Da Vincis Code
Member
- Jul 21, 2021
- 15
- 20
Emptied
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wambulu mmeamua kututenenezea storySakata la kujiuzulu kwa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania ndg JOHN BAYO limechukua sura mpya baada ya uchunguzi wetu mahiri kubaini kwamba ndg John Bayo alichezewa karata tatu na Rogarth John Stephen Akhwari ambaye ni mtoto wa “The Legend John Stephen Akhwari”.
Mapema Mwezi January mwaka huu Rogart alimshawishi John Bayo agombee umakamo wa Rais wa RT, Bayo akaghairi na kumweleza wazi kwamba yeye hana vigezo vinavyotakiwa, lakini Rogarth akamhakikishia mzee “Safe Havens” kwa kumuaminisha kwamba yeye yupo kitengo cha “Cyber Crimes” pale Police Mkoa wa Arusha na anaweza kuweka mambo sawa na hakuna atakayethubutu kutoa siri hiyo na akitokea wa kufanya hivyo ata dili naye.
Mzee alipoona amehakikishiwa usalama wake akachukua fomu na baada ya muda mfupi Rogarth akamualika Dr. Tiboroah Arusha ili naye ahahikikishiwe usalama wake na apate bahasha nzito, Tiboroah naye hakusita maana usalama wake upo guaranteed akaja Arusha January hiyo na kukutana na Rogarth, Bayo na kundi la vijana ambao Tiboroah aliaminishwa kwamba ni watemi wa Arusha kumbe wala siyo.
Tiboroah alishangaa kutomona Gidabuday kwenye lile kundi, alipouliza aliambiwa na Rogarth “Gida hana lolote, tumemchomekea tuhuma ya milioni 108 hivyo hawezi sema neno”. Wakati huo wacheza dili hao walisahau yaliyowakuta timu nzima iliyomfanyia fitina Gida; kwamba kabla hawajamaliza kicheko cha kumtoa Gida wakapigwa fimbo moja ikawa chale kwa wote.
Sasa baada ya anguko la John Bayo, Polisi Mjanjajanja Rogarth John Stephen Akhwari ametunga uongo (ambao timu yetu ya uchunguzi imeshindwa kuthibitisha); kwamba Gidabuday ameitukana CCM, tuhuma ambayo imeundwa pale uwanjani kati ya askari huyo na mtu ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa.
Gidabuday alipotafutwa na timu yetu ya siri akiwa kijijini kwao alipoulizwa kuhusu iwapo ameikashifu CCM? - alijibu kama ifuatavyo; “Mimi siwezi kuikashifu Chama Tawala maana nilishawahi kugombea Ubunge kupitia CCM Jimbo la Hanang na nimeilipia kadi yangu ya uanachama wa CCM kwa miaka mingi, wanaodai hivyo kama wanayo ushahidi wawaonyeshe, mimi nipo kijijini natekeleza ile Kauli Mbiu ya KAZI IENDELEE”.
Kinachofuata ni nini? Je ni kweli Bayo alighushi chetI kwa ushawishi wa huyo askari polisi ambaye pia kwa sasa ni Katibu wa Riadha Mkoa wa Arusha? Je huyo askari kama ana ushawishi huo yeye vyeti vyake vipo salama? Je mashindano aliyodai kushinda Ulaya na pengine kumpaisha kazini ni ya kweli?
(UP NEXT TIMU YETU IMEPIGA KAMBI MBULU NA ARUSHA, MAJIBU YATAPATIKANA SOON)