Ronaldinho alikuwa zaidi ya Messi Barcelona


Yaani hata kwenye 20 bora ya Brazil hayumo?
 
Sawa embu niambie, amesaidia vip kwa hizo facts zako kwa timu ya taifa Argentina? Mm ninavyofahamu ktk soka mafanikio ya timu au mchezaji ni mataji tu,

kwa kigezo chako pedro wa barcelona ana mchango mkubwa sana kushinda Ronaldo de lima ambaye pia alicheza barca....kwa sababu amechukua mataji mengi zaidi yake...kimsingi mataji pekee sio kigezo cha ubora wa mtu.... ni kheri umpime mtu kwa individual awards
 
kwa hio wote wana medali ya Champions League...

ok Dinho Mnyama kabeba World Cup Mara 1.

haya vp kuhusu Nesi?

Nilijua tu utakimbilia huko! Soma heading ya thread, usikurupuke! Tunazungumzia impact ya Dinho na Messi kwenye klabu ya Barcelona!
 

Kapimwe akili wewe, sio mzima!
 

Mkuu, umemaliza. Kina Gang Chomba badala ya kutuletea numbers wanaleta siasa kama Magufuli!
 
Last edited by a moderator:

Tatizo Gang Chomba na wengine wanasumbuliwa na mahaba niue. Mimi nimeshampa Gang Chomba statistics mara kibao ku-crush msemo wake maarufu wa "Ronadinho made Barca and Barca made Messi". Lakini haelewi, utafikiri kanyweshwa maji ya chupi!
 
Last edited by a moderator:
Ronaldhinho on Messi Breaking Pele's record

Reporter : Messi breaks Peles record is he better than Pele?

Ronaldinho : To be better than pele you have to win 3 world cups. Not to score against Zaragoza ; Getafe and Mallorca #Dinho
 
Asante Mungu kwa kumshuhudia Messi,,na kwa mambo aliyoyafanya messi,mchezaj atakaye weza zaidi yake,basi huyo atakuwa Malaika,,,messi amefanya mpira uonekane mwepesi while si hivyo,Alikua Pele na maradona,,ila messi ameshaingilia show,,ukimtaja pele na maradona jna la messi linakujia kichwani automatically,,,Na messi akiwa na miaka 23 hta angeacha soka,tayar ameshakuwa legendary
 
Kustaafu kwa Lionel Messi kuichezea timu ya taifa ya Argentina kumeigeuza nchi hiyo juu chini siku kadhaa zilizopita, taifa lote likitetemeshwa na habari hizo baada ya Chile kuwafunga tena kwenye fainali ya Copa America.

Rais wa Argentina Mauricio Macri, Meya wa Buenos Aires Horacio Rodriguez Larreta na mungu wa soka Diego Maradona wamemuomba mshambuliaji huyo wa Barcelona kubadili mawazo yake na huenda ujumbe wote unaosambaa umekuja kupitia mwalimu wa Entre Rios Yohana Fucks.

Ombi lake limebamba kwa mamilioni ya mashabiki wa Argentina ambao wanatamani sana Messi abadili wazo lake la kustaafu soka la kimataifa.

Barua kamili kama inavyosomeka:

"Lionel Messi,

"Yawezekana usiisome barua hii. Lakini naiandika, si kama shabiki wa soka lakini kama mwalimu wa Argentina, kazi ninayoipenda kama unavyopenda ya kwako.



"Ningeweza kukuandikia kuhusu vipaji vyako vya kipekee katika mchezo maarufu nchini mwetu, furaha ninayopata kuwa na fursa ya kuona kizazi cha soka na kwa bahati njema kabisa kukushuhudia ukifanya miujiza dimbani hali kadhalika jinsi unavyokonga nyoyo za mataifa yote duniani. Kuelezea hayo nitakuwa narudia mambo. Badala yake nataka unisaidie kutatua changamoto kubwa kuliko uliyokabiliana nayo wewe. Nataka unisaidie zoezi gumu la kurekebisha tabia za watoto ambao wanakuona kama shujaa wa soka na mfano wao wa kuigwa.

"Hajalishi ni kiasi gani nina mapenzi na ubobezi katika kazi yangu, siwezi kupokea sifa nzuri sana kutoka kwa wanafunzi wangu kama ninavyokukubali. Sasa wataona mfano wao wa kuigwa ukikata tamaa. Nakuomba usiwaridhishe watu dhaifu; wale ambao wamekasirishwa kwa kushindwa kutimiza ndoto zao maelfu ambazo walishindwa kutimiza kama wachezaji soka, wale ambao wanazungumzia mapumziko kwa sababu ni jambo rahisi kutendeka. Unasikia hili kutoka kwa mwalimu, ambaye licha baina yetu, lakini nashughulika na tabia za Argentina za kudhani kazi ya mtu mwingine ni rahisi, kwamba kufunga magoli ni rahisi kama kujenga nyumba au mustakabali kwa ajili ya mtu. Ni mtazamo huo unaoangusha wengi au kuzusha hoja za kijinga zikiambatana na dharau na jazba juu ya ufanisi wa wengine, kuthamini ushindi tu na kuhesabu makosa kuwa ni kushindwa, makosa hayo hayo ndiyo yanayotufanya tuwe watu na tuendelee kujifunza.

