Rose Muhando: Kutoka ombaomba hadi nyota wa muziki wa Injili kimataifa

Rose Muhando: Kutoka ombaomba hadi nyota wa muziki wa Injili kimataifa

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Maisha uliyoishi zamani hayawezi kukukwamisha kufikia malengo uliyojiwekea. Hakuna mtu ambaye alifikiri leo hii Rose Muhando angeweza kuwa mwanamuziki mkubwa wa nyimbo za Injili anayelipwa fedha nyingi kutokana na muziki wake, hasa kwa wale waliomjua tangu utoto wake.

Lakini mwanamuziki huyo aliyesaini mkataba wa miaka mitano na Kampuni ya Sony Music Africa ya Afrika Kusini alioanza kuutumikia mwaka huu 2014, anasema kuwa maisha yake yalianzia katika hali duni kwani alikuwa akiombaomba baada ya kufukuzwa katika familia yake huko Dumila mkoani Morogoro kwa kosa la kubadili dini.

“Nilikuwa mwimbaji mzuri sana wa kaswida, nilihudhuria kila siku madrasa nikiwa Dumila. Baadaye maisha yangu yalikuwa magumu sana, chanzo cha haya yote ilikuwa ni ugonjwa uliosababisha afya yangu kudhoofu. Kwa wakati huo nilipimwa kila ugonjwa sikukutwa na tatizo, ndipo siku nilipoamua kwenda katika maombi,” anasema Rose Muhando ambaye sasa anatamba na wimbo Wololo alioutoa chini ya Sony Music Africa.

Anasimulia kuwa baada ya maombi hayo, alipona na hapo ndipo alipoamua rasmi kubadili dini akiwa na umri wa miaka 12.

“Nilipobadili dini, wazazi wangu walichukizwa na uamuzi wangu, waliona ni busara kunifukuza nyumbani, kumbe walizidi kunihatarishia maisha yangu. Niliendelea kutangatanga na baadaye nilipata waume, ambao walinizalisha watoto watatu,” anasimulia na kuongeza:

“Nikiwa na mtoto wa miezi sita niliwahi kufukuzwa na mchungaji mmoja jijini Arusha kwa kuwa tu nilikwenda kumwomba msaada wa fedha kidogo za kurekodi studio. Kitu hicho kiliniuma sana na sitakisahau katika maisha yangu. Kila nikikaa hukumbuka na kuumia sana.”

Anasema kwamba alifika Arusha kwa ajili ya kurekodi wimbo wake wa kwanza, ambapo kutokana na kutokuwa na fedha aliona ni busara kumwomba msaada mchungaji huyo, lakini ilishindikana.

“Alinifukuza nikiwa na mtoto mchanga aliyekuwa na mgonjwa wa pumu, niliumia sana na hapo ndipo nilipomwambia Mungu nikasema yeye anajua ameniandalia nini kwenye maisha yangu,” anaeleza Rose.

Anasimulia kuwa alianza safari ya kurejea nyumbani, lakini kwa bahati nzuri njiani alikutana na watu wenye asili ya Somalia na kujitambulisha kwao kuwa aliwahi kuwa muumini wa dini ya Kiislamu, nao walimsaidia na kumsafirisha hadi mkoani Morogoro.

Baada ya kufika Morogoro aliendelea na maisha na baadaye kujiunga na kwaya moja mjini Dodoma, wakati huo alikuwa tayari na watoto watatu akiwa pia ameshaokoka.

“Nilianza muziki katika kwaya iliyopo Dodoma, baadaye nikawa mwalimu wa kwaya hiyo ya Dodoma St. Mary’s katika Kanisa la Kianglikana la Chimuli. Niliendelea hivyo mpaka nilipoamua kuanza kutunga nyimbo zangu mwenyewe kwa msaada wa mfuko wa kwaya yetu,” anabainisha na kuongeza:

“Januari mwaka 2005, ndipo nilipoanza kuona uwepo wa Mungu, nilipokea tuzo mbalimbali ikiwamo ya MtunziBora wa nyimbo za Injili, Mwimbaji Bora na Albamu Bora ya Mwaka, zilizotolewa na Tanzania Gospel Music Awards 2004.”
 
