Roma na wimbo wa k

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,959
Reaction score
24,935
Ninavyomjua mimi ROMA ni msanii ambaye alianza na nyimbo za kiarakati
Yaani aliifanya HIP HOP yake kuwa kama njia ya kuikosoa serikari .
Mashairi ya nyimbo zake yalilenga zaidi kuelezea moja kwa moja maisha halisi ya MTANZANIA na kile kinachondelea katika Jamii,makosa na nini serikari inaitaji kufanya ili kuleta maendeleo ,

Dhumuni la kuandika uzi uuh ni kuhusu Nyimbo iliyotoka kwa Jina la K,
ingawa si yake ya kushirikishwa lakini kulikuwa na umuhimu wowote wa ROMA kukubali kushiriki kuimba wimbo huo ukizingatia na maudhui ya Wimbo wenyewe,
ROMA yule wa kiarakati ni kweli kakubali vipi kuimba huo wimbo ukizingatia heshima yake na jamii ilivyokuwa inamchukulia?
Hili ni swali ambalo kila nikikaa najiuliza tangu siku nilipoisikia nyimbo iliyopewa jina la K



MZIZI MKAVU.
 
Siku zote katika fasihi tunasema Msanii katika kazi yake yeyote huitazama Au kuiakisi jamii yake na huifanyia kazi ya kisanaa hivyo bhaasi.. .Roma kushirikishwa sioni shidaa Iwe ni Siasa utamaduni au jambo lolote yupo sahihi
 
...dah,basi tu kwa heshima yako humu imebidi nikaushe tu!,ila
..ukiona huelewi,HAIKUHUSU!
 
ndio k
.
mlitaka alale njaa? maisha magumu sio zama za kuimba harakati...
halafu show hupati unakazi ya kutunga mashairi magumu... kwenye vina uweke mara mwakyembe mara mwigulu!!
unadhani mchezo[emoji23]
kaona afanye mziki unaotakiwa maisha yaendelee!
hajaajiriwa na chadema[emoji23][emoji23]
 
Roma ali hit sana na nyimbo zake ila sasa hivi kaufyata
 
Ameleta kibwagizo, asili yake hataiacha......wapenda vigodoro na shughuri hapa ndio mahali pake. Ameamua kuwapa raha na majirani waliopo upande wa pili
 
Hiyo ID inachanga sana na Mdau MziziMkavu,Ungeomba Mods wa Add hata Mzizi Mkavu Jr au Mzizi Mkavu II ili kutofautisha na Nguli mwenyewe.
 
mkuu..!
unasema kila ukikaa unajiuliza hilo swali..

mi nakushauri lisikupe tabu achana nalo.. mbona yapo maswali mengi ya maana ya kujiuliza! hilo lisikupotezee muda mkuu..!

ila kwa upande mwingine..
mi naona tupunguze Negativity juu haya masuala..
binafsi sioni tatizo yeye kuimba kisingeli chenye ujumbe kama huo .. maana visingeli vingi huwa ndio vinamaudhui ya Uswahilini hivyo hivyo.. wengine huuita ni mziki wa wahuni.. na hata Roma nae akili zake huwa anazijua mwenyewe yule mi hata simshangai..

Anyways..
hawa watu wanatafuta channel ya kufanya kazi zao.. waache wafanye kazi .. si unaona hali ilivyokuwa ngumu mtaani.
 
Sawa mkuu nimekusoma
 
Sio mjinga, amesoma alama, asije mfuate Lema Segerea, kumbuka Mimi huwa sijaribiwi, wala sutajaribiwa. Bora aimbe K maana hainaga ushemu
 
Kwani maudhui yake ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…