Rorya: Mme amkata Mkewe titi na mkono kisa wivu wa kimapenzi

Rorya: Mme amkata Mkewe titi na mkono kisa wivu wa kimapenzi

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Mkazi wa kijji cha Isango wilaya ya Rorya, Maria Marwa (36) amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mara baada ya kudaiwa kukatwa mkono na titi na mumewe.

Mwanamke huyo alipata majeraha hayo baada ya kuibuka ugomvi baina yake na mume wake huku chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi ambapo mbali na kukatika mkono na titi, amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake.

Akizungumza na Mwananchi akiwa hospitalini leo

Jumanne, Septemba 20, 2022, Maria amesema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 7 saa 3 usiku ambapo mumewe alitaka namba ya mtu aliyempigia simu.

Akimzungumzia mgonjwa huyo, Daktari wa hospitali hiyo, Nurdin Nuru amesema kuwa walilazimika kumkata mkono mwanamke huvo baada va kufika hospitalini hapo akiwa tayari mkono umeharibika.

"Tulimpokea hapa Septemba 8 mkono ukiwa tavari umeharibika huku titi la kushoto likiwa limening'ing'inia na mkono uliharibika" amesema

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Rorya, Geofrey Sarakikya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kuwa jeshi la polisi linaendelea kumsaka mwanaume huyo aliyetoroka baada ya kufanya tukio hilo.

Mwananchi
 
Akizungumza na Mwananchi akiwa hospitalini leo

Jumanne, Septemba 20, 2022, Maria amesema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 7 saa 3 usiku ambapo mumewe alitaka namba ya mtu aliyempigia simu.
Yeye alipotakiwa kutoa namba ya simu ya aliyempigia alifanya nini?kama alikataa then kuna tatizo mahali na yeye mwenyewe analijua wamuulize vizuri.
 
Na yeye akatwe kende zake chap kwa haraka.
Msengerema huyo Mutu yeye ndio aliyetoa bikra.??
 
Duh,wanaume wa kanda ya ziwa
Wakiumizwa kwenye mambo ya mapenzi,wana react vibaya sana

Ova
 
Huu ukatili utaisha lini jamani? Afrika kuna maajabu aise, kwa wenzetu huwezi kukuta ukatili wa namna hiyo.
 
Hivi Visa vya wivu vimezidi Sasa.
 
Back
Top Bottom