Hoja ya Rostam haina kichwa wala miguu.
1. Ukiondoka nchini kwako, passport yako inagongwa muhuru (EXIT) na tarehe ya kuondoka.
2. Nchi unayokwenda, unapoingia, airport immigration officials wanagonga - baada ya kuthibitisha VISA yako - muhuri wa kuingia (ENTRY) wenye tarehe hiyo
3. Unapoondoka ugenini, unagongewa muhuri wa kuondoka (EXIT), wenye tarehe hiyo ya kuondoka
4. Unaporejea kwako unagongewa muhuri wa kuingia (ENTRY), wenye tarehe hiyo uliyofika
Rostam anatuonesha passport yenye mihuri miwili, ya KUONDOKA na KUINGIA Tanzania. I wapi mihuri ya KUINGIA na KUONDOKA Afrika Kusini?
Bila hiyo mihuri, HANA UTHIBITISHO kwamba ni KWELI alisafiri!
Imekula kwake! Asitufanye sisi wajinga! MPEKEKEENI HII AKASOME!
-> Mwana wa Haki