Rolnado watatu maarufu duniani walio shinda chukua Ballon d'Or na mchezji bora wa Fifa

Rolnado watatu maarufu duniani walio shinda chukua Ballon d'Or na mchezji bora wa Fifa

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
12,823
Reaction score
21,210
Kuna Ronaldo watatu maarufu sana ktk historia ya soka ambao wamesha wahi kushinda tuzo za Ballon d'Or .
Wawili wanafahamika zaidi kwa jina la Ronaldo mmoja akiitwa Ronaldo de lima na mwingine ni Cristiano Ronaldo.

Huyu wa tatu anafahamika zaidi kama Ronaldinho Gaucho. Ingawa wengi hawajui au wanajua ila hawaja zingatia ukweli kwamba huyu jamaa jina lake halisi ni Ronaldo de Assis Moreira, au maarufu kama Ronaldinho.

Tujiulize kwanini hakupenda kujitambulisha zaidi kama Ronaldo?
Je, alitaka kuweka utambulisho wake wa kipekee hakutaka kutembelea jina la Ronaldo ambae tayari alikuwa maarufu wakati huo?
Kama ni hivyo unahisi jamaa(Gaucho) anajiamini sana kipaji chake hakutaka kutembelea nyota ya mtu?
Mwisho tujiuize Cristian Ronaldo alipendelea kuitwa Ronaldo wakati yeye ni Cristiano kwa vile alitaka kutembelea jina la Ronaldo halisi?

Toa maoni yako mdau.
 
Kiuhalisia watu wengi hutumia majina ya pili Kama utambulisho wao. Kama upo kazini au chuo sidhani Kama unaitwa kwa jina lako la kwanza ivyo ivyo kwa Cristiano
 
kibrazili sufix -inho- ni mdogo hii ina maana hiyo ronald-inho ni ronaldo mdogo.

Ilikuja ili kuweza kuwatofautisha hawa wachezaji wawili masuperstar wa kibrazili kwani walicheza katika zama moja ingawaje ronaldo de lima alitangulia kuwa maarufu.
 
Kiufupi Gaucho alishajicommit kwamba yeye ni Ronaldo mdogo sasa unasemaje kaja na utambulisho wake wakati alikubali kuwa yeye ni mdogo kwa Ronaldo De Lima
 
Kiuhalisia watu wengi hutumia majina ya pili Kama utambulisho wao. Kama upo kazini au chuo sidhani Kama unaitwa kwa jina lako la kwanza ivyo ivyo kwa Cristiano
Sio kwamba aliona fursa ya kutembelea nyota ya Ronaldo mnyama mwenye kasi, akili, na uwezo mkubwa wa kuliona lango la goli?

Anyway, upo sahihi hoja yako kwani Lionel Messi a.k.a 'La Pulga' anafahamika zaidi kwa jina la mwisho yaani Messi.
 
Mtoa mada utakuwa una tatizo binafsi na Cr7 kwani karibia wachezaji wengi hawatumii jina la kwanza kama utambulisho vilevile katika soka hakuna kutembelea nyota ya jina wala nchi kama uwezo wako mdogo utapotea mapema tu wapo wachezaji walioitwa zidane,pele nk. Lakini hawakufika hayo mafanikio kwahiyo badala ya kuwaza kutembelea nyota ya jina waza kipaji cha mtu husika kwanza
 
Ha haa
Hapana mkuu. Nilitaka watu wajue kuna Ronaldo watatu waliobeba tuzo kubwa kabisa duniani katika soka.

Ulikuwa unajua Ronaldinho jina lake halisi ni Ronaldo?
Hilo jina la bahati ktk soka, mpe mtoto wako wa kiume.
 
Yaap nilikuwa nafahamu kwani Ronaldinho ni moja ya wachezaji niliokuwa nawafuatilia sana hata hivyo mkuu ni kweli inaonyesja jina hili lina bahati kwenye soka nitautumia ushauri wako kwa kijana wangu
 
Pongezi zimuendee Ronaldo de lima kwa kulitendea haki jina lake na kuliwekea misingi mizuri jina hili kwa waliokuja kulirithi, safiii sana Ronaldo Luis Nazario De Lima
 
Back
Top Bottom