Na kumiliki mume wa mtu hadi kudhulumu ndoa hiyo.
 
Ukitoka huko kwa wale ukaja huku kwetu sisi,kwa kubadiri dini.Na ukawa public figure...wale wanamaind kweli kweli siajabu walijalibu kukutumia ndugu zao "waarabu" ikashindikana.Na bado watakusakama.usimuache yesu kristo wa nazareth.
 
Amwimbie sasa Mungu aache skendo... Tunataka wanaomwimbia kwa roho na kweli sio kupiga hela tu, hela piga ila toa fundisho..
 
Na kumiliki mume wa mtu hadi kudhulumu ndoa hiyo.
Ni rahisi kutuhumu mwenzio ukasahau kwamba nawe una udhaifu kadha. Lakini anayejua kuhukumu kwa haki ni Mungu peke yake.

Binadamu asinunue kesi za wenzie kutoka kwa Mungu kwani Mungu humrehemu anayependa kumrehemu pasipo kuangalia udhaifu wa ntu huyo. Kama Mungu angekuwa na fikra kama ya binadamu hakuna ntu angepona hukumu kali ya Mungu.

Mungu ni mpole na mwenye huruma sana. Anachojali zaidi ni kwa ntu kutambua kwamba ni nkosaji na kwamba hawezi kujiokoa mwenyewe kutoka hachira ya Mungu. Vinginevyo zile Torati za Musa zingetosha kuwapeleka watu mbinguni na kuchngekuwa na haja ya kuja Yechu Krichtu. Hakuja kuimwaga bure damu yake kwani Mungu anamwona kila binadmu kuwa ni nchafu na moyoni ameoza pia na kunuka.

KIRI UCHAMEHEWE, mwache Rochi Nhando achane mbuga kwenda Mbinguni na awaelekeze wengine kwenda kumwona Mungu uchinkatiche tamaa. Uchijekuwa unataka kugombana a Mungu aliyentuma kuifanya kazi hiyo adhimu.

Tunaambiwa tutiane moyo na wala chio kukatichana tamaa.
 
kazana dada rose mhando mungu atakufikisha mbali kwan nyimbo zako c mchezoo kuanzia nibebe,utamu wa yesu na huu unaovuma saizi wema wako aisee nazipenda sana nyimbo hizo.
 
Ni rahisi kutuhumu mwenzio ukasahau kwamba nawe una udhaifu kadha. Lakini anayejua kuhukumu kwa haki ni Mungu peke yake. Binadamu asinunue kesi za wenzie kutoka kwa Mungu kwani Mungu humrehemu anayependa kumrehemu pasipo kuangalia udhaifu wa ntu huyo. Kama Mungu angekuwa na fikra kama ya binadamu hakuna ntu angepona hukumu kali ya Mungu. Mungu ni mpole na mwenye huruma sana. Anachojali zaidi ni kwa ntu kutambua kwamba ni nkosaji na kwamba hawezi kujiokoa mwenyewe kutoka hachira ya Mungu. Vinginevyo zile Torati za Musa zingetosha kuwapeleka watu mbinguni na kuchngekuwa na haja ya kuja Yechu Krichtu. Hakuja kuimwaga bure damu yake kwani Mungu anamwona kila binadmu kuwa ni nchafu na moyoni ameoza pia na kunuka. KIRI UCHAMEHEWE, mwache Rochi Nhando achane mbuga kwenda Mbinguni na awaelekeze wengine kwenda kumwona Mungu uchinkatiche tamaa. Uchijekuwa unataka kugombana a Mungu aliyentuma kuifanya kazi hiyo adhimu. Tunaambiwa tutiane moyo na wala chio kukatichana tamaa.

Well said
 
Kuna ule wimbo aliimba moja ya part anasema :walionizalisha wamenikimbia"

Mzee wa Upako akasema waliomzalisha au aliozaa nao kwani aliforciwa si alinnihii kwa hiyari yake
 
Kuna ule wimbo aliimba moja ya part anasema :walionizalisha wamenikimbia"

Mzee wa Upako akasema waliomzalisha au aliozaa nao kwani aliforciwa si alinnihii kwa hiyari yake

Hahahahaaaa...mmh!..na wewe umo. Haya endelea kunifunga kamba.
 
Back
Top Bottom