IAMswaggstatic
Member
- Apr 23, 2012
- 76
- 71
:: pichani ni Malkia wa mwisho wa Rwanda Rosalie Gicanda (aliyeolewa na mfalme Mutara III Rudahigwa mwaka 1942)....
mfalme Mutara III Rudahigwa alikuwa mfalme wa Rwanda kati ya mwaka 1931-1959, alikuwa mfalme wa kwanza wa Rwanda kubatizwa na ndiye aliyeruhusu ukatoliki kuingia nchini Rwanda., alibatizwa mwaka 1943.
Alizaliwa machi 1911 katika jimbo la Nyanza, alifariki 25 July 1959 akiwa na miaka 48 huko Bujumbura, Burundi. Alikuwa mfalme anayetoka katika ukoo maarufu kwa jina la 'Abanyiginya' katika Kabila la Watutsi.
.., 'Abanyiginya' wa falme ya kinyarwanda kutoka ukoo wa kitutsi, ni miongoni mwa falme ambazo zilipata kukua na kuenea maeneo mengi sana haswaa upande wa maziwa makuu, kwa nchi kama Tanzania ulifika na kumea mizizi..., na miongoni mwa makabila yaliyopatwa kutawaliwa na ufalme wa Kitusi ni kabila la Waha na Wafipa...,
kuna mambo kadhaa yanafanana katika makabila hayo haswaa masuala ya matambiko, vyakula na muingiliano wa maneno katika lugha yake!
Baba yake na Mutara III Rudahigwa, alikuwa mfalme, alikuwa akiitwa mfalme (King) Yuhi V Musinga, na mama yake aliitwa malkia (Queen) Kankazi
Kabla ya kumuoa Rosalie Gicanda mwaka 1942, alikuwa na mke wake wa awali alikuwa akiitwa, Nyiramakomali (alimuoa mwaka 1933 wakaachana mwaka 1941)
Baada ya kubatizwa alijulikana kwa jina la Charles Léon Pierre na kuna nyakati alikuwa akiitwa jina la Charles Mutara III Rudahigwa.
Wabelgiji walianza kumtumia Mutara kama sehemu ya kuingiza ukatoliki katika ardhi ya Rwanda, baba yake (Mfalme Musinga) aligoma kubatizwa na kubadili dini kuwa mkatoliki, wabelgiji wakamuona muasi.., mwaka 1929 ndiyo walianza kazi hiyo.
Baada ya kuwa mfalme mwaka 1931, Mfalme Mutara III Rudahigwa alirihusu ardhi yote ambayo alikuwa akiitawala na maeneo yake kuwa rasmi kwa ajili ya dini ya ukatoliki, mwaka 1946.
Utawala wa mfalme Mutara III Rudahigwa ulishuhudia njaa kubwa kuwahi kuikumba ardhi ya Rwanda kati ya mwaka 1941-1945, watu 200,000 kati ya wati takribani milioni 2 walifariki kwa kukumbwa na baa la njaa!
Mfalme Mutara III Rudahigwa baada ya kufariki nchini Burundi kwa kinachodaiwa kuwa ni matatizo ya ndani ya ubongo (ingawa kuna taarifa kwamba aliuwawa na wabelgiji) nafasi yake ilichukuliwa na mdogo wake (asiyetoka katika tumbo la mama yake) alikuwa akiitwa Jean-Baptiste Ndahindurwa, na alipewa jina la kifalme kama Mfalme Kigeli V..
Baada ya kifo cha mfalme Mutara III Rudahigwa, mke wake Rosalie Gicanda aliendelea kubaki nchini Rwanda, na alikutwa na mauti mwaka 1994 katika mauaji ya kimbari (Rwanda Genocide) kwa ruhusa ya Idelphonse Nizeyimana (ambaye baadae alikamatwa na kuhukumiwa kwenda jela maisha yake yote na mahakama ya Umoja wa mataifa ya uhalifu wa kivita, UN war crimes court, 19 June 2012,)
Idelphonse Nizeyimana, alihukumiwa pia kwa kutoa ruhusa ya kumuua Rosalie Gicanda katika. Mwanzo wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 katika eneo la Butare, pia Alihukumiwa kwa kuhusika moja kwa moja katika vita hiyo.., alikuwa mzaliwa wa Gisenyi, eneo moja na Rais wa wakati huo Juvénal Habyarimana.
Luteni. Pierre Bizimana, kwa ruhusa ya kapteni Idelphonce Nizeyimana walikwenda na kuzunguka nyumba aliyokuwa akiishi malkia huyo wa zamani wa falme ya Rwanda, walimteka pamoja na watu wengine waliokuwemo ndani na kuwapeleka katika msikiti wa taifa na kuwapiga risasi..
Msichana mdogo pekee ndiye aliyebaki na kutoa simulizi hizo, siku mbili baadae, mama yake na malkia huyo pia alifariki katika machafuko hayo.
Kwa maombi ya Padri, meya wa Butare Kanyabashi alikubali kuchukua mwili wa malkia huyo na kukubali kuuzika pembezoni mwa nyumba yake, alikuwa na umri wa miaka 80 wakati huo!
Idelphonce Nizeyimana alikuwa na cheo cha Kapteni, mwaka 1994 alikuwa akihudumu katika jeshi la Rwanda maarufu kama Rwandan Armed Forces (RAF), alikuwa wa pili kwa maamuzi (second-in-command) baada ya Tharcisse Muvunyi, wa École des sous-officiers (ESO)
Martin Maranja Masese
Mwananchi wa kawaida
(courtesy of historia ya Afrika)