Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Msanii wa muziki wa hip-hop Tanzania Ibrahim Mussa maarufu Roma Mkatoliki, ametoa maoni yake kuelekea Uchaguzi Mkuu na Serikali za Mitaa, kuhusu masuala ya uongozi na maendeleo ya nchi, akisisitiza kuwa changamoto za maji na umeme zilipaswa kutatuliwa tangu miaka ya mwanzo baada ya uhuru. Kupitia mtandao wake wa Instagram Roma amewataka wananchi kuangalia mbali zaidi ya ahadi za huduma za kimsingi kama maji, umeme, barabara, shule na madawati wakati wa kuchagua viongozi ifikapo 2025.
"Maoni yangu binafsi, 2025 tusimchague kiongozi kwa kutazama tu huyu atatuletea maji, umeme, barabara, shule na madawati. NO!!" amesema Roma.
Badala yake, amesisitiza umuhimu wa kuchagua kiongozi ambaye atavumilia kukosolewa ndani ya miaka mitano ya uongozi wake, kiongozi ambaye hatatishia raia kwa kutoa maoni yao, na ambaye atakuwa tayari kufariji na kutatua matatizo badala ya kutumia nguvu kuwatuliza.
"Hivi kwangu mimi ni bora kwanza kuliko hata hayo maSGR sijui mandege," amehitimisha Roma, akiweka msisitizo juu ya haki za raia na uhuru wa kujieleza kuwa ni kipaumbele kikubwa.