Rostam ni mtu mwema sana, kama uliweza kufadhili Royale Tour, tulipie na deni la Taifa Trilioni 116 tafadhali

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,937
Reaction score
41,161
Salaam!

Tulipata msiba wa kufiwa na baba yetu, kiongozi wa shamba letu,


Hata hatujapoa, akaibuka kibopa,tajiri mmoja mkarimu sana mwenye tabasamu la Mamba Rost Tamu,akaipenda familia yetu, akaahidi kutupenda Sisi na mama etu bila kutubagua.

Aliweza kummsaidia sana mfiwa mamaetu kwa kumpeleka kutalii na kuigiza movie ya Royal Tour Ili kuondoa stress. Na akalipia bills zote. Tukamshukuru.

Kilichotushangaza ni kuwa,kabla hata ya kuanza kupata faida za royale tour, tulishtushwa kusikia habari ya madege makubwa kutua mbugani na kusomba wanyama wetu ambao mfiwa alipiga nao picha aliporekodi movie ya Royale Tour, sasa tukajiuliza, wakija watalii, waone Nini?

Tuache mambo mengi.

Ndugu Rost Tamu tafadhali tulipie deni letu la taifa Trilioni 116 tafadhali, maana inaonyesha una mfuko mkubwa mpana sana usokauka.

Twakuomba tafadhali tulipie deni

Nawasilisha 🙏
 
Tunakuomba,

Waongezee mshahara askari na walimu wetu tafadhali
 
Jamaa anapaswa anyongwe , kunaeneo kama Taifa yafaa ifike level ya kumtambua na kukabiliana na adui wa Taifa letu kwa macho makavu .

Kinachofanywa na mtu kama Polepole kwa tafasiri yoyote ile ila bado nikitendo cha kizalendo mnooo .

Tusipochukua hatua ipo siku hili Taifa litabakia kama kopo tu ,jamaa wanakomaa nakulinyonya tena usiku na mchana
 

I know Pablo Escobar ,The Real Noriega He owes me hundred favor.
 
Mwenye pesa kunyongwa SI rahisi,

Pesa yake itakata kamba.
 
Hata akilipa deni la taifa kwasasa watu mtataka na roho yake.
 
I know Pablo Escobar ,The Real Noriega He owes me hundred favor.
nilisoma story ya pablo kutoka kwa kaka yake, nikajikuta nampenda sana yule jamaa...

jamaa alikua mpambanaji...

mtu mwenye matumizi mazuri ya akili...

mwana mikakati mzuri...

na aliyependa watu...

pablo hakuwaza kusaidia watu, alisaidia kadri alivyoweza...

kuwajengea nyumba, kusomesha, kugawa pesa...

kabla sijasoma ile story, nilikua nimesoma ile ya cali cartel...

mle wamemchafua sana pablo...

nilichojifunza, tunamjua mtu kwa kusikia kutoka pande zote...

kwa waliompenda na kwa waliomchukia...
 
Ametupiga kwenye gas ya kupikia ya 15 kg kwa shs. 57,000 wakati bei ya gas nchi nyingine ipo chini sana. Kibaya zaidi Taifa Gas imeingizwa na serikali kwenye "Nishati safi project" na gas inayotumika inatoka nje ya nchi kwa pesa kidogo zile za kigeni tunazohitaji sana. Watanzania wengi hawaelewi, Mitungi ya gas inagawiwa kila mahali kama project ya serikali hata ikiisha tutakuwa wateja wa Rostam milele, ataendelea kuwa Billioni kupitia migongo ya watanzania, (Sawa hatukatai tukiwa wateja wake, lakini tunapigwa kwa bei) natural gas kwa kawaida inapaswa kuwa na bei ndogo. Hiyo 57 Kg kwa kg 15 ni bei kubwa sana. Siyo hivyo tu, kwenye Vodacom na kampuni nyingine za simu, tunaonewa bei ya bundle ni kubwa na kabla hujatumia bundle zinaisha haraka haraka.
 
Rost Tamu Aziiv kaiweka mfukoni 'sirikali' ya chura kiziwi, kwa msaada wa mhuni wa Msoga!!.
 
Chungeni kama TAIFA mcje kuvuliwa ubingwa sw
Kazi ni kipimo cha utu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…