Roho ya mwanadamu

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Wadau,
Roho ya mwanadamu hutiririka na kuenea ndani na nje ya mwili wa mwanadamu.Kila mwanadamu ana roho,na roho ya mwanadamu sio sehemu ya utambulisho wa mwanadamu bali kila roho ina utambulisho wake ambao ni nje ya utambulisho wa mwanadamu.

Kwa kawaida wengi wetu bila kujua wala kutaka huwa tunabadilishana roho na wakati mwingine huwa tunatumia roho ile ile moja kwa wakti mmoja hasa tunapokuwa katika hali za kipekee kwa wakati mmoja.Mfano nia watu wanpokuwa kwenye makundi kwa muda mrefu au kwa nia moja hujikuta wanaongozwa na roho moja na kujikata wakifanya mambo kama vile wanaongozwa na mashine bila kutumia utashi.

Mfano wa nyakati ambazo watu hushea roho moja ni wakati wa mvuto wa kimahaba,wakati wa hofu inayotisha watu wengi,wakati wa orgasm.Vile vile kwa wanafamilia,watu wanaoishi pamoja kwa muda mrefu kama vile wanofanya kazi pamoja,wafuasi wa ama imani moja au dini moja au kitu chochote ambacho kinaunganisha.

Roho haina uhusiano na mwili unavyofanya kazi bali ina uhusiano na suala la kuwa hai kama ambavyo damu inavyofanya kazi mwilini na kutiririka basi na roho nayo hutiririka mwilini mwako.Roho moja yaweza kutiririka dunia nziima na kuongoza miili yote duniani au miili mingi duniani ingawa hilo halijawahi kutokea

Mtu anapokufa roho inawezakuchangua katia yafuatayo,ama kuendelea kuzunguka na kutafuta mwili mwingine wa kutumia ama kuende sehemu na kukaa tu kwa upweke hasa kama roho haijapata mwili ambao inauona kama unafaa kukaliwa mfano roho iliyokuwa inatirika ndani ya mtu mwovu sana hupata shida sana kupata mwili kama ule na mara nyingi hubaki ikihangaika duniani.

Roho zinazohangaika ni nyingi na nyingine zimebeba kumbukumbu za watu ambao zilikuwa zikitiririka kwao na hivyo zina uwezo kabisa wa kukutokea na kukueleza baadhi ya mambo ambayo watu wao ama waliyaficha au hayakujalikana au hata kukuonya kutegemea na uhusiano wako na watu hao.

Unawezaji kuamsha roho safi ndani mwako?Kuna namna nyingi za kuhakikisha kuwa roho inafanya kazi ndani ya maisha yako tena kazi nzuri,kwanza waza sana kuhusu ile hali ya maisha unayoitaka,pili kila ukipata wakati wa kusema iseme sana ile hali unayotaka,katika sala kwa mujibu wa imani yako,hata kama unaamini katika miti,katika ukristu au katika uislamu.Lengo la kusema ni ili kuhakikisha kuwa fikra na mawazo yako yanavuti a aina yaroho ambayo unataka kuwa nayo

Ukishafanikiwa kuwa na aina sahihi ya roho itakuiwa rahisi kwa wewe kufanya lolote bila wasiwasi na kufanikiwa
Elimu na ujuzi huu sio wa wazi na sio wa kueleweka na kila mtu isipokuwa kwa wachache waliochaguliwa kuelewa hili kwamba ili uelewa hili lazima roho yako itake kuelewa hili.

Ninaandika hili kwa uhakika na kwa utafiti,binafsi nimewahi kuwa na uhusiano na roho za watu ila baadaye niliona kuwa roho za watu hawa zilikuwa safi kuliko uwezo,na mtindo wangu wa maisha.Hili lilitokea miaka mingi sana iliyopita

Hata sasa hivi ninapoandika andiko hili ninaona hali hii ikitokea kwangu yaani kuna kitu kinazuia nisiandike uzi huu ila mimi ninakazana namalize kuuandika ili tuujadili na nitawaomba sana muusome kwa umakini na kuujadili na kwa wale wenye ujasiri fanyeni majaribio na mlete mrejesho.

