Rostam azizi mchimba madini adhimu (almasi-mwadui) Tanzania.

Mtakumbuka ,
Recruitment ya
Wadunguaji
Mtakumbuka
Itakuwa vicheko badala ya
Vilio
Mtakumbuka.

Hivi nani ameimba hii?
 
Pia alikuwa share holder wa shirika la reli la Kenya kupitia kampuni yake ya Milambo na sasa kawauzia Wamisri hizo share zake,huyu jamaa si muchezo Iran connection
 
Acha uwongo,
Rostum hana miradi kibao nje ya Tanzania. Hela yake kaipata kwa kuwafisidi Watanzania. Period.
 
Uwongo mwingine huu. Kama huijui family ya akina Mbowe kaa kimya. Baba yake Freeman hajawahi hata siku moja kuwa mtumishi wa serikali. Yeye ndiye aliyemsaidia Mwalimu Nyerere kueneza TANU katika jimbo la Moshi. Una uhuru wa kumtetea fisadi mwenzako Rostum lakini usiseme uwongo kuhusu familia ya akina Mbowe.
 
Kinachojadiliwa hapa ni upataji wa fedha paipo uhalali... hatukatai utajiriwa haki... ila kama ndo ivyo inabidi tukubali kuwa kwenye sekta ya madini kwa hapa Tanzania kuna mambo ya ajabu mno. Na taifa linapoteza pesa nyingi mno kutokana na mikataba iliyo tata.

So kwa hali hiyo kama RA yupo katika sekta hiyo kama muwekezaji, then unamaanisha yeye ndo chanzo cha mikataba iliyo tata. Na kwa maana hiyo pato linalopotea ni yeye ndo anaiba na wenziwe.

Utajiri wa rasilimali kwa hapa tanzania kwa upande wa madini ni mkubwa mno, ila hakuna faida yeyote iliyopo na kwa misingi hiyo ni kwamba, yeye ndo anachukua haki na fedha zetu... na uthibitishi wa hili ni jinsi anavolindwa na serikali.

Kifupi inauma, na inavyoonyesha ni kuwa hata tenda za uchimbaji wa migodi hii haziendeshwi kwa haki. Sina hakika kwa mtanzania mzawa kwa uwezo wake binafsi akawa na uwezo wa kumiliki MIGODI yoote iliyotakwa kwa haki iliyosawa ya ushindani wa kibiashara.

So jamaa hafai hata kujiita mtanzania... na istoshe kuna wapuuzi wako humu ndani ETI WANAMTETEA KWA HOJA DHAIFU inauma mno.

Jamaa ndio kama mtawala tena ambaye hajachaguliwa na wananchi wa TZ
 
Rostam anatuona wajinga sana,mmegundua kwamba ni fisadi lakini wananchi wanapishana nae hawamfanyi lolote.
 
SSS, wewe kweli mwanamke wa shoka! Umeamua kuwapasulia ukweli au siyo? Sijaelewa kitu though, wewe unakusudia watu wamwache RA endelee kuitafuna nchi au unataka wasiwasahau mafisadi wengine? Ushauri wangu ni kwamba mafisadi waandamwe kwa kuwa katika hali ya kawaida huwa hawaachi ushahidi wa kutosha kuwatia matatani kiasi kikubwa.
Umeisikia Powers of Attorney ya RA ktk Dowans? What else can a normal person do wakati serikali ipo mifukoni mwa RA. Upo sahihi 100% kukumbushia habari za mafisadi wengine pia.
 
Jiulizeni maswali yafuatayo kabla ya baadhio kubwabwaja hapa na nkumtetea Rostam.
  1. Je?mnajua Caspian Agriculture ltd? inafanya shughuli gani na imewekeza kwenye kilimo gani?
  2. Je? unajua fedha za stimulus package kwa ajili ya kilimo zilizopelekwa kanda ya ziwa , unajua Caspian Agricultuire ltd walichukuia asilimia ngapi?na walipewa kwa sababu gani?
  3. Je? unajua kuwa viwanda vya ngozi nchi hii vimekufa , vimeuwawa na kampuni gani? na ngozi zetu huwa zinauzwa wapi?nani alishiriki?
  4. je? unajua kuwa CEO wa Caspian ndio alisaini cheque za Richmond , ambazo walikuwa wanawalipa Harry Sighn & sons ltd,(hawa ni kampuni ya ujenzi ndio walifunga mitambo ya Richmond ubungo) japo zilibounce bank?
  5. Unajua kuwa Ngeleja , aliwekwa nishati na madini ili kufanya jambo ama mambo gani?
  6. unafahamu kuwa wakati kamati ya bunge ya nishati na madioni walipokaa na kusema mitambo ya Dowans iwashwe, walilipwa na wapo waloiopewa bahasha nzito sana? unajua walilipwa na nani?
Nitaendelea baadae kwani hapa nataka wachangiaji mtafakari kwa kina, piaq jueni mpaka nyaraka zinapatikana zina mambo gani?
 

mahlouji,surtees na minja wote hao zuga, kuna mdogowe RA anaitwa Akram ndio CEO wa mradi huo. but their days are numbered. MENE MENE TEKELI NA PERESI.
 

