Tatizo la wamiliki wa vyombo vya habari hususani vya kielekroniki - Radio na Runinga wanasahau kwamba, masafa ni rasilimali ya umma na kwamba licha ya kuwa wao wamewekeza mitaji, lakini masafa angani ni mali ya wananchi wote na wao wamedhaminiwa kuyatumia ili wananchi wote wafaidike, hii ni pamoja na kufanya kazi kwa maslahi ya umma, kinachotangazwa kama habari, licha ya matakwa mengine ya kitaaluma lakini piwe kiwe na maslahi ya umma, yaani mwananchi kwanza. Niliona hii habari ITV, nilishtuka kama wengine walivyofaynya.
Lakini kingine kinachokwenda sambamba na hili ni la leo asubuhi, kwenye Matangazo ya Asubuhi Njema ya Channel Ten, ambako pia huwa kuna mapitio ya magazeti, Mtangazaji alipokuwa akipitia magazeti ... na kufika kwenye gazeti la Kulikoni na Thisday ... aliruka bila kuzisoma habari kubwa kwenye magazeti haya na ambazo zilikuwa zinaonekana exclusive ....kisa huenda kwa sababu zilikuwa zinamuhusu Manji.
Niliwahi kuona kitu cha aina hii pia kwa enzi zile TVT ambapo habari ambazo zilikuwa zinaonekana mwiba kwa serikali ... zilikuwa zikirukwa.
haya ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma -- yaani masafa ... na hili halina tofauti na ufisadi.