Kumbukeni sio rahisi sana na kwa wakati unaweza kujikuta unahisi kama unakufa

Itaendelea sehemu ya pili kwa sasa wacheni nilale nimechoka sana baada ya kuita roho ya mtu nisiyemjua,hapa nimeamshwa na mke wangu kwa sababu ya kiherehere chnagu cha kucheza na roho nimejikuta nimepiga kelele kama vile nimeota jambo la kutisha lakini kiuhalisia nilikuwa nacheza na roho nikahisi kuzidiwa na nguvu.

Hapa hadi modem imegoma kufanya kazi ili niswape hii taarifa lakini ninataka niwape hii taarifa ili na nyinyi mjifunze ila kuweni makini msiutumie huu utaalam vibaya kwani unaweza hata kuwa kichaa au hata kufa kama ukikosea kanuni na kanuni zake mimi mwenyewe sijazifahamu kwani bado ni sayansi mpya sana katika namna ambavyo ninaifuata ila katika njia za kidini na kiimani ni rahisi zaidi wewe kuitumia bila kuumia hivo ifanyie zoezi ndani ya mfumo wako wa imani na usiende kwa fujo utaumia.

Wanadamu wote wana uwezo huu ila sasa sio kitu cha kuchezea na kujaribu.

Karibuni katika mjadala
 
Mimi nahisi kuelea kwenye anga za wafu, nadhani muda si mrefu Muumba atanichukua..!
 


1.Una Mahusiano na Roho.!

2.Una uwezo wa kuziita..!

3.Umekurupushwa na na roho ya mtu usiyemjua..!?

Sasa ndugu kama ni hivi, nadhani itakuwa zaidi ya mateso.

Kwa kutuambukiza hiki kiherehere, huoni itasababisha Wake watukimbie.!?

Au ulitaka kutupa taarifa juu ya uwezo wako wa kupiga Ramli.!? Nawaza Tu

Maana maswali ni mengi kuliko Majibu,uzi umekaa kivitisho labda ndio maana wachangiaji wachache.

Ebu ukipata mda uje Tuwekane sawa
 
1. Inawezekanaje Roho ya MTU huyu kumuingia yule.. Naomba ufafanuzi.
2. Hizo roho zinazozunguka hutafuta miili ya watu wazima au watoto ambao ndo wapo kwenye mchakato wa kuzaliwa!?
 
huo ni mtazamo tu hauna uhalisia wowote Roho ni nguvu ya uhai haioni, haina hisia, wala haina uwezo wa kuweka kumbukumbu...ni sawa na upepo au nguvu za umeme..
 
Hii elimu nzuri Sana, ubaya wake inachagua watu wake wa kuielewa. Hakuna lamri hapa its pure science
 
Itabidi niifuatilie niijue nataka niite roho ya Billionaire mmoja hivi nami nitusue hili life
 
Nakubaliana na wewe kuhusu vingine vyote lakini kusema kuwa mnaweza kushare roho moja watu wawili au zaidi, Mimi binafsi nasema huu in uongo mkubwa.
Mimi ninachokiamini ni kuwa roho inakaa kwa mwili was pekeyake. Na inaweza kwenda kurandaranda na kuuacha mwili wake halisi ungali hai na kurudi. Pia inaweza ongoza binadamu mwingine wakati mwanadamu huyo akiwa na roho take mwenyewe.
 
Ninahisi wakati Ghadafi anakaliwa na wananchi wa Libya walikua wamevaa roho moja.ninahisi wakati Chadema ikiwa inaandamana kupinga jambo wanakua wamevaa roho moja.nawaza tu

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
huo ni mtazamo tu hauna uhalisia wowote Roho ni nguvu ya uhai haioni, haina hisia, wala haina uwezo wa kuweka kumbukumbu...ni sawa na upepo au nguvu za umeme..
nakuunga mkono kua roho ni nguvu .mfano gari haiwezi kutembea mpaka itiwe nishati ambayo ni mafuta kwa kutembea so binadam hawezi kufanya chochote kama hana roho. Maana akiwa nayo itaect kama ni nishati kwenye mwili
 
Ninahisi wakati Ghadafi anakaliwa na wananchi wa Libya walikua wamevaa roho moja.ninahisi wakati Chadema ikiwa inaandamana kupinga jambo wanakua wamevaa roho moja.nawaza tu

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
Upo sahihi,Ili muweze kfanya jambo jema au baya kwa umoja bila kuhoje ni lazima waote muwe na roho moja.Roho ina uwezo kuwa sehemu nyingi kwa wakti mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…