Rostam: Mimi nilikuwa mfanyabiashara wa kwanza kuingia bungeni, nilizua kasheshe sana na nilikuwa na uchaguzi mgumu

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mimi nilikuwa mfanyabiashara wa kwanza kuingia bungeni, wakati huo fomu za bunge za kugombea ubunge zinabox mbili awe mkulima au mfanyakazi mimi nilikrozi zote mbili nikaandika mfanyabiashara, kwahiyo nilizua kasheshe kwenye kamati kuu ya chama wanabishana sasa huyu tunafanyaje kwa sababu si mfanyakazi wala mkulima. Siku wakabishana na hatimaye wakakubali sekta binfasi, biashara ndio tunako kwenda kwahiyo nivuziri kupata wawakilishi, Amesema Rostam Aziz
Your browser is not able to display this video.
 
hivi aliingia bungeni kabla a.gulamali kweli? ...
 
Nadhani hili ndio wengi hawakulijua

Rostam Aziz ndiye mfanyabiashara wa kwanza kuwa mbunge wa Bunge la JMT

Rostam ndiye mbunge aliyeingia bungeni wakati mfumo wa vyama vingi nchini ndio mpya kabisa 1994 akishinda a na nguli wa Siasa za Upinzani nchini Mzee Mapalala wa CUF na Mzee Kasela Bantu wa UDP kwenye Uchaguzi mdogo baada ya Mbunge wa Igunga kufariki

Rostam Aziz kwenye Fomu ya Ubunge ya CCM yenye vibox viwili 1. Mkulima 2. Mfanyakazi alikata vibox vyote viwili na kuandika Mfanyabiashara

Kamati kuu ya CCM ilikaa kwa Siku mbili kutafakari iwapo wakubaliane na Hoja ya Rostam ya kuruhusu u Wafanyabiashara Bungeni ama la na Hatimaye Kamati kuu kwa kauli moja

Rostam aliingia bungeni kwa Uchaguzi mdogo 1994 na alipoondoka 2011 alisababisha Uchaguzi mdogo

Ahsanteni sana 😄🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…