"Tafadhali usiache soka, usiwafanye wachezaji wangu waamini kwamba nchi hii inajali ushindi tu kwanza. Usiwaonyeshe kwamba hata uwe umefanikiwa kiasi gani hutaweza kuwafurahisha wengi, na usiwafanye waamini kwamba wanaishi ili kuwafurahisha wengine. Usiwape ujumbe wa makosa, licha ya kukabiliana na changamoto nyingi hadi umekuwa maarufu leo hii.



"Iwapo mtu kama wewe, mwenye familia inayokuunga mkono, ukiwa na utajiri na mashabiki wengi, huwezi, wataaminije kwamba wanaweza kukabiliana na vita hizo nyingi usiku na mchana?

"Siwaelezi ni jinsi gani Messi anacheza soka la kuvutia, lakini maelfu ya mashuti aliyopiga kufanya mazoezi ya kupeleka mpira katika kona ambayo kipa hawezi kufika. Nawaeleza kuhusu Messi anayepata maumivu ya kuendelea kukimbiza ndoto zake; Messi ambaye kwa fedha zote alizo nazo amefanikiwa kuwasaidia watoto wenye mazingira magumu; Nawaambia kuhusu Messi aliyepevuka; baba wa familia na anayefanya kazi muhimu duniani, mzazi mwema; Messi ambaye anakosa pia penalti, makosa yetu ndiyo yanayotufanya tuwe wanadamu, na hii inadhihirisha kwamba mchezaji bora hukosea pia.

"Usikate tamaa, usitupe fulana yenye rangi za nchi yetu mbali nawe, fulana hii ya Argentina inatuwakilisha sote. Tafadhali usiwafanye wanafunzi wangu kuamini kuwa wao ni watu wa kushindwa.


"Wanafunzi wangu wanahitaji kuelewa kwamba mashujaa, wawe ni Madaktari, askari, waalimu au wacheza soka, ni wale wanaojitolea kwa ajili ya wengine hata wakijua kwamba hakuna anayewathamini au kuthamini kile wanachotoa, lakini wakiamini kwamba ushindi utakuwa ni wa wote, na kushindwa kutakuwa juu yao wenyewe. Lakini pamoja na yote hawakomi kuthubutu. Lakini pia wana ujasairi ndani yao, wanapopambana dhidi ya kushindwa hata ulimwengu wote ukisema hatutashinda.

"Na siku moja watafurahia ushindi mkuu: Watafurahia pamoja na changamoto zote walizokabiliana nazo.

"Kila mmoja huzungumzia mpira, lakini naamini moyo wako ni thabiti."
 
RONADINHO.... Yeye aliufanya mpira uwe burudani, yaani kama muziki tu.. aliweza kuutuma na kuuamuru alivyotaka na mpira ulitii, unapomuangalia akiwa ameshika mpira unajikuta unatabasamu ni kama unamuangalia mtumbuizaji jukwaani, hakuwahi kuwa serious sana au kuukamia mpira daima kwake aliurahisisha sana mchezo wa mpira wa miguu, kwangu huyu ndo MCHEZAJI MWENYE KIPAJI ZAIDI CHA SOKA.

MESSI.... Mpira kwake ni matokeo ya mwisho, hakuna manjonjo yoyote ambaye yanamtambulisha kama ilivyo kwa Ronaldinho, au Zidane, yaani kuna pasi au kuna chenga ikipigwa unajua hii ilikuwa staili ya fulan lakin Messi hana staili inayomtambulisha kiasi cha wengine kuiga, daima hufanya bidii kwenye kutafuta nafasi ya kufunga au kutoa pasi ya hatari kwa mpinzani.. kwangu Messi ndo MCHEZAJI MWENYE MADHARA ZAIDI.
 
Kweli mkuu ...kinachoniuma mimi ana wengi ni kukosa kiumbe mpya mwenye kariba ya dinho katika karne hii ...

Hakuvunja rekodi nyingi katika historia yake wala kufunga mabao mengi ila aliufanya wengi tupende mpira wa miguu na miujiza yake akiwa uwanjanii ...sikuwahi kuona akitumia nguvu yeye na mpira mpira na yeye na tabasamy lake usoniii what man in football history ...[emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]

Ronadinho aliufanya mpira kwake kitu simple tu kama kumsukuma mlevi ...na mpira ulimpigia salute
 
Kabisa, jamaa alkuwa na kipaji cha hali ya juu sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…