Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Petr Kellner
Taarifa mbalimbali kwenye duru za michezo zinaeleza kwamba mabilionea wawil Roman Abramovich na blionea wa kutoka jamhuri ya Czech aitwae Petr Kellner wanataka uuziana timu ya Chelsea ya Uingereza.
Roman Abramovich ambae hivi sasa anaishi nchini Israeli na ni raia wa huko, anataka kufanya mazungumzo na bilionea huyo ambae nae kama Abramovich yumo kwenye orodha ya mabilionea wanaotambulika kwenye jarida ka Forbes.
Abramovich ambae aliinunua timu ya Chelsea mwaka 2003 kutoka kwa Ken Bates, anataka kuuza sehemu ya hisa ili kupata fedha zaidi za kuwekeza kwenye miradi yake iliyopo nchini Israel.
Katikati ya mwaka huu Abramovich alikataa offer ya pauni bilioni 2 kutoka kwa mfanyabiashara wa Uingereza aitwae Jim Ratcliffe.
Petr Kellner anatajwa kuwa na utajiri wa kiasi cha pauni bilioni10.2 swa na dola bilioni 12.
Katika orodha ya mabilionea wa dunia Kellner ambae ana umri wa miaka 54 anashika namba 88.
Chanzo cha habari ni gazeti la Czech liitwalo Tyden.
EXKLUZIVNĚ: Petr Kellner má zájem o fotbalovou Chelsea