Rostam: Umasikini siyo jambo la kujionea fahari

Ana hoja nyingi nzuri kwa mustakabali wa ukuaji wa biashara nchina na uwekezaji wa ndani. Kusikiliza kila upande ni muhimu kuliko kujifungia au kujichagulia upande wa kusikiliza.
Ni kweli,mimi nilicheza nae utotoni maana wazazi wetu walikuwa na urafiki,tulipotezana mimi nilipoenda kusoma na yeye pia ajaenda uingereza.Japo namzidi elimu simfikii kwa utajiri,ujanja wa kibiashara,nampongeza sana kwao kule igunga anasomesha watoto wa familia maskini na ameleta impact kubwa sana kwenye nchi.Japo kuna watu huwa hawapendi kusikia lolote kuhusu huyu mtu na ukiwaulizo kwanini,watakujibu mwizi,kaiba nini hawajui
 
Je, amezitaja hizo kampuni kwa majina? Pili, hizo kampuni za Uingereza na Australia ni za wazungu au wabongo? Maana kuna wabongo wanasajili makampuni huko nje kisha zinakuja kutubamiza hapa nyumbani.
Ni za wazungu na zinamilikiwa na watu wa nje, Amezitaja ikipata wasaa msikilize
 
Bad enough, hawapendi pia kumsikiliza anapoongea.
 
Arudi kwao Iran aone kama Ayatollah Khamenei atamchekea kwa ufisadi anaofanya
 
Bad enough, hawapendi pia kumsikiliza anapoongea.
Bro,huwezi kuamini nikikwambia rostam kazaliwa kijijini mwisi,wilayani igunga,kwenye nyumba ya matope na bati masufuria,pengine wengi wanaomtukana wamezaliwa pazuri kuliko yeye,baba yake alikuwa ni mtu mwema,alikuwa ana duka na gari hapo kijijini,kila mwanakijiji wa hapo alikuwa anamjua,katika ukoo wao ndugu zake wote wamesoma sana,mwenye elimu ndogo yaani digiree moja ni yeye tu.Anyway mimi naangalia tu wanavyomsema,na huwezi kuamini sijawahi kukutana nae tena toka wakati huo tukicheza pamoja na pengine tukikutana hatanikumbuka
 
Na shida ya maskini Huwa wanadhani wakiwachukia matajiri basi umaskini wao utaondoka.

On top of that Maskini wamedanganywa kwamba tiketi ya kuingia mbinguni ni kuwa maskini eti Tajiri hawezi kupenya 😂😂

Na waliowalisha hizo pumba wao ni matajiri wanaishi vizuri.

Kina Mwalimu Nyerere walishawajaza watu pumba hizo Ili wawatawale vizuri ndio maana Sasa Kila maskini anaitwa mzalendo na mwenye pesa anaitwa fisadi.

Better Kuitwa fisadi tena papa kuliko kuwa fukara.
 
Tatizo letu tunafocus na upande mmoja tu, Mimi simfahamu kabisa Rostam ila ninamsikiliza.
 
Una hoja nzuri katika maelezo yako
 
Hana uwoga wowote maana kila kona ya nchi kuna madili yake mizigo ina flow tu
Msikilize, ameshauri vizuri sana hata katka masula ya mikopo ya wafanyabiashara na wawekezaji wa ndani pamoja na kuunganisha Benki zetu Ili ziwe na nguvu na uwezo.
 
Msikilize, ameshauri vizuri sana hata katka masula ya mikopo ya wafanyabiashara na wawekezaji wa ndani pamoja na kuunganisha Benki zetu Ili ziwe na nguvu na uwezo.
Huyu ni miongoni mwa mafisadi papa waliotajwa na mengi kipindi hicho kabla ya vuguvugu la sasa ni vigumu kutenganisha ushauri wake mzuri na mtego wa kutupiga
 
Huyu ni miongoni mwa mafisadi papa waliotajwa na mengi kipindi hicho kabla ya vuguvugu la sasa ni vigumu kutenganisha ushauri wake mzuri na mtego wa kutupiga
Ila ni haki yake ya msingi kabisa kusikilizwa, tumsikilize
 
Hili ni tatizo la kutokuongelea issues moja kwa moja kwahio uwezekano wa kuhamisha magoli au kujikita kwenye symptoms badala ya root causes...

Ingekuwa watu wanachukia masikini kwanini kila siku wasingewakaba kina Bhakresa, Mo hata achana na hao ma tycoon hata wenzao ambao kwa nguvu zao wameweza kujitoa hapa mpaka pale (mfano madogo wasanii)

Issue hapa kubwa kwanza kabisa ni Uwazi / Transparency; ambayo haipo kwenye Mali ya UMMA haijalishi kama anauziwa mu-Australia au Mmasai (kuwepo na Uwazi) na kama ni vitu ambavyo ni commanding Heights za Uchumi au vinatoa huduma moja kwa moja vibaki mikononi mwa UMMA.

Mbili kuna maswali muhimu ambayo hayakujibiwa mfano kama ni kweli anafanya lobbying kwa ajili ya biashara zake zinazomsaidia yeye na kuwadidimiza wenyenchi / wananchi; Mfano suala la Serikali kupigia chapuo mitungi ya gesi badala ya kumalizia na kuwekeza kwenye miundombinu ya UMMA mfano Umeme ili bei zishuke kwa ajili ya wote lakini tunapigia chepuo vitu kwa manufaa ya mtu sababu tu amefanya lobbying...; Hili jambo halina Uhai kwa Taifa na sio Tanzania tu watu kama hawa wapo nchi nyingi mfano kina Gupta Family huko Africa Kusini; Oligarchs walivyojitwalia mali za Warusi n.k.

Kwahio maswali ambayo angeulizwa ni kama la Chapuo za Kupigia Gesi / Nishati Safi; au Mikataba iliyosainiwa kipindi hiki ni ipi na kama ina maslahi kwa taifa na kwanini kusiwe na Uwazi...

Better Still tujiulize ni mfumo gani wa Uongozi tunautaka sababu huu wa kufanya lobbying hata USA (angalau wenyewe wana Taasisi zenye nguvu kidogo kuliko sisi, ila bado unawatafuna)


NB: Tusibadilishe hizi hoja zikawa baina ya wapenda Umasikini, Masikini na Matajiri (Divide and Rule) bali tuungane kuhakikisha hakuna loopholes za kuweza kutumia na wahujumu Uchumi / Walamba Asali... kwa detriment ya UMMA na vizazi vinavyo
 
Ni kweli kabisa umasikini si jambo la kujivunia hata kidogo, kuna mwanamziki mmoja wa Reggae aliwahi imba kuwa 'To be poor is a crime' na I agree with him, lakini kuwa tajiri kwa kufukarisha wengine kwa maksudi ni crime pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…