Rooney:Ninasubiri kwa hamu sana kwenda Tanzania

SDG

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2017
Posts
7,631
Reaction score
8,073
Nyota wa soka wa England Wayne Rooney, ambaye amekamilisha uhamisho wake kutoka Manchester United na kurejea Everton amesema anasubiri kwa hamu sana kuzuru Tanzania.

"Naisubiri sana kwa hamu na ghamu (safari ya kwenda Tanzania) - inafaa kuwa safari nzuri," aliambia runinga ya evertontv.

"Itakuwa nzuri sana na natumai kwamba nitaweza kuingia uwanjani na kucheza.

"Huwa vizuri sana unaposafiri na timu. Ni vizuri kuwa hotelini na wachezaji, kujumuika nao na kuwafahamu zaidi.

"Sijawahi kwenda Tanzania, na kwa hivyo nasubiri sana kwenda huko."

Rooney atakuwa kwenye kikosi cha Everton kitakachocheza mechi ya kujiandaa kwa msimu ujao katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Amesema ziara hiyo itampa fursa mwafaka ya kufahamiana na wachezaji wenzake wapya.

says Everton's pre-season trip to Tanzania provides the perfect opportunity for him to get to know his new teammates.

Rooney, anayeongoza kwa ufungaji mabao England alitia saini mkataba wa miaka miwili Goodison Park Jumapili.

Rooney alifika kwa mazoezi USM Finch Farm leo Jumatatu na anapangiwa kuungana na wenzake kwa safari hiyo ya Tanzania baadaye wiki hii.

Bbc

May Allah bless Me and You
 
Karibuni Everton na Rooney

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Reactions: SDG

May Allah bless Me and You
 
Heheh naona watu wanashindana na joseverest sasa

Sent from my Iphone 7 using JamiiForums mobile app
 
Reactions: SDG
Kila la heri Wazza the legendary, the captain.
 
Nyota wa soka wa England Wayne Rooney, ambaye amekamilisha uhamisho wake kutoka Manchester United na kurejea Everton amesema anasubiri kwa hamu sana kuzuru Tanzania.

"Naisubiri sana kwa hamu na ghamu (safari ya kwenda Tanzania) - inafaa kuwa safari nzuri," aliambia runinga ya evertontv.
"Itakuwa nzuri sana na natumai kwamba nitaweza kuingia uwanjani na kucheza.

"Huwa vizuri sana unaposafiri na timu. Ni vizuri kuwa hotelini na wachezaji, kujumuika nao na kuwafahamu zaidi.

"Sijawahi kwenda Tanzania, na kwa hivyo nasubiri sana kwenda huko."
Rooney atakuwa kwenye kikosi cha Everton kitakachocheza mechi ya kujiandaa kwa msimu ujao katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Amesema ziara hiyo itampa fursa mwafaka ya kufahamiana na wachezaji wenzake wapya.

says Everton's pre-season trip to Tanzania provides the perfect opportunity for him to get to know his new teammates.

Rooney, anayeongoza kwa ufungaji mabao England alitia saini mkataba wa miaka miwili Goodison Park Jumapili.
Rooney alifika kwa mazoezi USM Finch Farm leo Jumatatu na anapangiwa kuungana na wenzake kwa safari hiyo ya Tanzania baadaye wiki hii.

..Wayne Rooney was 18-years-old when he left Everton for Manchester United in 2004 and returns to the club at the age of 31

Vijana hao wa Ronald Koeman watacheza dhidi ya mshindi wa Kombe la Super Cup la SportPesa, Gor Mahia kutoka Kenya, katika mechi ya kirafiki Alhamisi.

Mechi hiyo itakuwa ya kusherehekea udhamini mkubwa uliotolewa na Sportpesa kwa Everton.
Rooney, 31, tayari anafahamiana na baadhi ya wachezaji wa sasa wa Everton.
Amewahi kucheza pamoja na Morgan Schneiderlin, Michael Keane, Phil Jagielka, Leighton Baines na Ross Barkley baadhi ya klabu na wengine timu ya taifa.

Chanzo BBC Swahili
 
Heheh naona watu wanashindana na joseverest sasa

Sent from my Iphone 7 using JamiiForums mobile app
Kabisaa mkuu kijana kaja juzijuzi anawahije nafasi za wazee

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Dah aise watu wangejua umuhimu tuliopata na bahati kwa rooney kuandika neno tanzania kwenye social networks na everton official website...aiseee
 
Reactions: SDG
Muda si mrefu utaona wakenya watakavyo anza mambo yao yale.....
 
Akija apewe Mtaa wa Lumumba...

Sent from my Diamond Rose Iphone 32 GB using JamiiForums Mobile App
 
Reactions: SDG
Nafasi ya bashite kujitangaza baada ya ukimya mwingi. Dvd za Nje zinauzwa kama kawaida tena
 
Reactions: SDG
Fursa nyingine nchi yetu kujitangaza kiutalii

Sent from my GT-N7100 using JamiiForums mobile app
 
Harmorapa ana kitu cha kufanya hapa, hapaswi kuacha lipite hivi hivi
 
Ataachaje kuja Arusha kwa mfano...

Karibu Arusha ujionee maajabu ya African
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…