Rosa Parks alivyosabibisha Montgomery Bus Boycott nchini Marekani

Rosa Parks alivyosabibisha Montgomery Bus Boycott nchini Marekani

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2022
Posts
276
Reaction score
460
Mnamo mwaka 1955 Nchini Marekani kuliwahi kushuhudiwa mgomo mkubwa wa watu weusi wakazi wa mji wa Montgomery wakisusia kutumia mabasi ya umma waendapo na warudipo nyumbani kutoka kazini kwa sababu ya ubaguzi katika huduma za mabasi hayo dhidi ya watu weusi.

Mgomo huo ulianza mnamo mwezi Novemba mosi 1955 na kudumu kwa Miezi kadhaa, ulianzishwa chama cha Maendeleo ya watu weusi nchini humo National Association for Advancement of Coloured People NAACP kikiongozwa na baadhi ya wanaharakati weusi Kama Martin Luther, Malcolm X bila kumsahau Rosa Parks aliekua mwanamke mwanaharakati jasiri.

Mgomo huo uliitishwa ili kushinikiza serikali kuchukua hatua dhidi ya wale wanaoleta ubaguzi katika maeneo ya huduma za umma ikiwemo mabasi ya mji na Migahawa.

Rosa Parks alizaliwa mnamo 1913 Nchini Marekani katika familia ya watu weusi na alipata kukulia Katika mateso ya ubaguzi hivyo alichoshwa na hali hiyo akajiingiza katika harakati za kudai usawa.

Rosa Parks anasimulia jinsi alivyopata kubaguliwa "ilikua jioni ya tarehe moja mwezi Novemba 1955 nilikuwa narejea nyumbani kutoka kazini, nilienda Moja kwa moja katika eneo la Court Square ili kupanda Basi linalopita katika Barabara ya Cleveland inayo elekea Nyumbani.

Pindi nilipo ingia kwenye Basi sikuangalia Nani alikua anaendesha Hadi nilipo tulia ndipo niligundua Ni yule aliye wahi kunishusha katika Basi miaka 11 nyuma lakini sikua na la kufanya kwa Sababu nilikua tayari nimesha kulipa nauli na Kama ningemuona mapema nisinge panda lile basi.

Alikua bado ni mrefu,mnene na anelekea kwenye rangi nyekundu kwenye ngozi yake nilijiuliza je miaka yote alikua anafanya kazi kwenye lile Basi maana Kuna kipindi mamlaka zilikua zinabadilisha sana madereva kwenye magari ya umma.

Nilipo tuliza macho nikaona siti ya wazi Upande wa katikati nikaenda Kukaa sikupata kujiuliza kwanini katikati palikua na nafasi za wazi ingawaje Kuna watu wamesimama nyuma? sikufikiria yote hayo Ila nikadhani kua huenda waliniona wakati naingia ndio maana wakaacha siti wazi ili nipate Kukaa.

Kulikua na mwanaume aliekaa pembeni yangu Upande wa dirishani na wanawake wanawake wawili walikaa upande wa Pili usawa ule.

Gari likaanza Safari na kituo kilicho fuata ilikua ni Empire Theater lilipo simama wazungu wawili waliingia ndani wakakaa na kujaza siti nyeupe na mmoja akabaki amesimama dereva akageuka na kumuona aliye simama na akageuka tena Upande wetu akisema hebu wapisheni wakae Upande wa katikati lakini Hakuna aliye simama Kati yetu kuwapisha tukabaki tumekaa Kama tulivyo kua, tulikua wanne katika ujumla wetu.

Akageuka Tena na kusema Ni vema mkafanya uamzi mapema mkanganyuka na kuachia hizo siti, mwanaume aliekaa mbele yangu Upande wa dirishani akanyenyuka na nikamkwepa ili kumpa Nafasi apite.

Nilipo tazama upande wa pili niliwaona wale wanawake wawili nao wamesimama nami nikasogea upande wa dirishani alipokua amekaa yule mwanaume nikakaa sikuangalia wale waliosimama walienda wapi bali nikajisemea Moyoni kadri tunavyo wapisha ndivyo wanavyo tufanyia vibaya.
Nilifikiria miaka ya nyuma ambapo nilikaa Usiku mzima pasipo kulala huku baba yangu Akiwa ameshikilia bunduki yake mkononi kujihami.

