Rose Ndauka Ajifungua mtoto wa Kike..!!

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka amejifungua mtoto wa kike kwa njia ya upasuaji mwanzoni mwa wiki hii katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar.

Akizungumza na Ijumaa, Rose Ndauka alisema anamshukuru sana Mungu kwa kumjaalia kujifungua salama huku mwanaye huyo akiwa na afya njema.

“Ki ukweli kabisa namshukuru sana Mungu kwa zawadi ya mtoto kwa maana nimejifungua salama kabisa,mimi na mtoto tuko vizuri na nafurahi sana kuingia kwenye ulimwengu mwingine kabisa wa cheo kipya cha kuitwa mama,” alisema Rose.

Akasema hivi sasa ataweka shughuli zote pembeni kwa ajili ya kuanza kumlea mtoto mpaka atakapofisha umri ambao anastahili kuachwa ndipo ataendelea na shughuli zake za sanaa.
 
Hongera dada mungu akukuzie.
 
Hongera yake.
Mungu amkuzie.
 
ndo nani huyo?
alikua bodyguard wa kanal muamar ghadafi,baada ya ghadafi kufa akaja tanzania na kufanya kazi pale makao makuu ya chadema.kwa sasa ni msemaji wa timu ya mbeya city inayoshrki ligi ya madagascar.ushamjua?
 
Umenichanganya kweli mkuu, bora niishie hapo alikua bodyguard wa gadafi...well ndo kapata mtoto lini?
 
..Nasikia wengi ukisikia kajifungua kwa operation....jua anatumia sana XPRESS URSELF...
 
..Nasikia wengi ukisikia kajifungua kwa operation....jua anatumia sana XPRESS URSELF...

Zipo sababu nyingi sio hyo tu panua kufikiri kwko ww!!!
mwengine njia ndogo, wengine mtoto anakuwa amekaa vibaya tumboni, wengine hawataki kupitia uchungu n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…