Rosa Ree amshtaki Harmonize kwa wizi wa mdundo wa wimbo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
MSANII wa muziki Bongo, Rosa Ree amefunguka kuwa kesi na Harmonize kwa sasa ipo kwenye mikono ya sheria kuangaliwa ni jinsi gani haki inaweza kutumika kwasababu muziki ni biashara.

Rosa Ree amesema wimbo wake Kanyor Aleng aliwahi kumsikilizisha Harmonize awali lakini akashangaa kuja kusikia kitu kinachofanana na hicho.

Ikumbukwe Julai 26, mwaka huu wimbo wa Harmonize unaokwenda kwa jina la Amen uliondolewa kwenye mtandao wa YouTube, hii ni kutokana na wimbo huo kufanana mdundo na wimbo wa Rosa Ree uitwao Kanyor Aleng.

Harmonize alitoa wimbo huo (Amen) kufuatia kifo cha Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, wimbo huo umeelezea mazuri kibao yaliyofanywa na Mzee Mkapa enzi za uhai wake na jinsi Dunia ilivyobaki na simanzi kwa kuondoka kwake.

Ikumbukwe hili ni mara ya pili kutokea kwa Harmonize, mwanzo ni kwenye wimbo wa Uno ambao ilisemekana una vionjo vya mdundo wa Prodyuza kutokea Kenya, Magix Enga.
 
Sio kamsikilizisha Haromize bali alishatoa hiyo nyimbo na Harmonize akaichukua beat yake na kumuimbia marehemu Mkapa bila ridhaa yake.
 
Mbona wengine wanatuhumiwa kuiba ila hawatolewi nyimbo zao, kumbe huwa ni wivu na chuki tu kwa Diamond maana huwa anafuata taratibu kwanza, Konde anakurupuka.
 
Sio mara ya pili aliiba na wimbo wa Papa Wemba na ukafutwa kwenye album yake, kiufupi dogo anakurupuka sana katika kazi zake
 
Hapo hajaiba kachukua kaifanya isikike mwenye anataka mali yake aende akamdai walipane baasi.
 
Harmo konde kiufupi ubunifu wake ni mdogo sana ata ukiangalia nyimbo walizoimba na domo alikuwa anaiga adi pozi za kushika maiki ukiskiza nyimbo nyiiingi ni vingi amekopi labda zingine alifuata taratibu zingine ndo kama ivo kukurupuka anaumbuka
 
Mmakonde alichokosea ni kua chini ya mtu ambae maisha yamemuendea kombo,yani kashindwa kumundu biashara zake ndio aweze kummudu msanii.
Jembe ni hewa yupoyupo tu hana mipango,ukumbi wake umemshinda ndio aweze kumtoa konde
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…