Royal Tour: Yanayosemwa, yasiyosemwa na yanayodhaniwa

Royal Tour: Yanayosemwa, yasiyosemwa na yanayodhaniwa

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Naomba nishare nawewe alichokisema kaka yangu James Gayo kwa maneno haya.

Kinachosemwa huku mitaani ni kwamba, Tanzania imetengeneza sinema (Wengine wameiita tangazo na wengine makala) ya Royal Tour ili kuvutia utalii na Rais wa Tanzania ndiye mwigizaji mkuu. Kwa kauli hiyo inadhaniwa kuwa huu ni mradi wa Serikali.

Kisichosemwa ni kwamba, kampuni ya Check Six Production ya Califonia ndiyo iliyotengeneza Royal Tour Tanzania na kumshirikisha Rais wa Tanzania! Kwa kuwa haisemwi pia kuwa, Royal Tour kadhaa zimeshatengenezwa kwingineko duniani, inadhaniwa kuwa Royal Tour Tanzania ni ya kwanza!

Haisemwi pia kuwa, kabla ya Rais Samia kukubali kushiriki, watayarishaji wa Royal Tour walipata kuwashawishi Rais Kikwete na Rais Magufuli bila mafanikio.

Kwa kuwa inasemwa kuwa ni “sinema” na kwamba Rais “amecheza”, inadhaniwa kuwa ni sinema!

Kisichosemwa (pengine kutokana na uhaba wa msamiati) ni kwamba, Royal Tour, si sinema. Kama ambavyo hatuwezi kuviita vipindi vya Big Brother, isidingo, mada moto na Bongo Star Serach sinema, hatuwezi kuiita Royal Tour sinema—ni kipindi cha Runinga.

Ndio maana hata wasanii wetu wa Bongomovie hawajiiti tena waigizaji wa sinema siku hizi: Ukikutana nao na kuwauliza kama bado wanaigiza sinema hujibu, “hapana, siku hizi nimehamia kwenye tamthilia”.

Waliotuletea sinema wana ufafanuzi mrefu wa kuitofautisha sinema na vipindi vya runinga.

Huku yanayosemwa yakiendelea kuzua maswali kama: “Serikali imetumia kiasi gani kutengeneza Royal Tour? Hatimiliki ya sinema ni ya nani?” Serikali haifanyi juhudi zozote kutoa ufafanuzi wa yasiyosemwa na kupelekea watu kudhani wanavyotaka!

Hii si mara ya kwanza Tanzania kushiriki kwenye vipindi vya runinga vya kimataifa.

Ushiriki wa Mwisho Mwampamba na Idris Sultan kwenye “Big Brother Africa” ulifuatiliwa na watanzania wengi sana lakini ushiriki wao haukupata kuzua malumbano au kuacha maswali kama tunayoyasikia leo.

Kwanini? Mwandishi wa makala haya ANADHANI, watanzania walikuwa na taarifa nyingi zaidi za “Big Brother” kuliko “Royal Tour”?

CC: James Gayo.
 
Royal tour ni documentary na siyo sinema.

Hakuna duniani documentary ya kuigiza ni kitu halisi.

Siku hizi kwenye harusi zetu mitaani kabla ya siku ya harusi aliyechukuwa tender ya video uwafanyia mahojiano wazazi na maharusi hayo huwezi kuita maigizo ni vitu reality.

Tanzania imejaa majitu majinga sana ni bora hata population tungekuwa watu million 10 wenye akili kuliko tupo million 60 halafu wajinga ni three quoter.
 
Back
Top Bottom