Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Hicho kiburi kisiposhughulikiwa kitaiponza CCM.Kiburi,.mtanifanya mini
Sisi waswahili husema, baniani mbaya, kiatu chake dawa. Hata kama hukubaliani na uanachama wa Polepole CCM, haya anayoyasema kukuhusu yana athari za moja kwa moja kwa CCM. Watanzania tunahitaji kujua maelezo yako kwenye hili.
Itakumbukwa marehemu mzee Reginald Mengi, alikutaja ww kuwa fisadi kwenye orodha yake ya mafisadi papa. Hili lilikuwa kubwa, lakini likapita.
Kwenye mradi wa hoja na haja ya mabadiliko, kukitaka chama cha mapinduzi kujitenga na watu wenye makandokando, maarufu kujivua gamba, ww ni miongoni wa walioachwa.
Binafsi nataka kukupa benefit of doubt, kuwa malalamiko yako kuwa unachofanyiwa ni siasa ya maji taka kama ulivyoziita ww mwenyewe ulipotoka kujitetea. Lakini kwenye haya, na CCM inachafuka! Kama kweli unaipenda CCM, na hauna hatia, jitokeze, ujitetee, ujisafishe na kukisafisha chama, kisiathirike kuelekea uchaguzi mkuu.
View: https://vm.tiktok.com/ZMAFsg3Dw/
Mbona pesa zake za kuchangia chama mnazipokea.Hicho kiburi kisiposhughulikiwa kitaiponza CCM.
Uchaguzi wa 2010 na 2015, makada wa CCM tulipata shida sana. Ilikuwa ukionekana tu na sare za chama unazomewa mitaani! Wapo wana CCM walipigwa na wanachi wenye hasira; sababu kubwa tuhuma za ufisadi!
Ukimya wa wakubwa, unawaumiza wadogo huku chini. Haya maswali, asipoyajibu Rostam, watayajibu wana CCM watakaopota kuomba kura kwa wananchi.
Kuchangia chama ndio license ya ufisadi?Mbona pesa zake za kuchangia chama mnazipokea.
Zile namba tatu yaani Harbinder, Rostam, na yule wa GSM ni namba hatari sana kwa Rasilimali za Watanganyika.
Yes.Kuchangia chama ndio license ya ufisadi?
Sisi waswahili husema, baniani mbaya, kiatu chake dawa. Hata kama hukubaliani na uanachama wa Polepole CCM, haya anayoyasema kukuhusu yana athari za moja kwa moja kwa CCM. Watanzania tunahitaji kujua maelezo yako kwenye hili.
Itakumbukwa marehemu mzee Reginald Mengi, alikutaja ww kuwa fisadi kwenye orodha yake ya mafisadi papa. Hili lilikuwa kubwa, lakini likapita.
Kwenye mradi wa hoja na haja ya mabadiliko, kukitaka chama cha mapinduzi kujitenga na watu wenye makandokando, maarufu kujivua gamba, ww ni miongoni wa walioachwa.
Binafsi nataka kukupa benefit of doubt, kuwa malalamiko yako kuwa unachofanyiwa ni siasa ya maji taka kama ulivyoziita ww mwenyewe ulipotoka kujitetea. Lakini kwenye haya, na CCM inachafuka! Kama kweli unaipenda CCM, na hauna hatia, jitokeze, ujitetee, ujisafishe na kukisafisha chama, kisiathirike kuelekea uchaguzi mkuu.
View: https://vm.tiktok.com/ZMAFsg3Dw/
Kabisaaa ili haki itendeke naona inabidi tupate Ibrahim Traore wa Tanzania vinginevyo hii itabaki debe tupu Kwa malori 400 yanayobeba makaa ya mawe usiku kucha mchana kutwa na anaongeza mengine 200 nchi lazima raslimali zake ziishe NJIB HA wewe na pacha wako Mungu anawaona .