Rozay mbona hajapost waka waka ?

Ku post au kuto post inaweza kuwa na mantiki kutegemea na namna mtu anavyojisikia.
Ni mara kadhaa sasa Rozay amekuwa hapost hata nyimbo zake binafsi anazotoa.
Tumeshuhudia wimbo wake mpya wa 'Tiptoe' amekuwa hapost kabisa.
Na si nyimbo zake tu hata za wasanii wake pia.
 
Kabla hatuhukumu tunatakiwa kuangalia trend. Nitawakumbusha....

Diamond ali-post Waka usiku ambao kwa US ni mchana. Siku ya pili East Africa, Diamond akaanza ku-promote ngoma yake na wakati huo kwa US ni usiku!

Wakati Diamond akihangaika ku-promote ngoma yake, mara aka-post taarifa za kifo cha Black Bo. And remember, kifo kimetokea wakati RickRoss akiwa Miami na yeye Ross alitangaza habari za kifo hicho akiwa Miami kwenye event. Na hata ukiangalia page ya RickRoss, post zake za mwisho mbali na post za msiba ni zile zilizohusu event ya huko Miami!

Hii maana yake nini?! Wakati Diamond anaachia ngoma, RickRoss yupo kwenye hiyo event. Lakini hata kabla event haijaisha, RickRoss anapata taarifa za kifo cha Black Bo. Na Black Bo na RickRoss ni kama Diamond na Babu Tale au hata Sallam!

Sasa hapo tunatarajia awe anatoa post za ku-promote collabo wakati anaomboleza kifo cha mtu wake wa karibu?! Na tangu siku hiyo, RickRoss haja-post chochote mbali na habari za msiba wa Black Bo ambao kwa mara ya kwanza ali-post Instagram siku mbili baadae. And I can bet, Diamond alipata taarifa za kifo cha Black Bo kupitia kwa RickRoss na ndio maana ali-post mapema sana hata kabla habari zenyewe hazisambaa!!
 
Watu wanachosahau hapa ni kwamba release ya ngoma ya Diamond ilifuatana na kifo cha Black Bo, Meneja wa RickRoss. Na tangu kutokea kifo cha Black Bo, RickRoss hajawahi ku-post chochote mbalimbali na habari za hicho kifo!! In short, jamaa anaomboleza huku watu tukihoji kwanini ha-post wimbo wa Diamond!!
 
Hivi vifo vyote ambavyo tuna-post na kutoa RIP wahusika tunawafahamu?! Licha ya kwamba Diamond na Black Bo wameshawahi kukutana; hivi hata kama ingekuwa hawajawahi kukutana, hudhani kufahamiana kwa Diamond na RickRoss kulitosha kabisa Diamond kuonesha support kwa RickRoss? Btw, RickRoss kuna chochote alichowahi ku-post tangu kutokea kwa kifo cha Black Bo mbali na habari zinazohusiana na Black Bo?! Au kwa akili yenu mnadhani Wamarekani hawaumii au hawaombolezi wanapoondokewa na watu wao wa karibu?!

Bora basi ungeona RickRoss akiendelea kufanya posting ya mambo mengine ya kidunia lakini hajafanya hivyo hata mara moja tangu kutokea kwa msiba!
 
Rick Ross apost huo wimbo ili iweje?

Kwanza ni nani Marekani anaujua huo wimbo?

Urban station ipi ambao huo wimbo upo kwenye rotation?

Rick Ross wala hahitaji kabisa kuu promote huo wimbo.

Huo wimbo mnaushobokea huku tu kwa sababu ya huyo Rick Ross.

Mngejua jinsi Wamarekani wasivyojua chochote na wasivyo na raghba na miziki wa kwingineko wala msingehoji.
 
rich babe ameongea!
 
Wale wamarekani ndio walivyo hata Meek Mill hakum-sapoti Davido....Mkishafanya Collabo yaliyobaki ya kwako
 
Basi mkuu watu wa Madale wanadhani huo wimbo huko Marekani unatamba kweli kweli
 
Basi mkuu watu wa Madale wanadhani huo wimbo huko Marekani unatamba kweli kweli

Hakuna mtu Marekani mwenye Time na huo wimbo!

Hata kwenye top 200 haupo.

Na sijui urban station hata moja iliyoupiga!
 
Account zao ni za kibiashara collabo zinafanyika kibiashara hili mnapaswa mlielewe.

Kwenye mziki kuna biashara nyinhi ambazo aliyepo nje ya mziki ngumu kuzijua.

Rick anapofanya collabo na diamond biashara inahusika na kila mmoja anapima atafaidika kwa namna gani. Kiuhalisia diamond anafaida kubwa kufanya collabo na Rick.

kuhusu kupost au kutokupost inategemea na biashara yao walivyoifanya. Labda walikubaliana biashara ya collabo tu kuingia booth na kwenda location ya video basi.

Mambo ya matangazo dai ajitegemee. Maana kupostiwa kwenye ofisi/account ya mtu lazima ulipe otherwise awe amekukubali yeye aamue kukupa airtime.

Hizi accounts ni ofisi za watu ni biashara za watu sio wanapost post tu kama za kwetu ukitaka kumpost magufuli unaweka lowasa unaweka..yeye akiweka anapima kibiashara itamuathiri vipi.
 
Kuna vitu viwili vinaendesha music hasa hizi mishe za kupost au kutokupost.

Mapenzi binafsi na biashara.

accounts za IG na za kwingineko kwa wasanii ni biashara na pia ni ofisi zao. Hapa kika ofisi au biashara huwa na taratibu zake.

Lakini pia kama mwenzako anamapenzi na wewe kakukubali atakupost bila kujali athari yoyote kwa biashara yake.

Post yoyote kwenye wall ya diamond ni tangazo moja kubwa saana na kwa Rick pia akikupost ni promo moja kubwa. Na wao wanayajua haya hawafanyi bure bure
 
ni kweli mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…