Royal Oven hongereni kwa huduma nzuri ila mapungufu yapo.

Royal Oven hongereni kwa huduma nzuri ila mapungufu yapo.

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Customer service au huduma kwa mteja ni sehemu nyeti sana ya biashara yoyote duniani, ni kioo cha mwanzo cha biashara iwe inafanya kuuza bidhaa au kutoa huduma. Kuna baadhi ya makampuni ili wakupatie ajira basi lazma uwe na vigezo kama uso usio na chunusi, uso nyororo na mwenye umbo namba nane. Kama wanakutegemea wewe kwenda kuwa sura ya biashara basi watakutazama kila angle ili tu usije kuharibu.

1726992040282.png


Makampuni kama L'Oreal, Nivea, pamoja na Coty ni lazma uwe na mwili mzuri sana ili wakupe ajira. Kama umejaa jaa kama kifutu utaishia kusikia wenzako wamepata ajira. Ni standards ambazo wao wameona ni bora katika biashara zao. Ili uweze kumshawishi nteja kununua bidhaa za urembo basi lazma nawe uonekane mrembo hata kama kuna makeups ila basi uoneshe urembo na uwe na kiwango cha juu ya kuuza muonekano wako kwa mteja apate kununua bidhaa hizo.

Basi Jana Jumamosi nikaona ni vizuri niwapeleke out watoto wapate kuosha macho mjini, katika pita pita nikajisemea ngoja niende Royal Oven Mwanza City Centre karibu na Mwanza Hotel pembeni kabsa na Gold Crest Hotel. Ni sehemu nzuri ya kimkakati haswa katika kufanya biashara kwani kuna mzunguko mkubwa wa watu. Kusema ukweli Royal Oven hongera kubwa sana katika huduma zenu. Haya ni baadhi ya mambo ambayo nimepata kukutana nayo na sio mara ya kwanza:
1726991766099.png


1. Parking yenu ina eneo kubwa ingawa sio sana ila management yake haipo vizuri sana, watu wanaegesha magari katika utaratibu ambao sio mzuri. Ni kawaida kukutana na mlinzi akiwaelekeza watu watu namna ya kuegesha magari ila wakati wa kutoka inaleta taabu sana, kumbuka kuwa nyuma ya Jengo la Royal Oven kuna barabara ya Makoroboi inayoelekea Roundabout ya Samaki. Wekeni utaratibu wa kuegesha magari vizuri, wateja wapate huduma.

1726992184468.png


2. Ongezeni sehemu ya Jiko lenu, Royal Oven mmekuwa mnapata orders nyingi kiasi kwamba wapishi hao wawili wanazidiwa. Nilitoa order yangu kwa zaidi ya lisaa limoja huku nikiona wapishi wakihaha huku na kule kwa butwaa. Najua kuwa mnazingatia usafi katika kuandaa chakula ila wapishi wenu wanazidiwa na order.

3. Royal Oven mko vizuri sana kwenye matumizi ya teknolojia kama malipo kwa QR Code pamoja na Lipa Namba ila tatizo ni kwamba kuna mdada anayepokea order aisee dada ni mhuni sana. Huyu dada anafanya vitu vya ajabu sana, ukitoa order anakusubirisha huku akichukua order za watu wengi na yeye anapata commission.

1726992393004.png

Mara kadhaa watu wamekuwa wakilalamika kuwa huyu dada anawapatia kipaumbele wahindi na wazungu. Ongezeni wadada wawe wawili wanaopokea order pale jikoni.

4. Ndani sasa, wadada wengi wanatumia muda mwingi kupiga soga pekee. Ukiuliza bei ya chakula mfano, Mkate au Keki basi unapewa jibu kamilifu kwa maana usiulize tena. Wapo baadhi wanajibu kwa kisirani kiasi kwamba yeye ndo analipia chakula hicho. Ila akifika mzungu au mhindi ndo wataanza kuwa wanyenyekevu. Wafundisheni namna ya kumkarimu mteja, hata kama amekwenda kununua mkate basi atoke amenunua keki na sharubati.

1726992809660.png


Mwisho, Royal Oven angalieni msije kupata competition kali sana, mkapoteza wateja. Tengenezeni mazingira mazuri na mahusiano bora na wateja wenu maana kuna watu wameanza kuja kwa kasi sana kwenye kutengeneza Pizza, na mikate kama nyie. Gold Crest, Adden Palace nao wapo sokoni kutengeneza Pizza. Binafsi nikipewa nafasi ya kuwapatia rating basi bila kinyongo nawapa 3.1 katika 5.
SIO KWA UBAYA!​
 
Back
Top Bottom