Roho ya kwa nini inazidi kumtafuna Mavoko

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Siku zote katika maisha ili ufanikiwe inapaswa uwe na moyo mkunjufu ,moyo uliojaa shukurani bila kusahau kufanya kazi kwa bidii na kuwaheshimu wale wote wanaokusaidia ili uweze kutimiza ndoto zako.

Msanii Richard Mavoko ni miongoni mwa wasanii waliojaa chuki, husda na roho ya kwa nini.

Miaka michache iliyopita Mavoko alikuwa kwenye bifu zito na msanii grade one wa kimataifa Diamond Platnumz na kila kukicha alikuwa akimrushia vijembe na kumponda Diamond kwamba hajui kuimba ila anabebwa tu media .
Lakini siku zote Mungu si athumani baada ya miaka miwili kupita 2016 mwanzoni zilianza kama tetesi kwamba Mavoko ni msanii wa WCB bado tu kukamilisha mambo machache ili arasimishwe kwenye lebo hiyo, Mavoko kwa kuona aibu mwanzoni alipinga vikali jambo hilo lakini mwisho wa siku akaja kutia saini kweupe pee .

Ila Mavoko kwa kifupi aliamua kujiunga WCB ili tu aweze kujua mbinu anazotumia Mondi kutoboa kimataifa ili akishazipata hizo mbinu atoke katika hiyo lebo na aanzishe na yeye lebo yake.

Baada ya kuona lengo lake linakaribia kutimia akaamua kutafuta visababu visivyo vya msingi ili avunje mkataba na kutoa visingizio visivyo vya msingi ili mradi alipwe fidia ambayo ingemsaidia katika kuanzisha lebo yake ya Billionears Kids.

Lakini siku zote kwenye haki ,uongo hujitenga licha ya kubuni vijisababu na kwenda kushitaki Basata, Mavoko aliumbuka peupee na mwisho wa siku yeye ndiye aliyeonekana ana matatizo ndiyo maana hata siku zile baada ya kikao alionekana ni mtu mwenye stress nyingi na hasira za kijinga kwa sababu lengo lake lilibuma na akaishia kuumbuka peupe na mbaya zaidi amepoteza idadi kubwa ya mashabiki na ngoma zake wamezisusia ikiwemo ngoma mpya aliyoitoa hivi karibuni.


Mavoko hasira zake ameamua kuzituliza kwa kuwa unfollow watu wote ambao wameegemea zaidi upande wa Mondi ,mfano Ricardo Momo alikuwa ni swahiba sana wa Mavoko ila baada ya Mavoko kuleta chokochoko na Mondi Momo amekuwa akirusha utani wa hapa na pale ambao ulikuwa unamlenga Mavoko jambo ambalo lilimkera Mavoko na kuamua kum unfollow.

Mtu mwengine ambaye Mavoko amem unfollow ni Rommy Jones licha ya kuwa naye alikuwa swahiba wake mkubwa.


Wengine ni hawa , Rayvann,Salam Sk,Babu Tale, Mkubwa Fella na Diamond mwenyewe.
 
Mimi nacho jiuliza, inawezekana kweli mavoko alisain mkataba wa kinyonyaji Kama wanavyosema lakin alishindwa kumaliza hili swala Kwa kuongea Na uongozii wake kweli? Maana mondi anasaidia watu wengi tu , ndio kusema mavoko peke yake ndio anyanyaswe Na mondi Na si wengineo ? Hatua ya kutoka nje Kwa issue inahalibu brand ya label hivyo mavoko angehitaji kusikilizwa ni iman yangu mondi angekubali ili label yake isiwe counterfeited kirahisi, hizi assumptions zinanipa majibu sawa ya mtoa maada kwamba huenda kweli mavoko alikuwa Na lengo la kukatisha mkataba kihuni. Lkn ukitaka kuondoka sio lazima ugomv huo ni uswahili Na chuki pamoja Na husda mbona akina drake wana tangaza kabisa kwamba mwaka huu naondoka kweny label yangu? Hizi assumptions zilijizihirisha pale mavoko alipokuwa Na hasira Sana wwndishi wa habari walipotaka kumhoji!!!!! Mwisho tusimlaum mavoko asilimia zote inawezekana pia hata upande wa pili ikaww chanzo lkn pia mavoko hii hatua ilitakiwa iwe ya mwisho baada ya kutafuta justification za kutosha bila kuacha doubt zozote!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ajiunge na Ali Kiba katika kuurudisha muziki wa bolingo kwenye chart. Tuna-miss sana masebene
 
Wewe mleta mada ndò una roho ýa kwanini.

Wewe unataka Mavoko aendelee tu kuajiriwa pale WCB wakati nae ana malengo yake maishani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…