Baadhi ya watu walisema huenda sijasimama kuwapisha kwa Sababu ya uchovu lakini kwangu hiyo haikua sababu nilikua sijachoka Kimwili au kimajukumu ya kazi nilyoifanya siku nzima Wala sikua mzee ingawaje baadhi yao waliniona Kama mzee lakini nilikua na miaka 42 tu kiuhalisia.

Dereva alipogeuka kwa mara nyingine akaniona bado nimekaa akaniuliza unaelekea kusimama? nikamkibu hapana! akasema sawa nawatarifu Polisi utakamatwa, nikamjibu vyovyote utakavyo amua Wewe.
haya ndio maneno pekee tuliyo jibizana Mimi na yeye. Sikujua hata jina lake ambalo alikua akiitwa James Blake mpaka pele tuliposimama wote mahakamani.

Alipotoka nje ya gari alisubiri kwa muda ili Polisi wake nikijaribu kutulia pasipo kifikiria nini kitatokea nilijua kua lolote linaweza kutokea sikuweza kufikiria Sana Wala kuwaza kutoka nje ya Basi"

Rosa Parks akakamatwa na kufikishwa kortini ikalelekea wimbi zito la kudai usawa nchini humo ambao watu weusi waligomea mabasi ya umma walitembea kwa mguu, baiskeli waendapo kazini na warejeapo Nyumbani mgomo huo ukaitwa "Montgomery Bus Boycott".

Mgomo huu ulipelekea kukua kwa harakati za watu weusi l "Civil Right Movement ambapo hadi Kufikia mwaka 1961 Rais wa Taifa hilo kipindi hicho John F Kennedy akapendekeza mabadiliko ya kikatiba yatakayo wapa watu weusi haki sawa katika kila kitu nchini humo.

Peter Mwaihola
1671686756335.jpg
 
hata hapa Bongo bado Ubaguzi upo japo si wa rangi bali wa ukabila, kwa baadhi ya maeneo
 
hata hapa Bongo bado Ubaguzi upo japo si wa rangi bali wa ukabila, kwa baadhi ya maeneo
Bongo hata wa rangi upo yani ni nchini kwako na unabaguliwa na hakuna kitu utafanya chuga kuna kimtaa iko wanakiita PPF huko wa nakaa madoni( hasa wahindi na wazungu, weusi wapo ila wachache ).

Picha linaanza wamefunga njia zote za kuingilia hilo eneo wameweka mageti na KK kapuku ukitaka kupita apo ujieleze unaelekea wapi na kufanya nini then usign akija kidume anadrive anafunguliwa tu (tuchukulie hiyo ni sababu ya kiusalama kwasababu wanaishi wenyenazo (japo siamini hili kwasababu karibu kila nyumba ndani ya ilo eneo ina geti+electrical fence +kk +mbwa mkali ) kamahaitoshi walinzi wa kuingilia njia zote ndani ya ilo eneo wameweka na walinzi na geti lingine kuingilia baadhi ya barabara ndogondogo ndani.

Yote tisa kumi ukipenya humo ndani kama sio mfanya kazi let say umeenda kiserikali (kama mimi nilivyo enda) kauli zao na vitendo vya kibaguzi dhidi yako vinatia kinyaa
 
Kipindi flani nilihamia shule flani huko mikoa ya Pwani. Mi Wala sikuwa mzaliwa wa kabila la hapo. Basi wale watu ( wengine wenzangu wanafunzi) walikuwa wakinibagua waziwazi kwa utofauti wa kabila nililotoka. Walikuwa na jina la kidhalilishaji la kuniita kwa lugha yao. Wageni wote huwaita hivyo kasoro wamasai tu. Wamasai wao huitwa gendamwazi .
Nilijuta kuwa pale.
 
Kipindi flani nilihamia shule flani huko mikoa ya Pwani. Mi Wala sikuwa mzaliwa wa kabila la hapo. Basi wale watu ( wengine wenzangu wanafunzi) walikuwa wakinibagua waziwazi kwa utofauti wa kabila nililotoka. Walikuwa na jina la kidhalilishaji la kuniita kwa lugha yao. Wageni wote huwaita hivyo kasoro wamasai tu. Wamasai wao huitwa gendamwazi .
Nilijuta kuwa pale.
Kuwa muwazi tuwajue[emoji849]
 
Back
Top Bottom