Ngeleja hana ubavu wa kuzima maandamano, labda kama mtayarishaji kachukua kitu kidogo kutoka kwa RA
 
Mimi sijalaaniwa na sina matatizo yoyote.

Kama alivosema Majishindo, Hiyo roho mbaya mliyokuwa nayo baadhi ya wachache Watanzania wenye roho mbaya.Hebu angalia katika wabunge wote Tanzania,nafikiri ukimweka RA katika scale ya 1 to 10 (one being the lowest and 10 the highest) nafikiri RA atapata 10.Waulize wananchi wa jimbo lake.Watakuambia wameridhika naye.

Wana kila kitu na wakiwa na shida wanasaidiwa.Ukimwangalia RA mwenyewe,ni mtu mstaarabu na ana heshima yake. Sasa kama mambo yake ya biashara yamenyoka, Mwenyezi Mungu kampa.Mkisema mu irani sio kweli. Tuwaulize Wanyamwezi na Wasukuma wa Tabora watakueleza RA kazaliwa wapi, kakulia wapi na kasomea wapi?

Acha RA, Babu zake walikuwa watemi. Wamekuwa Tanzania zaidi ya miaka 150. Wewe sikiliza hata lugha akiongea ya Kiswahili au Kisukuma utajua kama ni Mtanzania halisi. Nina uhakika anazungumza Kiswahili kuliko hata wewe? Amekushinda.

Wewe asili yako wapi? Kama si ubaguzi na chuki. Angalia wote wanaoitetea Tanzania, wote mijizi. Tena angalia vizuri, hao wote wataje, kuanzia Dr Slaa, Mwakyembe ,n.k.. Asili yao? Hawana asili wala fasili.

Hebu jaribuni kusema ukweli Mwenye enzi Mungu atawasaidia. Acheni majungu na chuki. Hao kina Mengi na wenzao, walipata wapi utajiri? Tukiendelea na huu mzozo usio kuwa na maana Watanzania hatutafika kokote. Nyie wachache acheni chuki, fata kazi zenu.

ACHENI..........:lol:
 
Hujui unazungumza nini?Hio kampuni ya ngozi haikuwa ya RA.Wala hakuwai kuuza vitabu.1980,RA umri wake ulikuwa chini ya miaka 20 na alikuwa bado anasoma.Kwa hiyo wewe hata hujui RA ametoka wapi.Bora ungenyamaza kuliko kutumia lugha hiyo hapo juu.:washing:
 

Hapo best umechemsha, mzee Mbowe inaonekana hujawahi kumfahamu wala huna hata chembe ya taarifa! Kama unadhani aliajiriwa na serikali ingekuwa vema ukasema post aliyokuwa nayo, RA kweli tajiri lakini source ni wizi wa 'mali ya umma' hilo tu ndio linawakera wa Tanzania - deni la Mbowe Nssf mbona limefafanuliwa siku nyingi inaonekana huna hoja.
 
Lakini Fredmlay unazungumzia nini? Wizi gani? Hio biashara. Kama RA mwizi wa mali ya umma, basi viongozi wote wa serikali wezi. Kwa nini hawatajwi? Mmekalia RA RA mtachoka kama alivyochoka Dr Mwakyembe na Anna Kilango na wengineo.

Nashangaa mtu kama Anna Kilango kuwa mbunge. Mchunguzeni alipokuwa anafanya kazi Gulf Air Daressalaam aliiba tikiti na pesa za mwajiri wake.Ukitaka ushahidi iulize GSA ya Dar. Tukianza kufanya hivi itabidi tuwaandike viongozi wote wa Tanzania. Kwa ushauri wangu kama RA ana makosa basi tumpeleke mahakamani.

Kama hatuwezi, tumuachie huru aendelee na biashara na kazi zake.

UHURU:lol:
 

Ndugu, acha kuzusha mambo yasiyo ya ukweli, fanya utafiti ndo uongee, Mkwere hana hiyo miradi unayoisema! Yote hiyo ina wenyewe na wenyewe wanajulikana na hata walikotoa pesa kunajulikana...mimi ni Mkazi wa maeneo hayo na ninawajua hao watu vizuri sana...unahoji uwezo wa Fantom kuwa na kale ka-mgodi kweli, au ile Zavannah Plains International School, tena unahusisha miradi hii midogo na Mtu mzito kama JK? Haya mengine sasa madharau...Mengine jamani tunazidisha kwa kweli, duh!!! Tumuacheni huyu Mzee afanye kazi tuliyompa sasa, tuache kumzonga. Kila kukicha ni malalamiko tu, tufanyeni kazi sasa...........kama una machungu ya ukweli, karibu Nzega kwenye maandamano kuhamasisha mgodi wa dhahabu Nzega ufungwe!
 


Kiranja, hivi wewe ni JF Senior Expert member kweli? sasa hii ndo nini? Weka taarifa hapa bana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…