Ronaldo alivyojibu Messi kwa kuwasomesha namba mashabiki wa Barcelona pale Camp Nou

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Kama unakumbuka ilikuwa Aprili, mwaka huh pale Lionel Messi aliposhangilia baada ya kufunga bao mwishoni katika El Clasico kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, Madrid, akaamua kushangilia kwa kuwaonyesha mashabiki wa Madrid jezi yake.

Messi aliionyesha jezi hiyo kwa mashabiki wa Madrid na kuzua gumzo, lakini leo Cristiano Ronaldo naye amejibu akiwaonyesha mashabiki wa Barcelona jezi namba 7, waisome baada ya kufunga bao la pili katika mechi ya Spanish Super Cup.

Madrid imeshinda kwa mabao 3-1 katika mechi hiyo lakini Ronaldo aliyeingia, alikumbana na red card baada ya kupata yellow mbili. Mechi ya pili dhidi ya timu hizo itakayopigwa Agosti 17 kwenye dimba la Santiago Bernabeu itaamua bingwa.

Mytake: Hii inaitwa tit for tat kudadekiπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€


Baada ya kufunga bao hilo alivua jezi na kuwaonyesha mashabiki hao, sawasawa na alivyofanya Messi, Aprili, mwaka huu.
 
Messi yeye siku ile alivua kutokana na kazi kubwa aliyofanya ya kupiga bao mbili na bao la mwisho la ushindi ambalo lilipatikana muda mchache kabla mpira kumalizika.

Ila hawa watu wameacha rekodi kali sana watakaozivunja huwenda wakavunjika wenyewe kabla ya kuvunja rekodi zao.

Usinisahau kwenye Baraza Jipya.
 
Angalia Messi alivyovua ndani alivaa nini? Acha mapenzi ya bata!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…