Ronaldo atengeneza Tsh. Bilioni 2 kwa kila post ya udhamini (Instagram)

Drop shipping Tanzania

Senior Member
Joined
Jun 15, 2020
Posts
198
Reaction score
481
Instagram ya Ronaldo: Atengeneza Tsh Bilioni 2 kwa kila post ya udhamini

KARIBU

Nyota wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo, ametakiwa kukodisha akaunti yake ya mtandao wa Instagram kwa dau nono kwa muda wa mwaka mmoja.

Shirika kubwa la uwekezaji la Marekani lilimpigia simu nyota huyo na kumuahidia kumlipa donge nono la Euro milioni 100 awakodishe kwa kipindi cha mwaka mmoja ukurasa wake binafsi wa mtandao wa Instagram.

Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kwamba Ronaldo aliwajibu kwamba atalifanyia tathmini pendekezo hilo.

Ronaldo ana wafuasi wapatao milioni 187 katika mtandao wa Instagram, aliingiza kiasi cha Paundi za Uingereza milioni 38.2 kutoka shirika hilo.

Cristiano Ronaldo ndiye nyota anayeingiza pesa nyingi kupitia akaunti yake ya Instagram, katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita katika post za Instagram 49 kwa wastani alilipwa kiasi cha Dola 975,000 kwa kila posti moja ambapo kwa mwaka mzima idadi inafikia Dola 47.8 Milioni (Takribani TShs Bilioni 109.8).

Toa maoni yako 🙂
 
Dunia hii kuna watu hata wakiuza mavi yao watapata wateja wa kununua.
 
Aiseeee inakatisha tamaa kwa wasanii wetu wanaolipwa Buku 10 kwa Post.
 
wale wa Lumumba waakula buku ngapi kwa post???
 
Hawa ndo wanofaidi mitandao ya kijamii,..sio madada zetu wanaokesha kutuma picha tu..wakiwa kwenye magari ya kuazima
 
Hakuna mtu anayelipwa huku Africa wanaolipwa wote ni watu weupe.
Hapana Mkuu,

Wapo wengi wanaolipwa kwa Afrika kutokujali asili zao kama ni Chocolate, Cappuccino, Coffee, Banana au Wheat Bread!

Mfano, C4 Pedro (Angola) Ameweka scale tatu ya 1. TZS 6+ Million, 2. TZS 3.5+ Million na 3. TZS 400k - 2 Million PER Post kupitia Instagram.

Red One (Maroc) TZS 9+ Per 1 Post + 1 Sponsored Ad!

And Co...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…