Rose Ndauka na Charlz Baba "BIFU" zito

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Ni dhahiri kuwa sasa , staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka na Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ' Chaz Baba ' wapo kwenye bifu zito.

Habari kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa , chanzo cha bifu hilo ni fedha , ambapo Rose alikodisha gari la Chaz Baba kwa ajili ya matumizi yake lakini akalirudisha likiwa limeharibika na kumuomba Chaz alitengeneze kisha angemlipa fedha zake, lakini hakufanya hivyo .

Staa wa filamu za Kibongo , Rose Ndauka "Alikodi gari kwa Chaz , lakini aliporudisha lilikuwa bovu, akamuomba Chaz alitengeze angemlipa , baada ya hapo akaingia mitini . Chaz alikasirika sana, maana hata Rose alipopigiwa simu alikuwa hapokei .

"Imefikia hatua Chaz ametoa kiapo kibaya , amesema hata akifa, maiti yake isizikwe mpaka Rose alipe fedha zake kwanza , " kilitiririka chanzo hicho. Akizungumzia ishu hiyo , Chaz alisema , kitu alichokifanya Rose si kizuri na kamwe hawezi kumsamehe mpaka amlipe fedha zake .

Huyu hapa anafafanua zaidi : "Unajua Rose alikuja kwangu na kukodi gari yangu aina ya Toyota Noah , akarudisha likiwa halitamaniki kabisa , nilipomwuliza akasema walipata ajali , nikamtaka akalitengeneze, akasema hana pesa kwa hiyo nitengeneze atanilipa .

Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba ' "Tangu siku hiyo sijaona simu yake wala meseji, hata nikimpigia hapokei . Nimeingia hasara ya kwenda kutengeneza kwa shilingi laki tano, pesa yangu inaniuma , nataka anilipe .

"Hata kama nikifa leo , maiti yangu isizikwe mpaka Rose alipe haki yangu kwanza . Akitangulia yeye utaratibu utakuwa hivyo sitokubali azikwe hadi ndugu zake wanilipe fedha zangu, " alisema Chaz Baba .

Baada ya kupata habari hiyo Risasi Jumamosi lilimhoji Rose kulikoni ameshindwa kulipa deni la watu hadi mdai anatoa kiapo kibaya kama kile,akaruka vikali.

"Ni kweli kabisa mimi nilikodi gari ya Chaz nikawa natembelea na ilivyokuja kuharibika nililitengeneza mimi na kwenda kumkabidhi lakini hakuridhika na namna lilivyotengenezwa ndiyo maana anasema ananidai lakini mimi sijui hilo deni , " alisema Rose .
 
Du kweli bongo noma le supa sitaa anatembelea noah?
 
Anataka kulipwa kingine huyo sio gari!..na demu inaonekana kagoma kumlipa hicho anachotaka!..
 
Inakuwaje unaazima gari ya mtu? Piga bajaji tu
 
Hawana mpya hawa walipo peana mbona hawakutangzana? wazushi tuu na huyo jamaa nae laki 5 anatoa maneno kama haya duhh......
 
Ina maana huyu rose hadi leo hujafanikiwa kupata japo ka mkweche ka kwake mwenyewe?
 
Wabongo hua tunatafutana ubayaa

Yaani huyu rose ana bahat ajishauagi tu kama mama ubaya yan ningempa makavu live, sasa na yeye jaman anashindwa kumwambia bwana wake huyo malick bandawe amnumulie hata vits jaman? Yani kamzalisha bas tena hana thaman, rose na yeye mjinga uzur wote uo unakosa gar mjini apa? Yan una bahat tu hujishauag apa mjini mengine nakuhifadh kwa leo
 
Ina maana huyu rose hadi leo hujafanikiwa kupata japo ka mkweche ka kwake mwenyewe?

Bongo movie hailipi na huwez kununua gari et kwa ajil ya kuigiza, labda ma producer mkuu , hao wengine wot umalaya na ushoga ndo unaowaweka mjini, bora rose anaishi maisha yake japokuwa na yy ana ulimbuken mtu kama gar huna c unakituliza kwan bajaj wamewekewa wakina nan
 
Jamani naomba kuuliza hv Bodaboda wamewekewa kina nani?kwa nini uishi fake life.Yaani asilimia kubwa ya wasanii twenty4seven wapo location wanaact mpk real life yaani huwa nawaonea huruma sana.
 
Kuna mengine zaidi ya hayo..wasitudanganye...
 
Hawa bongomuvii ni wasanii sana yaan wanapenda kucheza scrpt mpaka kwenye normal life!!garii unaazima kweeeli??si upande bajajii??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…