wapi tunapata hiyo? tuelekeze please, wengi tunataka kujenga kwa hiyo.Go for mangalore from India they're da best 100yrs guarantee,zile nuymba zote za Magufuli (oysterbay),zilezekwa na vigae hivyo since then.Ule ni udongo uliokwa, ni vyepesi mnoo, sio yale mabati yanayomwagiwa uji kwa juu,au yale mavigae ya Mbezi Tile ambayo ni Cement na Mchanga.
uimara si sana kwani hata ati la geji 30 linafikisha miaka 30 bado linadunda tu
zaidi wanachoangalia watu ni show na ile sense of 'na mimi ninazo'
Go for mangalore from India they're da best 100yrs guarantee,zile nuymba zote za Magufuli (oysterbay),zilezekwa na vigae hivyo since then.Ule ni udongo uliokwa, ni vyepesi mnoo, sio yale mabati yanayomwagiwa uji kwa juu,au yale mavigae ya Mbezi Tile ambayo ni Cement na Mchanga.
Mkuu receive my honest and unbiased advice! Kama kauwezo cha fedha kapo nenda Nabaki Afrika kuna roof tiles(vigae) toka New Zealand. Wanaziita decra tiles. Unapewa guarantee ya 50 years against rust na 25 years against colour fading. Hii written guarantee from the manufacturer, New Zealand. Zipo tiles za aina tofauti kuna nyingine zina coat ya sand wanaziita sand blosted kama sikosei na nyingine hazina iyo coat wanaziita smooth decra tiles.
Kwa upande wa bei zile za sand coat zina bei zaidi kidogo ya hizi smooth. Mwaka 2011 nilinunua hizi smooth kigae kimoja kilikuwa Tsh. 13,750 wakati chenye sand kilikuwa 16,350. Vilevile ukiwa na roof plan (ramani) ya nyumba yako wanaweza kukusaidia kuestimate idadi ya vigae. Pia utuziwa na accessories zake kama kofia, misumari na gundi yake. Kifupi ni kuwa naiona thamani ya hela niliyoitoa maana roof lina ubora na lina pendeza!
Kigae kimoja kina ukubwa gani? rephrasing, kwa nyumba ya sq. m 120 simple roof approximately ni vigae vingapi?
Thanks so much mkuu. Umetupa practical experience nzuri sana. Je kuna tofauti kati ya kigae cha South na New Zealand katika ubora na bei?
Mkuu kigae kimoja kina urefu wa 1320mm (1.32m) na upana wa 370mm (0.37m). Kwa suala la kuestimate itakuwa ngumu kwangu maana sio mjuzi wa archtecture ila kwa experience nyumba yangu ina sq. m 292 nilinunua vigae around 650. Ila hapo nilimodify kidogo roof nikaongeza pitch hesabu ikaongezeka kidogo. Kwa roof plan niliyokuwa nayo walinipigia hesabu ya vigae 594. Hope sasa unaweza kuadjust mahesabu haya kwa kipimo cha nyumba yako. Ila pia ujue idadi inategemea aina ua roof.
Hivi ni kweli vigae vinaweza kuleta cancer