Royal Tour kuzinduliwa rasmi 18 Aprili 2022 New York

Royal Tour kuzinduliwa rasmi 18 Aprili 2022 New York

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
KESHO NDIO KESHO, ROYAL TOUR KUZINDULIWA RASMI NEW YORK- MAREKANI.

Na Bwanku M Bwanku.

Kesho ndio Kesho, Jumatatu Aprili 18, 2022 Dunia nzima itasimama wakati Filamu Maalum ya kutangaza Utalii wetu wa Tanzania ikizinduliwa pale New York, USA. Mhe. Rais Samia ni Mhusika Mkuu (Tour Guider) kwenye Filamu hii inayokwenda kueleza kila Vivutio vya Utalii na Uwekezaji vilivyopo nchini ili kuwavuta Watalii na Wawekezaji wengi zaidi Ulimwenguni kuja nchini ili tupate fedha nyingi zaidi kupitia Utalii na Uwekezaji ili tuzipeleke kwenye Uchumi na Maendeleo yetu. Kesho ndio kesho Ulimwengu utasimama na Tanzania.

Mhe. Rais Samia kwasasa ni Mwanamke anayetajwa kuwa na ushawishi mkubwa zaidi Barani Afrika na Duniani kwa Mujibu wa Majarida ya Avance Media la Ghana na Jarida la Forbes, hivyo uamuzi huu wa kurekodi Filamu hii ya Kutangaza Utalii wetu itafanya Ulimwengu mzima kutazama na kufuatilia Filamu hii na kujionea uzuri wa Tanzania na kumiminika kwa wingi kuja nchini. Watanzania wote Mabibi na Mabwana tuiunge mkono Filamu hii, inakwenda kutusaidia kupandisha idadi ya Watalii kutoka chini ya Milioni 2 wasasa mpaka kufikia Milioni 5 kufikia mwaka 2025 kama ilivyo Mipango yetu ya Ilani ya CCM inayotekelezwa na Taifa na Mipango yetu. Baada ya Kuzinduliwa New York, Filamu hii itazinduliwa pia Los Angeles Aprili 21, Dar es Salaam Aprili 28 na Zanzibar Mei 07, 2022.

Bwanku M Bwanku
bwanku55@gmail.com.

IMG_20220417_141024_897.jpg


dktabbasi~p~CcRNBpYrhXb~1.jpg
 
Why Mmetumia hela nyingi sana mnajua 8Bilion Ni mkwanja mrefu sana kurekodi tamthiliya 1 ya utalii!!!!
 
Mama Tuvushe Siye
Utuletee Vijipesa Kidogo
 
Mkitoka huko mje mvunje FAO LA KUJITOA NSSF maana kapu litakuwa zito.....
 
Nani anamfahamu mama Samia mpaka akitangaza utalii watu wavutiwe? Hadi tunavyoongea watalii wanaokuja ni wale wanaoletwa na tour agents wetu wa kawaida, na sio huo utapeli wa bibi ushungi.
 
Yule wa Chalinze ameshapata mwanafunzi. Yaani NI kukata anga, piga picha, tengeneza movies, majira na jamvi la Habari wanaongeza utamu, mei mosi inatoka hotuba ya ahadi na nchi inapata maendeleo na CAG anatoa ripoti Safi kabisa.
 
Back
Top Bottom