Ronaldinho reveals his Champions League dream team

Wapi Etoo?

Ndo ushangae hapo... jamaa kabugi kwa hilo.

Eto'o was just lucky to play in one of the great team.

Sasa hapo ungemtoa Henry au Ronaldo de Lema umweke Eto'o?

Eto'o alivyoondoka Barca na mpira wake ukaishia.

Bora akina Ibrahimovich anatepeta mpaka leo. Then kuna akina Shevchenko.

Ila kwenye timu yangu ya Champions League nitamweka Inzaghi aka the goal poacher. Yule jamaa utafikiri mwizi anayeiba bila silaha.
 
Gerrard? Raul? Eto'o? Kwa uchache tu.
Zidane????

Labda Zidane hapo. Jamaa alikuwa mashine nyingine.

Kuhusiana na Gerrad na Raul jiulize mbona hata akina Iniesta na Xavi hawapo?
 
EMT;

mi nahisi mapinduzi ya defensive yaliletwa na Gilberto Silva ktk world cup ya mwaka 2002...

Inawezekana bse Makelele was not the first holding midfielder. But during his time alionyesha jinsi nafasi hiyo inavyotakiwa kuchezwa.

Silva alikuwa influential, but Makelele became the incumbent of the position mpaka ikabatizwa "Makelele Role".

Baada ya kutamba sana, Makelele Role imekuja kuuawa na Barcelona's style of playing.

Style mpya ya ku-press higher up on the pitch inahitaji kuwa good passers. Ndo maana siku hizi nafasi hiyo imetawaliwa na watu wanaoposse mpira kama akina Pirlo,
Busquets, Matic, Wanyama, nk.

Enzi za kina Gatuso hazipo tena. Hata Makelele alipoondoka Chelsea hakuchezea tena ile role yake.
 
Last edited by a moderator:
juzi nilimwona makelele pale kwenye bench la PSG nilikumba mengi sana

He was a game spoiler. Mnapanga mashambuzi fresh jamaa anatibubua.

Nakumbuka kuna mechi moja kati ya Man Utd na Chelsea ambapo kazi ya Rooney ilikuwa ni kula sahani moja na Makelele.

Ndo mechi ambayo niliona Makelele akishindwa kufanya kazi yake. Rooney hakumpa nafasi afagie and that was the talking point of the game. Mwisho Man Utd walishinda goli moja.
 

ni kweli mtazamo wake lakini ronaldo de lima wa uefa hawezi kuwa juu ya eto'o au shevchenko
 

spoiler kuna game chelsea walicheza na liverpool UEFA matokeo yalikuwa 4&4 sasa makelele alimkaba geradi vya kutosha,geradi alipiga shuti moja tu tena lilikwenda nje kabisa
 
Makelele moja ya mashujaa wasioimbwa...shujaa wa Chelsea kwa msimu wa 2004-05
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…