Hizo mambo, what do they have to do with watalii?!.
P
Kama wewe ni mtaalam wa habari unajuwa mengi kuhusu marketing, culture, timing, quality and clarity ni vitu muhimu kwenye kufanikisha biashara:
1. culture: Unapokwenda kutafuta wateja/habari sehemu fulani lazima uzingatie utamaduni wa sehemu ile. Royal tour imekwenda kuzinduliwa Marekani, jee, wamarekani wana utamaduni gani kwenye mavazi, dini, siasa, demokrasia, lugha na tabia zao? Je, alivyovaa Mama Wamarekani vinawavutia au angevaa kama wao au kitalii?, je, siasa za Tanzania zinawavutia Wamarekani?, nk.
2. Timing: Tanzania tuna watalii ambao wamekwama kurudi kwao kwasababu ya Vita ya Ukraine mpaka sasa wapo. Dunia nzima focus yao kwa sasa hivi imeelekea kwenye vita ya Ukraine na urusi, maisha yamepanda na uchumi wa dunia unashuka kote duniani ikiwemo marekani. Je, huu ni muda mwafaka kwa sisi kwenda kutangaza utalii Marekani?, Kama Marekani ndiyo mfadhili mkuu wa Ukraine kwenye vita yake na Urusi, je kwenda marekani kipindi hiki cha vita kutangaza utalii wetu kunauweka wapi uhusiano wa Tanzania na Urusi, Belarus, N.Korea na pro-Russia wote kwenye mzozo huu?
3. Quality: Je, viwango vya huduma zetu za utalii vinalingana na expectations zao? ni kama za mshindani wetu yupi?, rule of law and democracy ipo.
Clarity: Je, tuyoyasema kwenye royal tour tunayaishi, ni kweli tuko na iko hivyo? tunaeleweka? wanatuelewa? tunaaminika? hatugeukigeuki? leo ni kama kesho au kisho ina mambo yake?
Maswali haya yalipaswa kuulizwa na watanzania wote na kujibiwa na Wizara ya maliasili na utalii na washauri wa mama wote.