figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Katika hafla iliyoandaliwa na TANZANIA PRIVATE SECTOR FOUNDATION (TPSF), Angelina Ngalula amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa EAST AFRICA BUSINESS COUNCIL (EABC)
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo bilionea Rostam Aziz.
Akiongea wakati wa kutoa pongezi zake, Rostam Aziz alisema kuwa “Nafurahi sana kuona dada yangu Angelina Ngalula anapata nafasi hii ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa EABC, Mwanamke ambaye ni mchapa kazi, mafanikio yake ndio mafanikio yetu, nina furaha kubwa sana na nampongeza sana. Asanteni”.
Nini tutegemee kutoka kwa Angelina? Je, ni kweli Wakenya Wanamuogopa?
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kuopongezwa kwa kuchaguliwa huko, Angelina alisema moja ya kazi yake atakayoifanya kwa kushirikiana na viongozi wengine ni kuhimiza kuwepo kwa mazingira bora ya uwekezaji kwa nchi wanachama ili kuwavutia wawekezaji.
"Hili ni jambo muhimu, tutahakikisha tunakuwa na sauti moja kama baraza kwa kuweka mazingira mazuri ya kibiashara, lakini kuhimiza kuimarisha kwa miundo mbinu ili kuvutua wawekezaji kwenye nchi zetu," alisema Angelina.
Aidha, alisema pia atahimiza kwa wafanyabiashara kulipa kodi stahiki kwa wakati ili kuzisaidia serikali kujenga miundo mbinu kmaa barabara na reli ambazo ndio msingi wa uwekezaji linapokuja suala la miundo mbinu.
"Lakini pia kwa nchi zetu tunachangamoto ya bidhaa zinazozalishwa ndani kutopata soko kubwa ndani ya nchi, changamoto hii inatokana na ubora wa bidhaa kuwa chini na gharama yake kuwa kubwa ukilinganisha na bidhaa kutoka nje, hili tutalifanyia kazi na kuhakikisha bidhaa za ndani zinakuwa na ubora na zinauzwa kwa bei rafiki, lakini pia wafanyabiashara wazitangaze biashara zao kwa sababu Dunia ya sasa lazima uzitangaze biashara zako," alisema Angelina.
Mkurugenzi Mtendaji wa EABC, John Bosco Karista alisema baraza hilo lina imani kubwa na mwenyekiti wao mpya na watampa ushirikiano unaotakiwa ili kufikia malengo.
" Baraza hili lilianzishwa miaka 25 iliyopita na kwa mara ya kwanza tunaoata mwenyekiti mwanamke, hii ni nafasi nzuri kwake kutoa mchango wake katika kufikia malengo ya Baraza," alisema Karista.
Alisema moja ya changamoto ambayo Baraza linakumbana nalo ni uwepo wa janga la Uviko 19, na mgogoro wa vita ya Ukraine ambao kwa sehemu kubwa umeathiri biashara maeneo mengi na hivyo Mwenyekiti wao mpya anaenda kukutana nalo na watampa ushirikiano mkubwa kuhakikisha wanavuka changamoto hizo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Taifa, Godwill Wanga, alimpongeza Angelina kwa kuchaguliwa kwake na kumuomba kwenda kusimamia vyema baraza hilo la Afrika Mashariki.

Juni mwaka huu kwenye mkutano wa EABC ukiofanyika Kigali, Rwanda, nchi wanachama walimchagua Angelina kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo linaloundwa na nchi saba mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.