajiwa!
 
Naona TFF wameahirisha mazishi ya chura churani!!
 
Mwaka huu tunawanyoosha kila upande
 
Baada ya Yanga(kiluvya) Sasa ni zamu yenu Kupewa Kibonde😛😛
Vibonde wakiisha Njooni Huku Kwetu tunawakaribisheni Chamazi,
 
Hivi Simba,Yanga na Azam kutokukutana kwenye hizi round ni coincedence?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…