Rorya: Madiwani wadaiwa kupanga kumteka M/kiti wa Halmashauri wakigombea eneo la kujenga Kituo cha Afya. RC Hapi atishia kuvunja Baraza la Madiwani

Rorya: Madiwani wadaiwa kupanga kumteka M/kiti wa Halmashauri wakigombea eneo la kujenga Kituo cha Afya. RC Hapi atishia kuvunja Baraza la Madiwani

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Moja kwa moja kwenye mada.

Katika Hali ya kushangaza, Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara walikutana usiku kupanga njama za kumteka Mwenyeki wa Halmashauri yao.

Kiini cha mgogoro ni kutokana na kutokubaliana sehemu ambapo panatakiwa kujengwa Kituo cha Afya.

Hatua hiyo imepelekwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi kutishia Kulivynja Baraza la Madiwani kwa Kumuomba mh.Rais ikiwa wataendelea kukiuka Taratibu za Sheria.

My Take:

Watu wa Mara licha ya Mh.Rais kuwaasa muache migogoro lakini Bado ndio kwanza mnalianzisha jipya.

Hivi kweli ugomvi wa kituo cha Afya ndio unawafikisha huko? Acheni hizo mnazingua.

Serikali pelekeni pesa zingine huko wapate vituo kadhaa kabla hawajafyekana mapanga 👇

======= =======

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi amesema atamuomba Rais Samia Suluhu Hassan avunje Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, ikiwa viongozi haowatashindwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwa Baraza hilo.

Akizungumza katika Kikao cha Baraza la Madiwani hao leo Mei 17, Hapi amekemea tabia ya baadhi ya madiwani hao kukumbatia migogoro inayokwamisha miradi ya maendeleo. RC Hapi amedai kuwa madiwani Saba wanatekeleza mikakati inayolenga kusababisha halmashauri hiyo isitawalike.

“Usiku wa kuamkia leo madiwani hao walikutana kwa siri maeneo ya Sirari, wilayani Tarime kukamilisha mpango wa kumteka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Gerald Ong'ong'a ili kukwamisha kikao hicho ambacho moja ya ajenda ilikuwa kuamua eneo la kujengwa Kituo cha Afya cha Kata hiyo”

Ilifahamika kuwa ajenda hiyo imechochea mgawanyiko wa madiwani hao, baadhi wakitaka kituo kijengwe katika Kijiji cha Makongro, wengine wakitaka kijengwe Kijiji cha Oriyo vyote vya Kata ya Rabour ambayo Diwani wake ni Ong'ong'a.

Source: HabariLeo
 
Back
Top Bottom