Roofing materials: Aina mbalimbali, faida na hasara zake

Hivi ni kweli vigae vinaweza kuleta cancer

Kuna roofing sheets zilikuwa zinaitwa asbestos tiles .... hizi zilikuwa zinatengenezwa kwa kutumia asbestos materials ikichanganywa na sisal fibres (mkonge) pamoja na cement .... kuna uwezekano mchanganyiko huu ilisababisha miale na harufu isiyogundulika ambayo kiasi flani ilichochea (aggrevate) growth of cancer desease .... siku hizi asbestos hazitengenezwi tena

pia ninashauri tuwe makini na roofing tiles za aina mbalimbali kwa kuangalia finishing coat ya roof tiles ( mpako wa kigae) kwani nyingi zina chemicals ambazo zaweza kuwa na madhara mwilini .... angalizo hili ni pale paa linapotumika kuvunia maji (rainwater harvesting)
 
Mkuu uko sashihi kabisa, na kwa kuongezea, vigae vya Magufuli alivinunua Nabakia Afrika na sio vigae vya India kama mdau alivyosema. Mshua wangu alimuuliza dr. kwani hata home tumeezekea hivyo vigae. Magufuli aliezeka tangu yr2000 na mpaka sasa viko vile vile. Tuliezeka 2008 na mpaka sasa viko poa.

Angalieni soko la ferry, pale stand mwenge au hata ubungo nyumba zilizo karibu na oilcom. Ni decra mkuu, walitupa mifano hai. Nenda mbezi sasa, decra balaa tupu, but beware of fake ones, pigia sim Nabaki wakueleze wenyewe. Au visit www.nabaki.com kupata contact na details zao.
 
Hivi sqm za nyumba (floor) zinaweza kukupa mwanga kwamba paa lako litakuwa na sqm kadhaa (i.e. baada ya ku factor in urefu wa kingpost etc)?

Mfano, sqm 250 za nyumba ni sawa na sqm ngapi za paa?
 
Hili somo linatuhusu wengi wakuu! Vigae vya msouth vinauzwa shingap kwa kimoja hapo Nabaki Africa? Na kina ukubwa gan? kwa mfano nyumba ya Sqm 250 inaweza kuingia vigae vingap?
 
Anayejua Costs za Ando Tiles atuambie tafadhali
 
Inadidi moderator atuwekee ukumbi wa ujenzi now !

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Kitu Kigae cha udongo MANGALORE unapata guarantee ya miaka 100.Tangu mkoloni mpaka leo kinapeta.Hakina joto wala baridi hskiungui na ajali ya moto hakipauki
 
Wakuu mie nataka nifahamishwe aina ya marumaru ambayo ni zuri kwenye nyumba ya makazi.
 
Nyumba yetu imejengwa kwa mabati ya asbestos toka mwaka 1992, tumekulia humo na hadi sasa tu watu wazima (wameoa na kuolewa) hamna aliyepata madhara yoyote na huwa tunavunia maji ya mvua na tunatumia kwa matumizi yote kupikia na kufulia n.k.
 
Mwaka 1992 si juzi tu hapa? Madhara huonekana baadae sana. Niliwahi sikia jambo hilo muda nrefu sana, tuombe wenye ushahidi wa kisayansi watujuze.
 
Kitu Kigae cha udongo MANGALORE unapata guarantee ya miaka 100.Tangu mkoloni mpaka leo kinapeta.Hakina joto wala baridi hskiungui na ajali ya moto hakipauki
Hivi hii kitu yapatikana East Africa?
 
Nyumba yetu imejengwa kwa mabati ya asbestos toka mwaka 1992, tumekulia humo na hadi sasa tu watu wazima (wameoa na kuolewa) hamna aliyepata madhara yoyote na huwa tunavunia maji ya mvua na tunatumia kwa matumizi yote kupikia na kufulia n.k.
Asbestor inawezeka ikawa na madhara kama ndani hujaweka ceillingboard.nina ushahidi kuna familia hawakuwa na ceillingboad ndani walisubuliwa sana na TB,mpaka walipogundua ni mabati ya asbestors ndio ilikuwa chanzo.baada ya kuweka ceillingboard TB ikatoweka mpaka leo.
 
Kitu Kigae cha udongo MANGALORE unapata guarantee ya miaka 100.Tangu mkoloni mpaka leo kinapeta.Hakina joto wala baridi hskiungui na ajali ya moto hakipauki
Mkuu BONGOLALA hii thread ni ya kitambo sana lakini naomba kuifufua. Vigae vya Mangalore vinapatikana wapi hapa Tanzania na kwa bei gani?
 
Acha uongo mkuu,asbestos haiwezi kuwa chanzo cha TB hata siku 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…