ZVI ZAMIR
JF-Expert Member
- Jun 23, 2015
- 921
- 2,163
Shalom Shalom.
Habari ya jioni. Hongereni kwa Ibada na mapumziko ya wikendi. Leo naomba kwa uchache tushirikishane juu ya Roho Mtakatifu. Kama sehemu ya Utatu mtakatifu yaani Mungu Baba, Mwana na Roho mtakatifu.
Ikiwa wiki moja imetimia sasa tangu sherehe ya pentekoste. Kuna mambo ningependa tushirikishane kwa wale ambao teyari wameshamwamini Yesu Kristo(Wakati mwingine nitaongelea Roho mtakatifu na wale ambao bado hawaamini).
Kumekuwa na mafundisho mengi sana juu ya Roho mtakatifu ambayo kwa sehemu kubwa yameishia kwenye nadharia na sio vitendo halisi vya kuona udhiirishwaji wa kile ambacho kimekuwa kikifundishwa au kuhubiriwa. Kiuhalisia Roho Mtakatifu ndo kila kitu kwenye kanisa la leo katika kumuishi Yesu Kristo kwa uthabiti na uhakika pasipo yeye ukristo unakuwa mzigo mzito sana na mwishoe ni kujipata kwenye misingi ya sheria zaidi. Kama waamini tutajidhatiti kuwa chini ya maongozo yake (Mungu Roho mtakatifu) hakuna namna yale ambayo Bwana Yesu aliahidi kuwa tutayafanya zaidi yake yatashindikanika.
Yako Mengi ya kuyaongea juu ya Mungu Roho Mtakatifu juu ya utendaji wake, na mengi yanayo muhusi kwa namna ya kawaida ambayo kwa hakika kila ataweka nia kufanya majaribio ataona matokeo. Kumbuka ni kupitia nguvu na uweza wa Roho mtakatifu ndimo karama na vipawa vyote hufanya kazi na hata ile hali ya ushuhuda halisi wa mwamini kuthibitika.
Nafahamu hapa watu wengi tu wamekuwa encountered na Roho mtakatifu hivyo maswali yatakayo ulizwa nina hakika yajibiwa kwa kina .Karibuni kwa michango na Maswali..