ANAUPIGA MWINGI
JF-Expert Member
- Apr 14, 2022
- 389
- 757
Mwaka huu Tanzania ilikuwa na kampeni kubwa sana ya kutanga utalii Duniani na kwenye hio kampeni inayo enda kwa jina la royal tour ilizinduliwa Marekani ambapo ndo kitovu cha utalii Duniani na pia likiwa ni taifa linalo toa watalii wengi sana Ttanzania na wenye mafuta kama waongoza watalii wanavyo waita.
Mafanikio ya royal tour ni pamoja na kuongeza kiwang cha watali wanao tembelea Tanzania, na kwa kweli watalii ni wengi sana kwa sasa, na tunashuhudia idadi kubwa ya watalii wakitembelea vivutio mbali mbali vilivyoko hapa Tanzania, hasa kwenye hifadhi za Taifa na pia kule Zanzivar.Watalii hawa hutuletea pesa za kigeni ambazo hutusaidia sana kuagiza bidhaa nje ya nchi hasa Asia na Ulaya na Marekani pia.
Watalii hawa wanao kuja kutembelea hifadhi za taifa, hawabebi vyakula vyao kutoka Ulaya, Marekani na Asia bali vyakula huja kuvikuta huku, vyakula huvikuta sisi tunacho fanya ni kuwapikia kwa kiwango kile cha kule kwao.
Je sisi kama vijana tunachangamkia vipi hii furusa ya uwepo wa idadi kubwa ya watalii Tanzania kwa kuzalisha vyakula vya kuwalisha hawa watalii?Hoteli zilizopo Zanzibar, Dar na Arusha na hifadhini wanahitaji tani na tani za vyakukula vya kuwalisha hawa watalii, vyakula hivyo huchukuliwa kwenye masoko yetu il kiwango kikubwa huagizwa nje ya nchi.
Ni kawaida sana kuona pale Arusha vyakula vinavyo fungwa kupelekwa Mahoteli ya kitalii vingi vinatoka nje ya nchi, nikawaida kukuta asilimia 99 ya matunda yanayo tumika kwenye hoteli za utalii yanatoka nje ya nchi, vitu kama nyama zipo zinazo toka nje, Uyoga, mbogaza majanai na kadhalika.
Je sisi kama sisi ni kwamba hatuzioni hizi furusa? Au ni hadi Mh Bashe au Mamama Samia atuambie kwamba tulime ili kuwalisha watalii? Kenya inafaidika sana na Royal tour kukiko sisi make hawa ndio wanao lisha Arusha vyakula vya Watalii.
Tunaweza sana wekeza kwenye aina mbali mbali za vyakula na matunda ya kulisha watalii, na tambua sio kila aina ya matunda au mboga mboga basi zinatumiwa na watalii hapana;
Uzalishaji wa Nyama hasa za kuku na mayai – Hizi hoteli zinatumia sana nyama ya kuku na mayai, hiki ni chakula kinacho liwa sana na watalii mahotelini, hizi ni nyama za kuku wa kisasa na mayai yake ya kisasa, hapa ni sehemu ambayo tunatakiwa kuzalisha zaidi ili tuwee kulisha wageni.
Mbogamboga- Kiwango kikubwa cha mboga zinazo tumika kwenye hizi hoteli zinatoka nje ya nchi, nchi kama South Africa, Kenya na Egypt, kwenye mboga ni sehemu ya kuwekeza hasa ili kuweza kulisha idadi kubwa ya watalii wanao kuja Tanzania kwa sasa.
Matunda- Hapa ndio sehemu tunayo feli kuliko sehemu zote, asilimia 99 ya matunda yanayo tumika mahotelini yanaoka nje ya nchi, tuna aridhi tuna maji lakini kwa nini matunda yote haya yanatoka nje? Jibu ni kwamba baadhi ya matunda yetu sisi kama machungwa hayana viwango vya kulisha watalii.Matunda yetu mengi kama Machungwa, zabibu, maembe, limao, Chenza, Strawberry, Blue berry na mengineyo yote yanatoka nje kwa sabau sisi tunayo zalisha hayana kiwango kabisa.
Vitu kama Uyoga ni aina ya vyakula ambavyo vinatumiwa sana na wageni Mahotyelini ila vinatoka nje ya nchi.
Hivi vyakula sio lazima uwe unaishi Dar, au Arusha au Moshi kwamba ndio uzalishe hapana, nchi yetu ina miundo mbinu ya kutosha kabisa kwa sasa, hivi vyakula unaweza zalisha ukiwa hata Mbeya, Iringa, Bukoba, Mwanza, Mara, Tanga, Singida au Dodoma na ukasambaza Arusha, Dar, Zanzibar na Moshi, kama machungwa yanatoka Misiri na yanafika Tanzania kwa nini wewe uamini lazima ukae Arusha ndo ulime mboga za kulisha Watalii?
Kikubwa kinacho paswa kufanywa na wewe ni kujua aina ya Vyakula kwa ajili ya watalii, ni aina gani za Mboga wanapendelea, ni aina gani za matunda wanapendelea, na hizi aina je naweza zilima hapana nilipo na je naweza zisafirisha hadi maeneo husika? Ukisha jua aina za matunda na mboga kinacho fuata ni kuangalia wanunusi ambao mara nyingi ni wale supplier wa kwenye mahoteli ya kitalii na uzuri hapa ni kwamba mboga na matunda utakayo zalisha pia utayauza na kwenye Super Market Kubwa.
Mboga na matunda yanatoka Kenya na yanakuja kwa njia ya barabara hadi Arusha, sasa ni kwa nini wewe ulieopo Mwanza au Singida hapo au hapa hapa Arusha ushwindwe kuzalisha kwa ajili ya Watalii? napia kwa ajili ya watu wasio watalii.
Hizi furusa tuzitumie vyema sana, kwa sababu watu kama Wakenya wako shapu sana na kuna ambao wanakuja hadi Tanzania wanatafuta mashamba wanalima aina hizi za mboga mboga za kulisha watalii, tuache kulalamika tuchukue hatua na tufaidike na huu utalii wetu.
Ni ajabu sana kwamba vitu kama Machungwa yanatoka Egypt sisi yale machungwa yetu ya Tanga hayana viwango na ni kweli hayana vinwago sio uongo ni kweli kabisa, vitu kama Starwberry rahisi kulima zinatoka South Africa, mboga mboga baadhi zinatoka Suth Africa, nyanya zinatoka Suoth Africa, Uyoga unatoka Kenye. Hii ni aibu kubwa sana kwetu sisi na wala hakuna wa kumulamu, make wengi tunapenda sana kulaumu Serikali, kwa sababu hata huko Kenya wanao lima sio Serikali ya Kenya inalima ni Wakenya wenyenyewe wanalima, huko South Africa sio Serikali ya South Africa inalima ni Raia wanalima, I weje sasa sisi tuseme serikali?
Royal tour inaweza kuwa na faida sana kwenye kilimo kuliko hata kwenye nyanja zingine sema sisi bado hatujaziona hizo furusa, na hizi hoteli zinazo agiza nje si kwa sababu hawatupendi hapana ni kwa sababu hatuzalishi vitu vya maana, na pia hazina ubora wowote, ni kivipi uchukue yale machungwa ya Tanga machachu kama limao ukalishe Watalii?
Tuchangamkie furusa wakuu, kuna siku hazitakuwepo, bora ujariu useme nilijaribu nikakosa soko kuliko kuto kujaribu na kuishia kulalamika tu.
‘’Excuse will always be there for you. Opportunity won’t.’’

Upvote
1