Alipohamia AC nikajikuta ninatazama Mechi za AC Milan, ikawa akitoka dakika za 70 au 80 na mimi nazima TV naenda chumbani kupumzika. Ronaldinho Gaucho, kijana pekee aliyependwa na kila mtu, hata madridista walimpenda, mpaka mashabiki wa EPL walimkubali sana kutokana na mbwembwe zake uwanjani na kucheka kwake.
Libarikiwe tumbo lililomleta LIONEL ANDRES MESSI DUNIANI, huyu mtoto hana mbwembwe wala sio mtu wa show off na hanaga mzaha uwanjani kama Gaucho na hii ndio sababu pekee mashabiki wa EPL wakisikia Jina la Messi lazima washikwe na hasira.
Lionel Messi, mtu pekee awezaye kuyafanya matokeo ya mechi yakae mguuni pake wa kushoto.